14 Jan
Ni Jinsi Gani Mwanadamu Ambaye Amemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Umeme wa Mashariki

        Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali. Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo. Mbali na Mungu, mwanadamu anapoteza uhai, ukweli na baraka za Mungu, lakini bado mwanadamu hajapokea uhai wala ukweli, na hata baraka kubwa Mungu anazowapa wanadamu. Wanadamu wote wanataka kumpata Mungu lakini bado hawawezi kuvumilia mabadiliko yoyote kwa kazi ya Mungu. Wale wasiokubali kazi mpya ya Mungu wanaamini kwamba kazi ya Mungu haibadiliki, na kwamba kazi ya Mungu milele inabakia kusimama. Kwa imani yao, yote yanayohitajika kupata wokovu wa milele kutoka kwa Mungu ni kuhifadhi sheria, na iwapo watatubu na kukiri dhambi zao, dhamira ya Mungu milele itaridhika. Wana maoni kwamba Mungu anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria na Mungu aliyesulubiwa kwa sababu ya mwanadamu; pia ni maoni yao kwamba Mungu hastahili na Hawezi kuzidi kiwango cha Biblia. Ni hasa maoni haya yaliyowafunga imara kwa sheria ya zamani na kuendelea kuwafumba kwa kanuni ngumu. Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu. Mwanadamu haitafiti kazi mpya ya Mungu kwa utunzaji wala haikubali na unyenyekevu; badala yake, mwanadamu anachukua mtazamo wa dharau, kusubiri ufunuo na mwongozo wa Mungu. Hii siyo tabia ya mwanadamu anayeasi dhidi ya na kumpinga Mungu? Ni jinsi gani wanadamu kama hawa wanaweza kupata idhini ya Mungu?


        Wakati huo, Yesu alisema kuwa kazi ya Yehova ilikuwa imebaki nyuma kwa Enzi ya Neema, kama Nisemavyo leo kwamba kazi ya Yesu imebaki nyuma. Kama kungekuwa tu na Enzi ya Sheria na siyo Enzi ya Neema, Yesu hangeweza kusulubiwa na hangeweza kuwakomboa wanadamu wote; kungekuwa tu na Enzi ya Sheria, kungekuwa na uwezekano wa mwanadamu kuendelea hadi siku ya leo? Historia inaendelea mbele; historia sio asili ya sheria ya kazi ya Mungu? Hii sio picha ya usimamizi Wake wa mwanadamu ndani ya ulimwengu mzima? Historia inaendelea mbele, na pia kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu yanaendelea kubadilika. Haingewezekana kwa Mungu kudumisha hatua moja ya kazi kwa miaka elfu sita, kwani kila mwanadamu anajua kwamba Yeye daima ni mpya na kamwe si mzee. Hangeweza kuendelea kuendeleza kazi sawa na kusulubiwa, na mara moja, mara mbili, mara tatu…. kupigwa misumari kwa msalaba. Huu ni mtazamo wa mwanadamu mjinga. Mungu haendelezi kazi sawa, na kazi Yake daima inabadilika na daima ni mpya, jinsi kila siku Nazungumza nanyi maneno mapya na kufanya kazi mpya. Hii ndiyo kazi Ninayofanya, umuhimu wake ukiwa kwa maneno “mpya” na “ajabu.” “Mungu habadiliki, na Mungu daima Atakuwa Mungu”; usemi huu hakika ni ukweli. Kiini cha Mungu hakibadiliki, Mungu daima ni Mungu, na Hawezi kamwe kuwa Shetani, lakini haya hayathibitishi kwamba kazi Yake ni ya daima na kabambe kama kiini Chake. Unatangaza kwamba Mungu yuko hivyo, lakini ni jinsi gani basi unaweza kueleza kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si mzee? Kazi ya Mungu inaendelea kuenea, na mapenzi ya Mungu yanaendelea kujitokeza na kufanywa kujulikana na mwanadamu. Wakati mwanadamu anakuwa na uzoefu wa kazi ya Mungu, tabia yake inaendelea kubadilika, na maarifa yake yanaendelea kubadilika. Basi mabadiliko haya yanatokea wapi? Siyo kwa kazi ya Mungu inayobadilika milele? Kama tabia ya mwanadamu inaweza kubadilika, mbona mwanadamu hawezi kuruhusu kazi Yangu na maneno Yangu pia kuendelea kubadilika? Ni lazima Nikabiliwe na vikwazo vya mwanadamu? Hutegemei tu maneno ya hila?


        Kufuata kufufuka kwake, Yesu alijitokeza kwa mitume na kusema, “Na, tazameni, Nawatumieni ahadi ya Babangu kwenu: lakini ngojeni katika mji wa Yerusalemu, mpaka mjaliwe uwezo kutoka juu.” Je, wajua jinsi maneno haya yalielezwa? Umepewa sasa nguvu Zake? Umeelewa sasa kile kinachoitwa nguvu? Yesu alitangaza kwamba wanadamu wangepewa Roho wa ukweli katika siku za mwisho. Sasa ni siku za mwisho; je, unaelewa jinsi Roho wa ukweli hutamka maneno? Roho wa ukweli huonekana na kufanya kazi wapi? Hizo roho chafu na roho ovu ni Roho wa ukweli? Hazina haki, wala hata utoaji wa uhai, na huzifuati sheria za zamani bila kufanya kazi yoyote mpya. Hizo ni Roho wa ukweli? Zina uhai, ukweli, na njia? Ziliibuka tofauti kwa dunia? Wale wanaojiweka imara kwa Biblia na kumshikilia kabisa Yesu—mmefuata kazi ya Yesu na maneno Yake? Ni jinsi gani mlivyo waaminifu kwa Yesu? Kitabu kikuu zaidi cha unabii cha Isaya kwa Agano la Kale hakikutaja kwamba mtoto anayeitwa Yesu angezaliwa kwa enzi ya Agano Jipya, bali kilisema tu mtoto mchanga wa kiume angezaliwa kwa jina Imanueli. Mbona hakutaja jina Yesu? Hakuna pahali popote kwa Agano la Kale panapotokea jina hili, hivyo mbona basi mnamwamini Yesu? Hakika hamkumwona Yesu kwa macho yenu kabla kuja kumwamini? Ama mlianza kuamini mlipopata ufunuo? Mungu kweli angewaonyesha neema kama hiyo? Na kuwapa baraka kubwa kama hiyo? Je, ni kwa msingi gani mlimwamini Mungu? Mbona basi hamwamini kwamba Mungu amekuwa mwili siku hii? Mbona mnasema kwamba kukosekana kwa ufunuo kutoka kwa Mungu kunathibitisha kwamba Hajakuwa mwili? Ni lazima Mungu amweleze mwanadamu kabla ya kuanza kazi Yake? Ni lazima apate idhini kutoka kwa mwanadamu? Isaya alitangaza tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa horini lakini hakutabiri kwamba Maria angejifungua Yesu. Mbona basi mlimwamini Yesu aliyezaliwa na Maria? Hakika imani yenu siyo isiyokuwa na uhakika na mkanganyiko! Wengine wanasema kwamba jina la Mungu halibadiliki, hivyo, mbona basi jina la Yehova likawa Yesu? Ilitabiriwa kuja kwa Masihi, hivyo mbona basi mwanadamu kwa jina Yesu alikuja? Mbona jina la Mungu lilibadilika? Kazi kama hiyo haikufanyika muda mrefu uliopita? Hawezi Mungu leo kufanya kazi mpya? Kazi ya jana inaweza kubadilishwa, na kazi ya Yesu inaweza kufuata baada ya hiyo ya Yehova. Haiwezi kazi ya Yesu kurithiwa na kazi ingine? Ikiwa jina la Yehova linaweza kubadilishwa kuwa Yesu, basi jina la Yesu haliwezi kubadilishwa pia? Hii si ya ajabu, na watu wanafikiria hivyo[a] tu kwa sababu ya akili zao rahisi. Mungu daima atakuwa Mungu. Bila kujali mabadiliko ya kazi Yake na jina Lake, tabia na maarifa Yake hayabadiliki milele. Ikiwa unaamini kwamba Mungu anaweza tu kuitwa na jina Yesu, basi unajua machache sana. Unathubutu kudai kwamba Yesu milele ni jina la Mungu, kwamba Mungu milele na daima atajulikana kwa jina Yesu, na kwamba haya hayatabadilika? Unathubutu kudai kwa uhakika ni jina la Yesu lililohitimisha Enzi ya Sheria na pia kuhitimisha enzi ya mwisho? Nani anaweza kusema kwamba neema ya Yesu inaweza kuhitimisha enzi? Kama sasa huwezi kujua kweli hizi wazi, hutaweza tu kuhubiri injili, lakini pia wewe mwenyewe huwezi kubaki umesimama. Itakapofika siku ambayo utatatua matatizo yote ya hao watu wa kidini na kukanusha imani zao za uwongo, hiyo itakuwa thibitisho kwamba una hakika kabisa ya hatua hii ya kazi na huna shaka hata kidogo. Ikiwa huwezi kukanusha imani zao za uwongo, basi watakushitaki na kukukashifu. Hii sio aibu?


        Wayahudi wa wakati huo wote walisoma kutoka Agano la Kale na walijua unabii wa Isaya kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa horini. Mbona basi, na maarifa haya, bado walimtesa Yesu? Hii siyo kwa sababu ya asili yao ya kuasi na kutojua kazi ya Roho Mtakatifu? Wakati huo, Mafarisayo waliamini kwamba kazi ya Yesu ilikuwa tofauti na ile waliyoijua ya mtoto mchanga wa kiume aliyetabiriwa; mwanadamu wa leo anamkataa Mungu kwa sababu kazi ya Mungu mwenye mwili haikubaliani na Biblia. Si kiini cha uasi wao dhidi ya Mungu ni moja na sawa? Unaweza kuwa yule ambaye anakubali tu bila swali kazi yote ya Roho Mtakatifu? Kama ni kazi ya Roho Mtakatifu, basi ni “mkondo” sawa. Unapaswa kuikubali bila wasiwasi hata kidogo, badala ya kuokota na kuchagua nini cha kukubali. Ukipata maarifa kiasi kutoka kwa Mungu na kujitahadhari dhidi Yake, hili silo tendo lisilohitajika? Unachopaswa kufanya ni kukubali, bila haja ya kuthibitisha zaidi kutoka kwa Biblia, kazi yoyote iwapo tu ni ya Roho Mtakatifu, kwani unamwamini Mungu kumfuata Mungu, sio kumchunguza. Hupaswi kutafuta ushuhuda zaidi ili Nionyeshe kwamba Mimi ni Mungu wako. Badala yake, unapaswa kupambanua kama Nina faida kwako; hiyo ndiyo muhimu. Hata kama umegundua ushuhuda usiopingika ndani ya Biblia, haiwezi kukuleta kikamilifu mbele Yangu. Wewe ndiye mmoja anayeishi ndani ya mipaka ya Biblia, na sio mbele Yangu; Biblia haiwezi kukusaidia kunijua, wala haiwezi kuimarisha upendo wako Kwangu. Ingawa Biblia ilitabiri kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa, hakuna yeyote angeweza kuelewa kupitia nani unabii ungetimia, kwani mwanadamu hakujua kazi ya Mungu, na hii ndiyo ilisababisha Mafarisayo kusimama dhidi ya Yesu. Wengine wanajua kwamba kazi Yangu iko katika maslahi ya mwanadamu, lakini bado wanaendelea kuamini kwamba Yesu na Mimi ni viumbe tofauti kabisa visivyopatana. Wakati huo, Yesu alizungumza tu na wanafunzi Wake mfululizo wa mahubiri kwa Enzi ya Neema, kama jinsi ya kuweka vitendoni, jinsi ya kukusanyika pamoja, jinsi ya kuuliza kwa maombi, jinsi ya kuwatendea wengine, na mengineyo. Kazi Aliyoifanya ilikuwa hiyo ya Enzi ya Neema, na alielezea tu juu ya jinsi wanafunzi na waliomfuata wanapaswa kuweka vitendoni. Alifanya tu kazi ya Enzi ya Neema na hakuna hata moja ya siku za mwisho. Wakati Yehova aliandika sheria ya Agano la Kale kwa Enzi ya Sheria, mbona basi hakufanya kazi ya Enzi ya Neema? Mbona hakueleza wazi mapema kazi ya Enzi ya Neema? Hii haingekuwa ya manufaa kwa kukubali kwa mwanadamu? Alitabiri tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa na kuja mamlakani, lakini Hakutekeleza mapema kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu jinsi mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani, ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu. Hasa, haingekuwa tendo la imani ya uwongo kutafuta ndani ya Biblia kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Nini unaweza kupambanua tu kwa kushika Biblia kwa mikono yako? Uwe mkalimani wa Biblia ama mhubiri, nani anaweza kujua mbeleni kazi ya leo?


        “Yeye ambaye ana sikio, na asikie yale ambayo makanisa yaliambiwa na Roho.” Mmeyasikia sasa maneno ya Roho Mtakatifu? Maneno ya Mungu yamekuja juu yenu. Mnayasikia? Mungu anafanya kazi ya neno katika siku za mwisho, na maneno haya ni yale ya Roho Mtakatifu, kwani Mungu ni Roho Mtakatifu na Anaweza pia kuwa mwili; kwa hivyo, maneno ya Roho Mtakatifu, yalivyosemwa zamani, ni maneno ya Mungu mwenye mwili wa leo. Kuna wanadamu wajinga wanaoamini kwamba maneno ya Roho Mtakatifu yanapaswa kuja chini kutoka mbinguni hadi kwa masikio ya mwanadamu. Yeyote anayefikiria hivi hajui kazi ya Mungu. Kwa kweli, matamshi yaliyosemwa na Roho Mtakatifu ni yale yaliyosemwa na Mungu aliyekuwa mwili. Roho Mtakatifu hawezi kuongea moja kwa moja na mwanadamu, na Yehova hakuongea moja kwa moja na watu, hata kwa Enzi ya Sheria. Si ungekuwa uwezekano wa chini zaidi kwamba Angefanya hivyo kwa enzi ya leo? Kwa Mungu kunena matamshi ili kutekeleza kazi, lazima Awe mwili, la sivyo kazi yake haiwezi kukamilisha malengo Yake. Wanaomkataa Mungu ni wale wasiojua Roho ama kanuni ambazo Mungu hufanya kazi. Wanaoamini kwamba sasa ni enzi ya Roho Mtakatifu lakini bado hawakubali kazi Yake mpya ni wale wanaoishi kwa imani isiyo dhahiri. Wanadamu kama hawa hawatapokea kamwe kazi ya Roho Mtakatifu. Wale wanaotaka tu Roho Mtakatifu azungumze moja kwa moja na kutekeleza kazi Yake, lakini bado hawakubali maneno ama kazi ya Mungu mwenye mwili, kamwe hawataweza kuchukua hatua katika enzi mpya ama kupokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu!


Tanbihi:


a. Nakala ya awali inasoma “ambayo ndiyo.”


Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING