28 Jun
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Desturi ya Sala

Nyinyi hamtilii maanani sala katika maisha yenu ya kila siku. Watu daima wamepuuza sala. Katika sala zao hapo awali walikuwa wakifanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati na kufanya mchezo tu, na hakuna mtu aliyeupeana moyo wake kwa ukamilifu mbele ya Mungu na kumwomba Mungu kweli. Watu humwomba Mungu tu wakati kitu kinawatendekea. Katika wakati huu wote, umewahi kweli kumwomba Mungu? Je, umewahi kutoa machozi ya uchungu mbele ya Mungu? Je, umewahi kujijua mwenyewe mbele ya Mungu? Je, umewahi kumwomba Mungu maombi ya kutoka? Kuomba hufanyiwa mazoezi polepole: Ikiwa kwa kawaida huombi nyumbani, basi hutakuwa na njia yoyote ya kuomba kanisani, na kama kwa kawaida huombi wakati wa mikusanyiko midogo, basi hutaweza kusali wakati wa mikusanyiko mikubwa. Ikiwa kwa kawaida humkaribii Mungu au kutafakari juu ya maneno ya Mungu, basi hutakuwa na chochote cha kusema wakati wa kuomba—na hata kama utaomba, midomo yako itakuwa tu ikisonga, hutakuwa unaomba kwa kweli.

Ni nini maana ya kuomba kwa kweli? Ina maana ya kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu, na kuwasiliana na Mungu baada ya kufahamu mapenzi Yake na kutegemea maneno Yake; ina maana ya kuhisi kuwa karibu na Mungu hasa, kuhisi kwamba Yeye yuko mbele yako, na kwamba una kitu cha kumwambia; na inamaanisha kuwa mwangavu hasa ndani ya moyo wako, na kuhisi kwamba Mungu ni wa kupendeza hasa. Utajisikia kutiwa moyo sana, na baada ya kusikia maneno yako ndugu zako watajisikia kufurahishwa, watahisi kwamba maneno unayosema ni maneno yaliyo ndani ya mioyo yao, maneno ambayo wangependa kusema, na kwamba kile unachosema kinawakilisha kile wanachotaka kusema. Hii ndiyo maana ya kuomba kwa kweli. Baada ya kuomba kwa kweli, moyoni mwako utahisi kuwa na amani, na kufurahishwa; nguvu ya kumpenda Mungu itaongezeka, na utahisi kwamba hakuna kitu chochote katika maisha yako yote kinachostahili au ni muhimu zaidi kuliko kumpenda Mungu—na yote haya yatathibitisha kuwa maombi yako yamekuwa yenye ufanisi. Je, umewahi kuomba kwa njia hiyo?

Na je, kuhusu maudhui ya sala? Unapaswa kuomba, hatua kwa hatua, kwa mujibu wa hali yako ya kweli na kile kinachotakiwa kufanywa na Roho Mtakatifu, na unapaswa kuwasiliana kwa karibu na Mungu kulingana na mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake kwa mwanadamu. Unapoanza kufanya mazoezi ya maombi yako, kwanza peana moyo wako kwa Mungu. Usijaribu kufahamu mapenzi ya Mungu; jaribu tu kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu. Unapokuja mbele za Mungu, sema hivi: "Ee Mungu! Leo tu ndio natambua kuwa nilikuwa nikikuasi. Mimi kweli ni mpotovu na mwenye kustahili dharau. Awali, nilikuwa nikipoteza muda wangu; kuanzia leo nitaishi kwa ajili Yako, nitaishi kwa kudhihirisha maisha ya maana, na kuridhisha mapenzi Yako. Ningependa Roho Wako afanye kazi ndani yangu daima, na daima aniangaze na kunipa nuru, ili nipate kuwa na ushuhuda wenye nguvu na unaosikika mbele Zako, unaomruhusu Shetani kuuona utukufu Wako, ushuhuda Wako, na thibitisho la ushindi Wako ndani yetu." Wakati unapoomba kwa njia hii, moyo wako utawekwa huru kabisa, baada ya kuomba kwa njia hii, moyo wako utakuwa karibu na Mungu, na kwa kuomba hivi mara kwa mara, Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako bila shaka. Ikiwa daima wewe humwita Mungu kwa njia hii na kufanya azimio lako mbele ya Mungu, siku itawadia ambapo azimio lako litaweza kukubalika mbele ya Mungu, wakati moyo wako na nafsi yako vyote vitapokelewa na Mungu, na hatimaye utakamilishwa na Mungu. Sala ni ya muhimu sana kwenu. Unapoomba, unapokea kazi ya Roho Mtakatifu, hivyo moyo wako unaguswa na Mungu, na nguvu za upendo kwa Mungu ndani yako huchipuka. Ikiwa hutaomba kwa moyo wako, ikiwa hutafungua moyo wako kuwasiliana kwa karibu na Mungu, basi Mungu hatakuwa na njia ya kufanya kazi ndani yako. Ikiwa, baada ya kusali, umesema maneno yote yaliyo ndani ya moyo wako na Roho wa Mungu hajasisimuka, ikiwa huhisi kutiwa moyo ndani, basi hili linaonyesha kwamba moyo wako hauna ari, kwamba maneno yako si ya kweli, na bado wewe ni mchafu. Ikiwa, baada ya kusali, unafurahishwa, basi sala zako zimekubaliwa na Mungu na Roho wa Mungu amefanya kazi ndani yako. Kama mtu ambaye huhudumu mbele ya Mungu, huwezi kuwa bila sala. Ikiwa unaona ushirika na Mungu kama kitu ambacho kina maana na cha thamani, ungeweza kuacha sala? Hakuna mtu anayeweza kuwa bila mawasiliano ya karibu na Mungu. Bila sala, unaishi katika mwili, unaishi katika utumwa wa Shetani; bila sala ya kweli, unaishi chini ya ushawishi wa giza. Natumaini kwamba ndugu wanaweza kuomba kila siku. Huku si kuzingatia mafundisho ya dini, hata hivyo, bali matokeo ambayo yanapaswa kutimizwa. Je, uko tayari kuacha usingizi kidogo na anasa, kusema sala za asubuhi wakati wa alfajiri na kisha kufurahia maneno ya Mungu? Ikiwa utaomba na kula na kunywa maneno ya Mungu, katika njia hii, kwa moyo safi, basi utakubalika zaidi na Mungu. Ikiwa unafanya hivyo kila siku, ukijizoeza kumpa Mungu moyo wako kila siku na kuwasiliana kwa karibu na Mungu, basi ufahamu wako wa Mungu utaongezeka bila shaka, na utaweza kufahamu vizuri zaidi mapenzi ya Mungu. Unapaswa kusema: "Ee Mungu! Ningependa kutimiza wajibu wangu. Ili Uweze kutukuzwa ndani yetu, na Uweze kufurahia ushuhuda ulio ndani yetu, kikundi hiki cha watu, naweza tu kutoa nafsi yangu yote kwako. Nakuomba Ufanye kazi ndani yetu, ili niweze kukupenda na kukuridhisha kwa kweli, na kukufanya Uwe lengo ambalo ninafuatilia." Wakati ambapo unakuwa na mzigo huu, Mungu atakufanya uwe mkamilifu bila shaka; hupaswi tu kuomba kwa ajili yako mwenyewe, bali pia kwa ajili ya kutekeleza mapenzi ya Mungu, na kwa ajili ya kumpenda Yeye. Hiyo ndiyo aina ya sala ya kweli kabisa. Je, wewe huomba ili kutekeleza mapenzi ya Mungu?

Hapo awali, nyinyi hamkujua jinsi ya kuomba, na mlipuuza maombi; leo, lazima mjitahidi kabisa kujifundisha kuomba. Ikiwa huwezi kuwa na ujasiri wa kumpenda Mungu, basi unawezaje kuomba? Unapaswa kusema: "Ee Mungu! Moyo wangu hauwezi kukupenda kweli, nataka kukupenda lakini sina nguvu. Napaswa kufanya nini? Napenda Ufungue macho ya roho yangu, napenda Roho Wako auguse moyo wangu, ili mbele Yako nivuliwe hali zote za kutoonyesha hisia, na nisishurutishwe na mtu yeyote, jambo, au kitu; nauweka moyo wangu wazi kabisa mbele Yako, ili nafsi Yangu yote ijitoe mbele Yako, na Uweze kunijaribu vile Utakavyo. Sasa, siwazii matarajio yangu, wala sifungwi na kifo. Kwa kuutumia moyo wangu ambao unakupenda, napenda kutafuta njia ya uzima. Vitu vyote na matukio viko mikononi Mwako, majaliwa yangu yako mikononi Mwako, na, zaidi ya hayo, maisha yangu yanadhibitiwa na mikono Yako. Sasa, nafuatilia kukupenda Wewe, na bila kujali kama Wewe unaniruhusu kukupenda, haijalishi jinsi Shetani anavyoingilia, nimeamua kukupenda Wewe." Unapokabiliwa na mambo kama hayo, unasali kwa njia hii. Ikiwa utafanya hivyo kila siku, nguvu ya kumpenda Mungu itaongezeka polepole.

Mtu huingiaje katika sala ya kweli? Wakati unaomba, moyo wako lazima uwe na amani mbele ya Mungu, na lazima uwe mwaminifu. Wewe kweli unawasiliana kwa karibu na kuomba na Mungu; usimdanganye Mungu kwa kutumia maneno ya kupendeza. Sala inalenga kile ambacho Mungu anataka kukamilisha leo. Mwombe Mungu akupe nuru na mwangaza mwingi zaidi, na ulete hali halisi na matatizo yako mbele za Mungu kuomba, na ufanye azimio mbele za Mungu. Sala sio kufuata utaratibu, bali ni kumtafuta Mungu kwa kutumia moyo wako wa kweli. Omba kwamba Mungu aulinde moyo wako, na Aufanye uwe na amani mara nyingi mbele za Mungu, Akuwezeshe kujijua, na kujidharau, na kujitupa katika mazingira ambayo Mungu amekuwekea, hivyo kukuruhusu uwe na uhusiano wa kawaida na Mungu na kukufanya mtu anayempenda Mungu kweli.

Ni nini umuhimu wa sala?

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato ambao mtu huguswa na Roho wa Mungu. Inaweza kusemwa kwamba wale ambao hawana sala ni wafu wasio na roho, ushahidi kwamba hawana uwezo wa kuguswa na Mungu. Bila sala, hawawezi kupata maisha ya kawaida ya kiroho, sembuse kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu; bila sala, wao huvunja uhusiano wao na Mungu, na hawawezi kupokea kibali cha Mungu. Ukiwa mtu anayemwamini Mungu, kadri unavyoomba, ndivyo unavyozidi kuguswa na Mungu. Watu kama hao wana azimio kubwa zaidi na wanaweza kupokea zaidi nuru ya hivi karibuni kutoka kwa Mungu; kwa hivyo, watu kama hawa pekee ndio wanaweza kukamilishwa mapema iwezekanavyo na Roho Mtakatifu.

Je, ni matokeo gani yanayofaa kutimizwa kwa sala?

Watu wanaweza kutekeleza mazoea ya sala na kuelewa umuhimu wa sala, lakini matokeo yanayofaa kutimizwa kwa sala sio jambo rahisi. Sala sio jambo la kupitia urasmi wa kisheria, au kufuata utaratibu, au kukariri maneno ya Mungu, ambalo ni kusema, sala haimaanishi kuiga maneno kama kasuku na kuwaiga wengine. Katika sala, lazima umpe Mungu moyo wako, ukishiriki maneno yaliyo ndani ya moyo wako na Mungu ili uweze kuguswa na Mungu. Ikiwa maombi yako yatakuwa na matokeo, basi lazima yategemee usomaji wako wa maneno ya Mungu. Ni kwa kuomba tu katikati ya maneno ya Mungu ndipo utaweza kupokea nuru na mwangaza zaidi. Sala ya kweli huonyeshwa kwa kuwa na moyo ambao unatamani sana matakwa yaliyowekwa na Mungu, na kuwa tayari kutimiza matakwa haya; utaweza kuchukia yote ambayo Mungu huchukia, kwa msingi huo utakuwa na maarifa, na utajua na kuelewa wazi kuhusu ukweli ulioelezwa na Mungu. Kuwa na azimio, na imani, na maarifa, na njia ya kufanya mazoezi baada ya kuomba—huku tu ndiko kuomba kwa kweli, na sala kama hii tu ndiyo inaweza kuwa na ufanisi. Lakini sala lazima ijengwe juu ya msingi wa kufurahia maneno ya Mungu na kuwasiliana kwa karibu na Mungu katika maneno Yake, moyo wako ukiweza kumtafuta Mungu na kuwa na amani mbele ya Mungu. Sala kama hiyo tayari imefikia kiwango cha kuwasiliana kwa kweli na Mungu.

Maarifa ya msingi kuhusu kuomba:

1. Usiseme kijinga chochote kinachokuja kwenye akili. Lazima kuwe na mzigo ndani ya moyo wako, ambalo ni kusema, lazima uwe na lengo wakati unapoomba.

2. Sala zako zinapaswa kuwa na maneno ya Mungu; lazima zitegemezwe kwa maneno ya Mungu.

3. Wakati unapoomba, huwezi kurudia mambo ya kale; hupaswi kuleta vitu ambavyo vimepitwa na wakati. Unapaswa kujifunza hasa kunena maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu; wakati huo tu ndipo utaweza kufikia kiwango cha ushirika wa kweli na Mungu.

4. Sala ya kikundi inapaswa kulenga kiini, ambacho lazima kiwe kazi ya Roho Mtakatifu leo.

5. Watu wote wanapaswa kujifunza jinsi ya kuwaombea wengine. Wanapaswa kupata sehemu katika maneno ya Mungu ambayo wanataka kuombea, ambayo kwayo lazima wawe na mzigo, na ambayo lazima waiombee mara nyingi. Hili ni dhihirisho moja la kujali mapenzi ya Mungu.

Maisha ya maombi ya kibinafsi yanategemea kuelewa umuhimu wa sala na maarifa ya msingi ya sala. Lazima mwanadamu aombee dosari zake mara kwa mara katika maisha yake ya kila siku, na lazima aombe juu ya msingi wa maarifa wa maneno ya Mungu ili kutimiza mabadiliko katika tabia yake ya maisha. Kila mtu anapaswa kuanzisha maisha yake ya maombi, anapaswa kuombea maarifa kutegemea maneno ya Mungu, anapaswa kuomba ili kutafuta maarifa ya kazi ya Mungu. Weka hali zako za kweli mbele ya Mungu, na uwe wa vitendo, na usitilie maanani mbinu; la muhimu ni kupata maarifa ya kweli, na kupata maneno ya Mungu kwa kweli. Yeyote anayefuatilia kuingia katika maisha ya kiroho lazima aweze kuomba kwa njia nyingi. Sala ya kimya, kutafakari maneno ya Mungu, kuja kuijua kazi ya Mungu, na kadhalika—kazi hii inayolengwa ya kuwasiliana kwa karibu, ni ili kutimiza kuingia katika maisha ya kawaida ya kiroho, kuifanya hali yako mwenyewe mbele za Mungu iwe bora zaidi, na kusababisha maendeleo makubwa zaidi katika maisha yako. Kwa kifupi, yote unayoyafanya—kama ni kula na kunywa maneno ya Mungu, au kuomba kimya au kutangaza kwa sauti—ni ili kuona wazi maneno ya Mungu, na kazi Yake, na kile Anachotaka kutimiza ndani yako. La muhimu zaidi, ni ili kufikia viwango ambavyo Mungu anahitaji na kuyapeleka maisha yako kwa kiwango kinachofuata. Kiwango cha chini zaidi ambacho Mungu anahitaji kwa watu ni kwamba waweze kufungua mioyo yao Kwake. Ikiwa mwanadamu atautoa moyo wake wa kweli kwa Mungu na kusema kile kilicho ndani ya moyo wake kwa Mungu, basi Mungu yuko tayari kufanya kazi ndani ya mwanadamu; Mungu hataki moyo wa mwanadamu uliopotoka, lakini moyo wake ulio safi na mwaminifu. Ikiwa mwanadamu hasemi yaliyo moyoni mwake kwa Mungu kwa kweli, basi Mungu haugusi moyo wa mwanadamu, au kufanya kazi ndani yake. Hivyo, jambo muhimu sana kuhusu kuomba ni kusema maneno ya moyo wako wa kweli kwa Mungu, kumwambia Mungu kuhusu dosari zako au tabia ya kuasi na kujifungua kabisa kwa Mungu. Wakati huo tu ndipo Mungu atakuwa na hamu ya sala zako; la sivyo, basi Mungu atauficha uso Wake kutoka kwako. Kigezo cha chini kabisa cha sala ni kwamba lazima uweze kuuweka moyo wako kwa amani mbele za Mungu, na hupaswi kuondoka kwa Mungu. Pengine, wakati huu, hujapata mtazamo mpya au wa juu, lakini lazima utumie sala ili mambo yaendelee kama yalivyo—huwezi kurudi nyuma. Hili ndilo jambo dogo zaidi ambalo unapaswa kutimiza. Ikiwa huwezi kufanikisha hata hili, basi inathibitisha kwamba maisha yako ya kiroho hayajaingia katika njia sahihi; kwa hiyo, huwezi kushikilia maono yako ya mwanzo, na kuondolea imani kwa Mungu, na uamuzi wako hatimaye hutoweka. Kuingia kwako katika maisha ya kiroho kunadhihirishwa na iwapo sala zako zimeingia katika njia sahihi au la. Watu wote lazima waingie katika uhalisi huu, lazima wafanye kazi ya kujifunza wenyewe kwa kufahamu katika sala, sio kusubiri kwa kukaa tu, lakini kwa ufahamu watafute kuguswa na Roho Mtakatifu. Wakati huo tu ndipo watakuwa watu wanaomtafuta Mungu kwa kweli.

Unapoanza kuomba, kuwa wa kweli, na usitake kufanya kupita kiasi; huwezi kufanya madai ya ubadhirifu, ukitumaini kwamba mara tu utakapofungua kinywa chako utaguswa na Roho Mtakatifu, utapata nuru na mwangaza, na kupewa neema nyingi. Hilo haliwezekani—Mungu hafanyi mambo yaliyo ya rohoni. Mungu hutimiza sala za watu kwa wakati Wake mwenyewe na wakati mwingine Yeye hujaribu imani yako kuona kama wewe ni mwaminifu mbele Zake. Unapoomba lazima uwe na imani, uvumilivu, na azimio. Watu wengi wanapoanza kujifunza kuomba, hawahisi kuwa wameguswa na Roho Mtakatifu na hivyo huvunjika moyo. Hili halikubaliki! Lazima uwe na nia ya kutobadili msimamo, lazima ulenge kuhisi mguso wa Roho Mtakatifu, na kutafuta na kuchunguza. Wakati mwingine, njia unayofuata ni ile isiyo sahihi; wakati mwingine, misukumo na dhana zako haviwezi kusimama imara mbele za Mungu, na hivyo Roho wa Mungu hakusisimui; vivyo pia kuna nyakati ambapo Mungu huangalia kama wewe ni mwaminifu au la. Kwa kifupi, lazima ujitahidi zaidi katika kujifunza. Ikiwa utatambua kuwa njia unayoifuata ni ya kuacha maadili, unaweza kubadilisha jinsi unavyoomba. Maadamu unatafuta kwa kweli, na unatamani kupokea, basi Roho Mtakatifu atakuingiza kwenye ukweli huu. Wakati mwingine unasali kwa moyo wa ukweli lakini huhisi kama umeguswa hasa. Katika nyakati kama hizi lazima utegemee imani yako, na uamini kwamba Mungu anayaangalia maombi yako; lazima uwe na uvumilivu katika sala zako.

Lazima uwe mwaminifu, na lazima uombe ili uondoe ujanja ndani ya moyo wako. Unapotumia maombi ili kujitakasa wakati wowote inapohitajika, na kuyatumia ili uguswe na Roho wa Mungu, tabia yako itabadilika polepole. Maisha ya kweli ya kiroho ni maisha ya sala, na ni maisha ambayo yanaguswa na Roho Mtakatifu. Mchakato wa kuguswa na Roho Mtakatifu ni mchakato wa kubadilisha tabia ya mwanadamu. Maisha ambayo hayajaguswa na Roho Mtakatifu si maisha ya kiroho, bado ni ibada ya kidini; wale tu ambao huguswa na Roho Mtakatifu mara kwa mara, na wamepewa nuru na kuangazwa na Roho Mtakatifu, ndio watu ambao wameingia katika maisha ya kiroho. Tabia ya mwanadamu hubadilika kwa uthabiti wakati anapoomba, na kadri anavyosisimuliwa na Roho wa Mungu, ndivyo anavyozidi kuwa hai na mtiifu. Kwa hiyo, pia, moyo wake utatakaswa polepole, baada ya hapo tabia yake itabadilika polepole. Hayo ndiyo matokeo ya sala ya kweli.

Chanzo: Kuhusu Desturi ya Sala


Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING