12 Jan
Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu

Umeme wa Mashariki


        Kila mmoja anapaswa kuchunguza maisha yake upya ya kumwamini Mungu ili kuona iwapo, katika mchakato wa kumfuata Mungu, ameelewa kwa dhati, amefahamu kwa dhati, na kuja kumjua Mungu kwa dhati, iwapo anajua kweli ni mawazo gani Mungu Anayo kwa aina tofauti za binadamu, na iwapo kweli anaelewa kile ambacho Mungu Anafanya juu yake na jinsi Mungu Anaeleza kila tendo lake. Huyu Mungu, Ambaye yuko kando yako, Akiongoza mwelekeo wa kuendelea kwako, Akiamuru hatima yako, na kukupa mahitaji yako—ni kiasi gani ambacho, katika uchambuzi wako, unaelewa nani kiasi gani ambacho kweli unajua kumhusu Yeye? Je, unajua Anachofanyia kazi kwako kila siku? Je, unajua kanuni na makusudi Anayozingatia katika matendo Yake yote? Unajua jinsi Anavyokuongoza? Unajua mbinu Anazotumia kukupa mahitaji yako? Unajua mbinu ambazo Anatumia kukuongoza? Je, unajua kile Anachotaka kupata kutoka kwako na kile Anachotaka kutimiza kwako? Je, unajua mtazamo Anaochukua katika namna nyingi ambazo unatenda? Unajua iwapo wewe ni mtu Anayependwa na Yeye? Unajua chanzo cha furaha, hasira, huzuni na uchangamfu Wake, fikira na dhana zinazohusiana na hayo, na kiini Chake? Unajua, hatimaye, huyu Mungu ni Mungu wa aina gani ambaye unamwamini? Je, maswali haya na mengine ya aina hii kitu ambacho hujawahi kuelewa ama kuwaza kuyahusu? Katika kufuata imani yako kwa Mungu, umewahi, katika ufahamu halisi na kuyatambua maneno ya Mungu, umeondoa hali za kutomwelewa? Je, baada ya kupokea adhabu na kurudi kwa Mungu, umefikia unyenyekevu halisi na kujali kwa kweli? Je, wakati wa kuadibu kwa Mungu na hukumu, umepata kutambua uasi na asili ya kishetani ya mwanadamu na kupata kiasi kidogo cha kuelewa kuhusu utakatifu wa Mungu? Je, chini ya uongozi na kupata nuru kwa maneno ya Mungu, umeanza kuwa na mtazamo mpya wa maisha? Katika majaribu yaliyotumwa na Mungu, umepata kuhisi kutovumilia Kwake makosa ya mwanadamu na pia kile Anachohitaji kutoka kwako na vile Anavyokuokoa? Iwapo hujui kutomwelewa Mungu ni nini, au jinsi ya kumaliza kutoelewa huku, basi mtu anaweza kusema hujawahi kuingia katika ushirika wa kweli na Mungu na hujawahi kumwelewa Mungu, ama angalau mtu anaweza kusema kuwa hujawahi kuwa na nia ya Kumwelewa. Iwapo hujui nidhamu ya Mungu na kuadibu ni nini, basi kwa hakika hujui kujiwasilisha na kujali ni nini, ama angalau hujawahi kujiwasilisha kwa Mungu kwa kweli au kumjali. Iwapo hujawahi kupitia kuadibu kwa Mungu na hukumu, basi kwa kweli hutajua utakatifu Wake ni nini, na utakuwa hata na ufahamu dhahiri kiasi kidogo kwa mintarafu ya uasi wa mwanadamu ni nini. Iwapo hujawahi kuwa na mtazamo sahihi wa maisha, au lengo sahihi katika maisha, bali bado uko katika hali ya mshangao na kutokuwa na uamuzi kuhusu njia yako ya maisha ya baadaye, hata kwa kiwango cha kusita kuenda mbele, basi ni dhahiri kuwa hujawahi kupokea nuru na uongozi wa Mungu, na mtu anaweza tu kusema kuwa hujawahi kupewa au kujazwa tena na maneno ya Mungu kwa kweli. Iwapo bado hujapitia majaribu ya Mungu, basi ni hakika kuwa bila shaka hutajua kutovumilia kwa Mungu makosa ya mwanadamu ni nini, wala hutaelewa kile ambacho Mungu Anahitaji hatimaye kutoka kwako, ama hata kidogo zaidi, hatimaye, kazi Yake ya kumsimamia na kumwokoa mwanadamu ni nini. Haijalishi ni kwa miaka mingapi mwanadamu ameamini katika Mungu, iwapo hajawahi kupitia ama kutambua chochote katika maneno ya Mungu, basi kwa hakika hatembei katika njia ya kuelekea wokovu, imani yake katika Mungu kwa hakika haina chochote, maarifa yake kumhusu Mungu pia kwa hakika ni sufuri, na ni hakika kuwa hana ufahamu wowote kuhusu ni nini kumcha Mungu.


        Miliki na uwepo wa Mungu, kiini cha Mungu, tabia ya Mungu—yote yamewekwa wazi katika maneno Yake kwa binadamu. Anapopitia maneno ya Mungu, katika mchakato wa kuyatekeleza mwanadamu atapata kuelewa kusudi la maneno Anayonena Mungu, na kuelewa chemichemi na usuli wa maneno ya Mungu, na kuelewa na kufahamu matokeo yaliotarajiwa ya maneno ya Mungu. Kwa binadamu, haya ni mambo yote ambayo mwanadamu lazima ayapitie, ayatambue, na kuyafikia ili kuufikia ukweli na uzima, kutambua nia ya Mungu, kubadilishwa katika tabia yake, na kuweza kutii mamlaka ya Mungu na mipango. Katika wakati huo ambao mwanadamu anapitia, anafahamu, na kuvifikia vitu hivi, atakuwa kupata kumwelewa Mungu polepole, na katika wakati huu atakuwa pia amepata viwango tofauti vya ufahamu kumhusu Yeye. Kuelewa huku na maarifa havitoki katika kitu ambacho mwanadamu amefikiria ama kutengeneza, ila kutoka kwa kile ambacho anafahamu, anapitia, anahisi, na anashuhudia ndani yake mwenyewe. Ni baada tu ya kufahamu, kupitia, kuhisi, na kushuhudia vitu hivi ndipo ufahamu wa mwanadamu kumhusu Mungu utapata ujazo, ni maarifa anayopata katika wakati huu pekee ndio ulio halisi, wa kweli na sahihi, na mchakato huu—wa kupata kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu kwa kuelewa, uzoefu, kuhisi, na kushuhudia maneno Yake—sio kingine ila ushirika wa kweli kati ya mwanadamu na Mungu. Katikati ya aina hii ya ushirika, mwanadamu anakuja kuelewa kwa dhati na kufahamu nia za Mungu, anakuja kuelewa kwa dhati na kujua miliki na uwepo wa Mungu, anakuja na kuelewa kujua kwa kweli kiini cha Mungu, anakuja kuelewa na kujua tabia ya Mungu polepole, anafikia uhakika wa kweli kuhusu, na ufafanuzi sahihi wa, ukweli wa mamlaka ya Mungu juu ya vitu vyote vilivyoumbwa, na kupata mkondo kamili kwa na ufahamu wa utambulisho wa Mungu na nafasi Yake. Katika aina hii ya ushirika, mwanadamu anabadilika, hatua kwa hatua, mawazo yake kuhusu Mungu, bila kumwaza pasi na msingi, ama kuipa nafasi tashwishi yake kumhusu Yeye, ama kutomwelewa, ama kumshutumu, ama kupitisha hukumu Kwake, ama kuwa na shaka Naye. Kwa sababu hii, mwanadamu atakuwa na mijadala michache na Mungu, atakuwa na uhasama kiasi kidogo na Mungu, na kutakuwa na matukio machache ambapo atamuasi Mungu. Kwa upande mwingine, kujali kwa mwanadamu na utii kwa Mungu kutakua kwa kiasi kikubwa, na uchaji wake Mungu utakuwa wa kweli zaidi na pia mkubwa zaidi. Katika ya aina hii ya ushirika, mwanadamu hatapata kupewa ukweli pekee na ubatizo wa uzima, bali wakati uo huo pia atapata maarifa ya kweli ya Mungu. Katika aina hii ya ushirika, mwanadamu hatapata kubadilishwa kwa tabia yake na kupata wokovu pekee, bali pia kwa wakati huo atafikia uchaji na ibada ya kweli ya kiumbe aliyeumbwa kwa Mungu. Baada ya kuwa na aina hii ya ushirika, imani ya mwanadamu katika Mungu haitakuwa tena ukurasa tupu wa karatasi, ama ahadi ya maneno matupu, ama harakati na tamanio lisilo na lengo na kuabudu kama mungu; katika aina hii ya ushirika pekee ndio maisha ya mwanadamu yatakua kuelekea ukomavu siku baada ya siku, na ni wakati huu ndio tabia yake itabadilika polepole, na imani yake kwa Mungu, hatua kwa hatua, itatoka kwenye imani ya wasiwasi na kutoeleweka na imani isiyo ya hakika mpaka katika utii wa kweli na kujali, na kuwa katika uchaji Mungu wa kweli, na mwanadamu pia, katika mchakato wa kumfuata Mungu, ataendelea polepole kutoka kuwa mtazamaji na kuwa na hali ya utendaji, kutoka yule anayeshughulikwa na kuwa anayechukua nafasi ya kutenda; kwa aina hii ya ushirika pekee ndipo mwanadamu atafikia kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu, kwa ufahamu wa kweli wa Mungu. Kwa sababu watu wengi hawajawahi kuiingia katika ushirika wa kweli na Mungu, ufahamu wao wa Mungu unakomea kiwango cha nadharia, katika kiwango cha barua na kanuni. Hivyo ni kusema, watu wengi, haijalishi ni miaka mingapi wamemwamini Mungu, ikija kwa kumjua Mungu bado wako mahali walipoanzia, wamekwama katika msingi wa aina za heshima, na mitego yao ya hadhi na kabaila za kishirikina. Kwamba maarifa ya mwanadamu kumhusu Mungu yanapaswa kukomea yalipoanzia ina maana kwamba hayapo kabisa. Mbali na uthibitisho wa mwanadamu kuhusu nafasi ya Mungu na utambulisho, imani ya mwanadamu kwa Mungu bado iko katika hali ya kutoeleweka na kutokuwa na uhakika. Hii ikiwa hivyo, ni kiasi gani ambacho mwanadamu anaweza kuwa nacho kuhusu uchaji Mungu wa kweli?


        Haijalishi kiwango cha imani yako katika uwepo Wake, hili haliwezi kuchukua mahali pa ufahamu wako wa Mungu, wala uchaji wako wa Mungu. Haijalishi kiwango ambacho umefurahia baraka Zake na neema Yake, hii haiwezi kuchukua nafasi ya ufahamu wako wa Mungu. Haijalishi ni kiwango gani unataka kuweka wakfu kila kitu chako na kugharimika kwa ajili Yake, hii haiwezi kuchukua nafasi ya maarifa yako kuhusu Mungu. Ama labda umeyazoea sana maneno ambayo Amenena mpaka unayajua kimoyomoyo na unaweza kuyasema upesi kinyumenyume; hata hivyo, hii haiwezi kuchukua nafasi ya maarifa yako kuhusu Mungu. Haijalishi kiwango cha dhamira ya mwanadamu katika kumfuata Mungu, iwapo hajawahi kuwa na ushirika wa kweli na Mungu, ama kuwa na uzoefu wa kweli wa maneno ya Mungu, basi ufahamu wake wa Mungu utakuwa utupu tu au ndoto isiyo na mwisho; kwa kuwa yote yale unaweza kuwa “umekumbana” na Mungu kwa kupita, au kukutana Naye uso kwa uso, ufahamu wako wa Mungu bado utakuwa sufuri, na uchaji wako wa Mungu utakuwa tu kidahizo ama njozi.


        Watu wengi huyashika maneno ya Mungu kuyasoma siku baada ya siku, kiasi kwamba wanaviweka akilini vifungu vyote maarufu humo kama vitu vyao vyenye thamani zaidi, na zaidi kuyahubiri maneno ya Mungu kila mahali, wakiwatolea na kuwasaidia wengine kwa njia ya maneno Yake. Wanafikiri kuwa kufanya hivi ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, kuwa na ushuhuda kwa maneno Yake, kwamba kufanya hivi ni kufuata njia ya Mungu; wanafikiri kuwa kufanya hivi ni kuishi kulingana na maneno ya Mungu, kwamba kufanya hivi ni kuleta maneno Yake katika maisha yao halisi, kuwa kufanya hivi kutawawezesha kupokea pongezi ya Mungu, na kuokolewa na kukamilika. Lakini, hata wanapohubiri maneno ya Mungu, hawazingatii maneno ya Mungu katika matendo, ama kujaribu kujileta sambamba na yale yanayofichuliwa katika maneno ya Mungu. Badala yake, wanayatumia maneno ya Mungu kupata upendo na imani ya wengine kwa hila, kuingia katika usimamizi wao wenyewe, na kubadhiri na kuiba sifa za Mungu. Wanatarajia, kwa ubatili, kutumia nafasi waliyopata kwa kueneza maneno ya Mungu ili kupewa kazi ya Mungu na pongezi Yake. Miaka mingapi imepita, lakini hao watu hawajaweza tu kupata pongezi ya Mungu katika hatua ya kuyahubiri maneno ya Mungu, na hawajaweza tu kugundua njia ambayo wanafaa kufuata katika hatua ya kushuhudia maneno ya Mungu, na hawajajisaidia tu ama kujipatia wenyewe katika hatua ya kuwapa na kuwasaidia wengine kwa njia ya maneno ya Mungu, na hawajaweza tu kumjua Mungu, ama kuamsha ndani yao uchaji wa kweli wa Mungu, katika hatua ya kufanya haya yote; kwa upande mwingine, kutoelewa kwao kuhusu Mungu kunakuwa hata wenye kina zaidi, kutokuwa na imani kwao kwa Mungu kunazidi kuwa na mashaka, na mawazo yao kumhusu yanatiwa chumvi zaidi. Wakijazwa na kuongozwa na mawazo yao kuhusu maneno ya Mungu, wanaonekana kuwa katika haki yao kamili, kana kwamba wanapitia ujuzi wao bila juhudi, kana kwamba wamepata kusudi lao katika maisha, wito wao, na kana kwamba wameshinda maisha mapya na kuokolewa, kana kwamba, maneno ya Mungu yakibiringika kutoka kwenye ulimi kwa kukariri, wameupata ukweli, kushika nia za Mungu, na kugundua njia ya kumjua Mungu, kana kwamba, katika wakati wa kuhubiri maneno ya Mungu, wanakuja kila wakati uso kwa uso na Mungu, pia, wana “sukumwa” kila wakati mpaka kiwango cha kilio, na kila wakati kuongozwa na “Mungu” katika maneno ya Mungu, wanaonekana kushika bila kukoma wasiwasi Wake wenye ari na nia njema, na wakati uo huo kushika wokovu wa Mungu kwa mwanadamu na usimamizi Wake, kuja kujua kiini Chake, na kuelewa tabia Yake ya haki. Msingi huu ukizingatiwa, wanaoneka kuamini hata zaidi katika uwepo wa Mungu, kujua zaidi hali ya utukufu Wake, na kuhisi hata kwa kina zaidi ukuu Wake na kuvuka mipaka Kwake. Wakiwa wameinuka katika ufahamu wao wa kijuujuu wa maneno ya Mungu, itaonekana kuwa imani yao imekua, kuamua kwao kupitia mateso kumetiwa nguvu, na maarifa yao kwa Mungu yamekuwa na kina. Ila hawajui kwamba, hadi watakapopitia maneno ya Mungu kwa kweli, maarifa yao yote kuhusu Mungu na mawazo yao kumhusu Yeye yanatoka kwa mawazo yao wenyewe ya kufikiri kwa ubunifu na kukisia. Imani yao haiwezi kusimama jaribio lolote kutoka kwa Mungu, wanachoita kiroho na kimo haviwezi kusimama chini ya majaribu ya Mungu na ukaguzi, uamuzi wao ni ngome tu iliyojengwa juu ya changarawe, na wanachoita maarifa juu ya Mungu pia sio zaidi ya ubunifu wa mawazo yao. Kwa hakika, watu hawa, ambao, ilivyokuwa, wameweka juhudi kubwa katika maneno ya Mungu, hawajawahi kutambua imani ya kweli ni nini, kujiwasilisha kwa kweli ni nini, kujali kwa kweli ni nini, ama maarifa ya kweli ya Mungu ni nini. Wanachukua nadharia, mawazo, maarifa, zawadi, utamaduni, ushirikina na hata tabia nzuri za binadamu, na kuyafanya kuwa “uwekezaji wa msingi” na “zana za kijeshi” za kumwamini Mungu na kumfuata, hata kuyafanya kuwa misingi ya imani yao kwa Mungu na katika kumfuata Yeye. Wakati uo huo, pia wanachukua uwekezaji msingi huu na silaha na kuyafanya kuwa hirizi ya uchawi kwa kumjua Mungu, ya kukutana na kubishana na ukaguzi wa Mungu, majaribu, kuadibu, na hukumu. Mwishowe, wanachopata bado hakijumlishi chochote zaidi ya hitimisho kumhusu Mungu zinazoegemea hisia za kidini, katika kabaila za ushirikina, na kwa yote yaliyo ya kimapenzi, ya kustaajabisha, na yenye ugumu kuelewa, na njia yao ya kujua na kumweleza Mungu imepigwa muhuri katika muundo sawa na wa wale watu wanaoamini katika Mbingu iliyo Juu pekee, ama Mtu Mzee aliye Mawinguni, wakati ukweli wa Mungu, kiini Chake, tabia Zake, miliki Zake na asili, na kadhalika, yote yanayomhusu Mungu wa kweli Mwenyewe, ni vitu ambavyo kuvijua kumekosa mshiko, havina uhusiano kabisa na viko mbali kabisa. Katika njia hii, ingawa wanaishi chini ya upaji na ustawishaji wa maneno ya Mungu, hawawezi hata hivyo kutembea kwa kweli katika njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Sababu ya hakika ya hii ni kwamba hawajawahi kupata kujuana na Mungu, wala hawajawahi kuwa na mawasiliano ya kweli ama ushirika Naye, kwa hivyo haiwezekani kufikia maelewano ya pamoja na Mungu, ama kuamsha ndani mwao imani halisi katika, kufuata, ama ibada ya Mungu. Kwamba wanafaa kuyahusisha maneno ya Mungu, kwamba wanafaa kumhusisha Mungu—mwelekeo huu na tabia imewahukumu kurudi mkono mtupu kutoka kwa jitihada zao, imewahukumu katika maisha yote wasiweze kutembea katika njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Lengo wanalolengea, na mwelekeo wanaoelekea, inamaanisha kuwa ni maadui wa Mungu milele, na kwamba hata milele hawatawahi kuweza kupokea wokovu.


        Iwapo, katika tukio la mwanadamu ambaye amemfuata Mungu kwa miaka mingi na kufurahia kupewa maneno Yake kwa miaka mingi, ufafanuzi wake kuhusu Mungu ni, katika kiini chake, sawa na ule wa mtu anayejisujudu kwa heshima mbele ya sanamu, basi hii itamaanisha kuwa huyu mtu hajapata ukweli wa maneno ya Mungu. Kwa kutazama katika chanzo cha hii, mtu anaona kuwa tu hajaingia katika ukweli wa maneno ya Mungu, na kwa sababu hii hali halisi, ukweli, nia, na matarajio juu ya binadamu, yote ambayo yana asili kwa maneno ya Mungu, hayana uhusiano wowote na yeye. Hivyo ni kusema, haijalishi ni kiwango gani mwanadamu wa aina hii anaweza kufanya bidii katika maana ya juu ya maneno ya Mungu, yote ni bure: kwani yale anayofuata ni maneno tu, kwa hivyo yale atakayopata yatakuwa pia ni maneno tu. Haijalishi kama maneno yanayonenwa na Mungu ni makubwa katika mwonekano wa nje, wazi ama magumu kuelewa, yote ni ukweli ulio lazima kwa mwanadamu anapoingia katika uzima; ni chemichemi ya maji ya uzima yanayomwezesha kuishi katika roho na mwili. Yanatosheleza kile ambacho mwanadamu anahitaji ili awe hai; kanuni na imani ya kufanya maisha yake ya kila siku; njia, lengo, na mwelekeo ambao lazima apitie ili kupokea wokovu; kila ukweli ambao anapaswa awe nao kama kiumbe aliyeumbwa mbele za Mungu; na kila ukweli jinsi mwanadamu anavyotii na kumwabudu Mungu. Ni uhakika ambao unahakikisha kuishi kwa mwanadamu, ni mkate wa kila siku wa mwanadamu, na pia ni nguzo ya msaada inayowezesha mwanadamu kuwa na nguvu na kusimama. Yamejaa utajiri wa ukweli wa ubinadamu wa kawaida anavyoishi binadamu aliyeumbwa, yamejaa ukweli ambao mwanadamu anatumia kutoka kwa upotovu na kuepuka mitego ya Shetani, yamejaa mafunzo bila kuchoka, kuonya, kuhamasisha na furaha ambayo Muumba anampa binadamu aliyeumbwa. Ni ishara ambayo inawaongoza na kuwaelimisha wanadamu kuelewa yale yote yaliyo mazuri, hakika inayohakikisha kuwa wanadamu wataishi kwa kudhihirisha na kumiliki yale yote yaliyo ya haki na mema, kigezo ambacho watu, matukio, na vitu vyote vinapimwa, na pia alama ya usafiri inayowaongoza wanadamu kuelekea wokovu na njia ya mwanga. Katika uzoefu wa kweli wa maneno ya Mungu tu ndipo mwanadamu anapewa ukweli na uzima; humu pekee ndimo anakuja kupata kuelewa ubinadamu wa kawaida ni nini, maisha yenye umuhimu ni nini, kiumbe halisi ni nini, utiifu wa kweli kwa Mungu ni nini; humu pekee ndimo anakuja kuelewa anavyofaa kumjali Mungu, jinsi ya kutimiza wajibu ya kiumbe aliyeumbwa, na jinsi ya kumiliki mfano wa mwanadamu wa kweli; humu tu ndimo anapata kuelewa maana ya imani halisi na ibada halisi; humu tu ndimo anaelewa nani ndiye Mtawala wa mbingu na nchi na vitu vyote; humu tu ndimo anakuja kuelewa njia ambayo Yule ambaye ni Bwana wa uumbaji wote Anatawala, anaongoza, na kuutosheleza uumbaji; na hapa pekee ndipo anakuja kuelewa na kushika njia ambayo Yule aliye Bwana wa uumbaji wote Anakuwa, Anadhihirishwa na kufanya kazi.… Akitenganishwa na uzoefu wa kweli wa maneno ya Mungu, mwanadamu hana maarifa ya kweli ama ufahamu katika maneno ya Mungu na ukweli. Mwanadamu wa aina hii ni maiti inayoishi tu, ganda lililoisha, na ufahamu wote unaohusiana na Muumba hauna chochote kingine kumhusu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu kama huyo hajawahi kumwamini, ama kuwahi kumfuata, na hivyo Mungu hamtambui yeye kama mwumini Wake wala mfuasi Wake, ama hata kama kiumbe halisi aliyeumbwa.


        Ili kuwa kiumbe halisi aliyeumbwa, sharti ujue Muumba ni nani, uumbaji wa mwanadamu ni wa umuhimu gani, jinsi ya kutekeleza majukumu ya kiumbe, na jinsi ya kumwabudu Bwana wa uumbaji wote, lazima aelewe, ashike, ajue, na kujali kuhusu nia za Muumba, mapenzi Yake, na madai Yake, na lazima atende kulingana na njia ya Muumba—kumcha Mungu na kuepuka maovu.


        Kumcha Mungu kuna maana gani? Na mtu anawezaje kuepuka maovu?


        “Kumcha Mungu” hakumaanishi woga na hofu isiyotajika, wala kukwepa, wala kuweka umbali, wala si kuabudu kama mungu ama ushirikina. Ila, ni kutazama na kupendezwa, sifa, imani, kuelewa, kujali, kutii, kuweka wakfu, upendo, na pia ibada isiyo na vikwazo au malalamishi, malipo na kujisalimisha. Bila ya ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na kupendezwa halisi, imani halisi, kuelewa halisi, kujali halisi ama utiifu, ila tu hofu na kukosa utulivu, shaka pekee, kutoelewa, kukwepa, na kuepuka; bila maarifa halisi ya Mungu, binadamu hawatakuwa na utakatifu na malipo halisi; bila ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na ibada halisi na kujisalimisha, uabudu kama mungu upofu tu na ushirikina; bila maarifa halisi juu ya Mungu, binadamu hawawezi kutenda kulingana na njia ya Mungu, ama kumcha Mungu, ama kuepuka maovu. Badala yake, kila tendo na tabia ambayo mwanadamu anashiriki litajaa uasi na kutotii, na kumbukumbu zinazokashifu na hukumu ya usengenyaji kumhusu Yeye, na mienendo miovu inayokwenda kinyume na ukweli na maana ya kweli ya maneno ya Mungu.


        Punde wanadamu wanapokuwa na imani ya kweli kwa Mungu, watakuwa wa kweli katika kumfuata Yeye na kumtegemea; kwa imani ya kweli pekee na tegemeo kwa Mungu ndipo binadamu watakuwa na kuelewa kwa kina na ufahamu; pamoja na ufahamu wa kweli wa Mungu inakuja kumjali Kwake kwa kweli; ni kwa kumjali Mungu kwa kweli pekee ndipo binadamu watakuwa na utiifu wa kweli kwa Mungu; na ni kwa utiifu wa Mungu kwa kweli pekee ndipo binadamu watakuwa na uwekaji wakfu wa kweli; na ni kwa uwekaji wakfu wa kweli kwa Mungu pekee ndipo binadamu watakuwa na malipo yasiyo na kiwango na kulalamika; ni kwa imani na msimamo wa kweli, kuelewa na kujali kwa kweli, utiifu wa kweli, utakatifu wa kweli na malipo, ndipo binadamu watakuja kujua kwa kweli tabia na kiini cha Mungu, na kujua utambulisho wa Muumba; Watakapopata kumjua Muumba ndipo binadamu wataamsha ndani yao ibada ya kweli na kujisalimisha; watakapokuwa na ibada ya kweli na kujisalimisha kwa Muumba tu ndipo binadamu wataweza kwa kweli kuweka kando njia zao za uovu, hivyo ni kusema, kuepuka maovu.


        Hii inajumlisha hatua yote ya “kumcha Mungu na kuepuka maovu” na pia ni maudhui katika kumcha Mungu na kuepuka maovu kwa ujumla, na pia njia ambayo ni lazima kupitia ili kufikia kumcha Mungu na kuepuka maovu.


        “Kumwogopa Mungu na kuepuka maovu” na kumjua Mungu ni uhusiano usiogawanyishwa na uliounganishwa kwa nyuzi zisizohesabika, na uhusiano kati yao ni dhahiri. Iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kuepuka maovu, lazima kwanza amche Mungu kwa kweli; iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kumcha Mungu kwa kweli, lazima awe na maarifa ya kweli kuhusu Mungu; Iwapo mtu anataka kupata maarifa ya Mungu, lazima kwanza ayapitie maneno ya Mungu, aingie katika ukweli wa maneno ya Mungu, apitie kuadibu na nidhamu ya Mungu, kuadibu Kwake na hukumu; iwapo mtu anataka kupitia maneno ya Mungu, lazima aje ana kwa ana na maneno ya Mungu, aje ana kwa ana na Mungu, na kumwomba Mungu Ampe fursa ya kupitia maneno ya Mungu katika hali ya aina yote ya mazingira inayowahusisha watu, matukio na vitu; iwapo mtu anataka kuja ana kwa ana na Mungu na maneno ya Mungu, lazima kwanza amiliki moyo wa kweli na mwaminifu, awe tayari kuukubali ukweli, kukubali kupitia mateso, uamuzi na ujasiri wa kuepuka uovu, na azimio la kuwa kiumbe halisi…Kwa njia hii, kuendelea mbele hatua kwa hatua, utamkaribia Mungu zaidi, moyo wako utakuwa safi zaidi, na maisha yako na thamani ya kuwa hai, pamoja na maarifa yako kumhusu Mungu, yatakuwa ya maana zaidi na yatakuwa hata ya kupevuka zaidi. Mpaka siku moja, utahisi kuwa Muumba sio fumbo tena, kwamba Muumba hajawahi kufichwa kutoka kwako, kwamba Muumba hajawahi kuificha sura Yake kutoka kwako, kwamba Muumba hayuko mbali na wewe hata kidogo, kwamba Muumba siye yule unayemtamania katika mawazo yako lakini kwamba huwezi kumfikia na hisia zako, kwamba Anasimama kwa kweli kama mlinzi kulia na kushoto kwako, Akiruzuku maisha yako, na kudhibiti majaliwa yako. Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho. Mungu kama huyo Anakukubali umpende kutoka moyoni, umshikilie, umweke karibu, umtamani, uhofu kumpoteza, na kutotaka kumkataa tena, kutomtii tena, ama kumwepuka tena ama kumweka mbali. Kile unachotaka ni kumjali tu, kumtii, kulipia kila kitu Anachokupa, na kujisalimisha katika himaya Yake. Hukatai tena kuongozwa, kupewa, kuangaliwa, na kuwekwa na Yeye, hukatai tena Anachoamuru na kukitawaza kwako. Unachotaka tu ni kumfuata, kutembea kando Yake katika kushoto ama kulia Kwake, kile utakacho ni kumkubali kama maisha yako ya pekee, kumkubali kama Bwana wako mmoja na wa pekee, Mungu wako mmoja na wa pekee.


Agosti 18, 2014 

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING