Jichunguzeni ili kuona kama mnatenda uhaki katika kila jambo mnalotenda, na iwapo matendo yenu yote yanachunguzwa na Mungu: Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo wale wanaomwamini Mungu wanafanya shughuli zao. Mtaitwa wenye haki kwa sababu mnaweza kukidhi matakwa ya Mungu, na kwa sababu mnakubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji, na wale wanaopatwa na Yeye, ni wenye haki, na Yeye huwatazama wote kama wenye thamani. Jinsi mnavyozidi kukubali maneno ya sasa ya Mungu, ndivyo mtakavyozidi kuweza kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu zaidi, na ndivyo basi mtakavyoweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu zaidi na kukidhi mahitaji Yake. Hili ndilo agizo la Mungu kwenu na ni lile nyote mnapaswa kuweza kulifikia. Mkitumia dhana zenu wenyewe kumpima na kumwekea Mungu mipaka, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiyobadilika, na mkiwekea Mungu mipaka katika vigezo vya Biblia kabisa na kumweka katika wigo wenye mipaka wa kazi, basi hili linathibitisha kwamba mmemshutumu Mungu. Kwa sababu Wayahudi katika Agano la Kale walimchukulia Mungu kuwa sanamu yenye umbo usiobadilika waliyoshikilia mioyoni mwao, kana kwamba Mungu angeweza tu kuitwa Masihi, na Yule pekee aliyeitwa Masihi ndiye angeweza kuwa Mungu, na kwa sababu wanadamu walimtumikia na kumwabudu Mungu kana kwamba Alikuwa sanamu ya udongo (isiyo na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—basi Yesu asiye na hatia alihukumiwa kifo. Mungu hakuwa na kosa lolote, ilhali mwanadamu alikataa kumsamehe, na alishikilia kumhukumu Yeye kifo na basi Yesu Akasulubishwa. Mwanadamu kila wakati huamini kuwa Mungu habadiliki na humfafanua kwa msingi wa kitabu kimoja tu, Biblia, kana kwamba mwanadamu amepenyeza kabisa usimamizi wa Mungu, kana kwamba mwaadamu amepata kila kitu Atendacho Mungu katika kiganja cha mkono wake. Wanadamu ni wapumbavu kupita kiasi, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha kutia chumvi sana wanapoelezea vitu. Bila kujali kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu, bado Nasema kwamba humfahamu Mungu, kwamba wewe ni mtu ambaye humpinga Mungu zaidi, na kwamba umemshutumu Mungu, kwa sababu huna uwezo wa kuiheshimu kazi ya Mungu kabisa na kutembea katika njia ya kufanywa kuwa kamili na Mungu. Ni kwa nini Mungu hatosheki kamwe na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hamjui Mungu, kwa sababu ana dhana nyingi sana, na kwa sababu maarifa yake ya Mungu hayaafikiani na uhalisi hata kidogo, lakini badala yake kwa uchovu hurudia tu mada ile ile bila mabadiliko na hutumia mwelekeo ule ule katika kila hali. Na hivyo, kwa kuwa amekuja duniani leo, Mungu Anasulubishwa kwa mara nyingine na mwanadamu. Wanadamu dhalimu! Kufumba watu macho na kula njama, kupokonyana na kunyang’anya mmoja kutoka kwa mwingine, kung’ang’ania umaarufu na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Licha ya mamia ya maelfu ya maneno ambayo Mungu amezungumza, hakuna hata mmoja ambaye amejirudi. Watu wanatenda matendo kwa ajili ya familia zao, watoto wao, kazi zao, matarajio yao ya baadaye, cheo, majivuno, na pesa, kwa sababu ya chakula, mavazi, na mwili, lakini kuna yeyote ambaye matendo yake kwa kweli ni kwa ajili ya Mungu? Hata miongoni mwa wale ambao wanatenda kwa ajili ya Mungu, ni wachache tu wanaomfahamu Mungu. Ni watu wangapi hawatendi kutokana na maslahi yao? Ni wangapi wasiokandamiza na kutenganisha wengine ili kulinda cheo chao wenyewe? Na hivyo, Mungu amehukumiwa kifo mara nyingi kwa nguvu, na mahakimu wakatili wasiohesabika wamemhukumu Mungu na mara nyingine wakamsulubisha msalabani. Wangapi wanaweza kuitwa wenye haki kwa sababu wanatenda mambo kwa ajili ya Mungu kwa kweli?
Je, ni rahisi vile kukamilishwa mbele ya Mungu, kama mtakatifu au mtu mwenye haki? Ni kauli ya ukweli kwamba, “hakuna wenye haki katika dunia hii, wenye haki hawapo katika dunia hii.” Mnapokuja mbele za Mungu, fikirieni kile mnachovaa, tafakarini juu ya kila neno na tendo lenu, juu ya fikira na mawazo yenu yote na hata ndoto mnazoota kila siku—zote ni kwa manufaa yenu. Je, hivi sivyo hali halisi ilivyo? “Haki” haimaanishi kuwatolea wengine sadaka wala haimaanishi kumpenda jirani yako vile unavyojipenda na haimaanishi kuepukana na magombano na ugomvi, au kunyang’anya na kuiba. Haki inamaanisha kuchukua agizo la Mungu kama kazi yako na kuiheshimu mipango na utaratibu wa Mungu kama wito wako utokao mbinguni, bila kujali wakati ama mahali, kama tu yote ambayo Bwana Yesu Aliyafanya. Hii ndiyo haki ambayo Amezungumzia Mungu. Kwamba Lutu aliweza kuitwa mwenye haki ni kwa sababu aliwaokoa wale malaika wawili waliotumwa na Mungu bila kuzingatia faida ama hasara yake mwenyewe; inaweza kusemwa tu kwamba alichotenda katika huo wakati kinaweza kuitwa haki, lakini hawezi kuitwa mwanadamu mwenye haki. Ilikuwa tu kwa sababu Lutu alikuwa amemwona Mungu ndipo akatoa wasichana wake wawili badala ya malaika, lakini si tabia yake yote ya hapo awali iliwakilisha haki. Na hivyo Nasema “hakuna wenye haki katika dunia hii.” Hata kati ya wale ambao wako katika mkondo wa urejesho, hakuna hata mmoja anayeweza kuitwa mwenye haki. Haijalishi matendo yako ni mazuri vipi, haijalishi jinsi unavyoonekana kulisifu jina la Mungu, kutowapiga na kuwalaani wengine, wala kuwaibia na kuwapora wengine, huwezi kuitwa mwenye haki bado, kwa sababu haya ndiyo mtu wa kawaida ana uwezo wa kuwa nayo. Kilicho muhimu sasa ni kwamba wewe humfahamu Mungu. Inaweza tu kusemwa kwamba hivi sasa una ubinadamu wa kawaida wa kiasi kidogo, lakini hakuna vipengele vya haki viliyozungumziwa na Mungu, na hivyo hakuna unachotenda ambacho kinaweza kuthibitisha kwamba unamfahamu Mungu.
Hapo awali, Mungu Alipokuwa mbinguni, mwanadamu alitenda matendo yake kwa namna isiyo ya dhati. Leo, Mungu amekuwa miongoni mwa wanadamu—hakuna anayejua ni kwa miaka ngapi—ilhali katika kufanya mambo mwanadamu bado anatenda kwa namna isiyo ya dhati na anajaribu kumdanganya. Je, si mwanadamu yuko nyuma sana katika fikira zake? Ndivyo ilivyokuwa na Yuda: Kabla Yesu aje, Yuda angesema uwongo kuwadanganya ndugu zake, na hata baada ya Yesu kuja, bado hakubadilika; hakumjua Yesu hata kidogo, na mwishowe alimsaliti Yesu. Je, hii haikuwaa kwa sababu hakumfahamu Mungu? Kama leo bado hammfahamu Mungu, basi kuna uwezekano kwamba mnaweza kuwa Yuda mwingine, na kufuatilia hili msiba wa kusulubiwa kwa Yesu katika Enzi ya Neema, maelfu ya miaka iliyopita, utarudiwa tena. Je, hamyaamini hayo? Ni ukweli! Hivi sasa, watu wengi wako katika hali kama hiyo—Naweza kuwa Ninayasema haya mapema sana kiasi—na watu wa aina hii wote ni wahusika wanaochukua nafasi ya Yuda. Sizungumzi upuzi, bali kwa msingi wa ukweli—na huna budi ila kuridhishwa. Ingawa watu wengi wanajifanya kuwa wanyenyekevu, katika mioyo yao hakuna kingine ila dimbwi la maji yaliyokufa, handaki la maji yanayonuka. Hivi sasa kuna wengi sana wa aina hii katika kanisa. Je, mnafikiri Sina habari yoyote kuhusu hili? Leo, Roho Wangu huniamulia na kunishuhudia. Unafikiri kwamba Sijui lolote? Je, unafikiri Sielewi fikira za ujanja katika mioyo yenu, vitu mnavyoweka katika mioyo yenu? Je, ni rahisi vile kumdanganya Mungu? Je unafikiri kwamba unaweza kumtendea kwa njia ile unayotaka? Hapo zamani, nikiwa na wasiwasi msije mkazuiwa, Niliendelea kuwapa uhuru, lakini wanadamu hawakuweza kutambua kwamba Nilikuwa mzuri kwao na Nilipowapa kidogo walitaka mengi. Ulizieni kati yenu: Nusura sijawahi kumshughulikia yeyote, na nusura sijawahi kumkemea yeyote juujuu—ilhali Sina tashwishi juu ya motisha na dhana za mwanadamu. Je, unafikiri Mungu Mwenyewe, ambaye Mungu Anamshuhudia, ni mjinga? Hali ikiwa hivyo, Ninasema wewe ni kipofu sana! Sitakukaripia, lakini hebu tu tuone utakavyoweza kupotoka. Hebu tuone iwapo werevu wako mdogo unaweza kukuokoa, ama iwapo kujaribu kadri uwezavyo kumpenda Mungu kutakuokoa. Leo, Sitakushutumu; hebu tungoje mpaka wakati wa Mungu tuone Atakavyokuadhibu. Sina wakati wa kupoteza kufanya maongezi yasiyo muhimu na wewe sasa, na Sina nia ya kuchelewesha kazi Yangu kuu kwa ajili yako tu. Buu kama wewe hastahili muda utakaomchukua Mungu kukushughulikia—kwa hivyo hebu tuone tu jinsi unaweza kuwa mpotovu. Watu kama hawa hawafuatilii ufahamu wa Mungu hata kidogo, wala hawana upendo hata kidogo Kwake, na bado wanataka Mungu awaite wenye haki—Je, huu si utani? Kwa sababu idadi ndogo ya watu kweli ni waaminifu, Mimi nitajishughulisha tu na kuzidi kumpa mwanadamu uhai. Nitakamilisha tu kile ninachohitaji kukamilisha leo, lakini katika siku zijazo nitaleta adhabu kwa kila mmoja kulingana na kile ambacho amekifanya. Nimesema yote yanayopaswa kusemwa, kwa sababu hii hasa ndiyo kazi Ninayoifanya. Ninafanya kile tu Ninachopaswa kukifanya, na si kile Nisichopaswa kukifanya. Hata hivyo, Natumai kwamba utatumia muda zaidi kutafakari: Kiwango gani hasa cha ufahamu wako wa Mungu ni wa kweli? Je wewe ni mtu ambaye amemsulubisha Mungu kwa mara nyingine? Maneno yangu ya mwisho ni haya: Ole wao wale wamsulubishao Mungu.