21 Jul
Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kufaa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, lazima kwanza uutoe moyo wako kwa Mungu, na uuweke moyo wako uwe mtulivu mbele za Mungu. Baada tu ya kuutoa moyo wako mzima katika Mungu ndipo utaweza kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho hatua kwa hatua. Kama, kwa imani yao katika Mungu, watu hawautoi moyo wao kwa Mungu, ikiwa moyo wao hauko katika Mungu, na wala hawauchukulii mzigo wa Mungu kama wao wenyewe, basi kila kitu wanachofanya ni kumdanganya Mungu, nayo ni matendo ya watu wa kidini, wasioweza kuipokea sifa ya Mungu. Mungu hawezi kupata kitu chochote kutoka kwa aina hii ya mtu; aina hii ya mtu anaweza tu kutumika kama foili[a] kwa kazi ya Mungu, kama pambo katika nyumba ya Mungu, kuchukua nafasi, naye hana manufaa—Mungu hamtumii aina hii ya mtu. Katika mtu kama huyo, sio tu kwamba hakuna nafasi kwa ajili ya kazi ya Roho Mtakatifu, hata zaidi hakuna thamani ya ukamilifu; aina hii ya mtu ni “mfu atembeaye” halisi—hana sehemu ambazo zinaweza kutumika na Roho Mtakatifu—wao wote wametwaliwa na Shetani, kupotoshwa kwa kiwango kilichokithiri na Shetani, ambao ni chombo cha kuondolewa na Mungu. Kwa sasa Roho Mtakatifu hawatumii tu watu kwa kuyaweka maadili yao katika matumizi, lakini pia kuwakamilisha na kubadilisha dosari zao. Kama moyo wako unaweza kumiminwa ndani ya Mungu, na kukaa kimya mbele za Mungu, basi utakuwa na nafasi na sifa za kuhitimu ili kutumiwa na Roho Mtakatifu, kupokea nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na hata zaidi, utakuwa na nafasi kwa Roho Mtakatifu kufidia dosari zako. Unapoutoa moyo wako kwa Mungu, unaweza kuingia kwa undani zaidi kwenye upande mzuri na kuwa kwenye kiwango cha juu zaidi cha uelewaji; katika upande hasi, utakuwa na uelewa zaidi wa makosa na dosari zako mwenyewe, utakuwa na hamu zaidi ya kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu, na hutakuwa katika hali ya kukaa tu, utaingia ndani kwa utendaji. Hii itamaanisha kuwa wewe ni mtu sahihi. Katika kigezo cha kwamba moyo wako uko shwari mbele za Mungu, jambo muhimu kama unapokea sifa kutoka kwa Roho Mtakatifu au la na kama unampendeza Mungu au la ni kama unaweza kuingia ndani kwa utendaji. Wakati Roho Mtakatifu anampa mtu nuru na anamtumia mtu, Hamfanyi hasi kamwe, lakini mara zote Humfanya aendelee kwa utendaji. Hata kama ana udhaifu, anaweza kutoishi kulingana nao, anaweza kuepukana na kuchelewesha kukuza maisha yake, naye anaweza kuendelea kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu. Hiki ni kiwango ambacho kinathibitisha kwa utoshelevu kwamba mtu ameupata uwepo wa Roho Mtakatifu. Ikiwa mtu yuko hasi daima, na hata baada ya kupata nuru ili kujijua bado yuko hasi na wa kukaa tu, bila uwezo wa kusimama na kutenda pamoja na Mungu, basi aina hii ya mtu anaipokea tu neema ya Mungu, bali Roho Mtakatifu hayuko naye. Mtu akiwa hasi, hii inamaanisha kuwa moyo wake haujamgeukia Mungu na roho yake haijaguswa na Roho wa Mungu. Hii inapaswa kutambuliwa na wote.

Katika uzoefu wako unaona kuwa moja ya masuala muhimu zaidi ni kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Ni suala ambalo linahusu maisha ya kiroho ya watu, na kuendelea kwa maisha yao. Ni kama tu moyo wako uko na amani mbele za Mungu ndio kutafuta kwako ukweli na mabadiliko katika tabia yako kutazaa matunda. Kwa sababu unakuja ukiwa na mizigo mbele za Mungu na huwa unahisi kila mara kuwa unapungukiwa kiasi kikubwa, kwamba kuna ukweli mwingi ambao unahitaji kujua, uhalisi mwingi unaohitaji kupitia, na kwamba unapaswa kujali kikamilifu kuhusu mapenzi ya Mungu—mambo haya kila mara huwa mawazoni mwako, ni kana kwamba yamekufinyia chini sana kiasi kwamba huwezi kupumua, na hivyo unahisi mzito wa moyo (lakini sio kwa hali hasi). Ni watu wa aina hii pekee ndio wanastahili kukubali kupata nuru ya maneno ya Mungu na kuguswa na Roho wa Mungu. Ni kwa sababu ya mzigo wao, kwa sababu ni wenye moyo mzito, na, inaweza kusemwa, kwa sababu ya gharama ambayo wamelipa na mateso ambayo wamepitia mbele ya Mungu ndio wanapata nuru na mwangaza wa Mungu, kwa kuwa Mungu hamtendei yeyote kwa upendeleo. Yeye huwa mwenye haki kila mara katika kuwatendea watu, lakini Yeye sio holela katika kuwakimu watu, na hawapi bila masharti. Huu ni upande mmoja wa tabia Yake yenye haki. Katika maisha halisi, watu wengi bado hawajaufikia ulimwengu wa aina hii. Kwa kiwango cha chini zaidi, mioyo yao bado haijamgeukia Mungu kikamilifu, na hivyo bado hakujakuwa na mabadiliko yoyote makubwa katika tabia ya maisha yao. Hii ni kwa sababu wanaishi tu kati ya neema ya Mungu, na bado hawajapata kazi ya Roho Mtakatifu. Vigezo vya Mungu kuwatumia watu ni kama ifuatavyo: Mioyo yao inamgeukia Mungu, wanasumbuliwa na maneno ya Mungu, wanakuwa na mioyo ya kutamani, na wako na azimio la kutafuta ukweli. Ni watu wa aina hii tu ndio wanaoweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu na mara kwa mara wapate nuru na mwangaza. Watu ambao Mungu hutumia huonekana kwa nje kama watu wasio na akili na huonekana kama wasio na uhusiano wa kawaida na wengine, ingawa wao huzungumza na adabu, hawazungumzi kiholela, na wanaweza daima kuwa na moyo uliotulia mbele ya Mungu. Lakini ni mtu wa aina hiyo tu ndiye anatosha kutumiwa na Roho Mtakatifu. Mtu huyu asiye na akili anayezungumziwa na Mungu anaonekana kama asiye na uhusiano wa kawaida na wengine, na hana upendo wa kuelekea nje au matendo ya juu juu, lakini anapokuwa akieleza mambo ya kiroho anaweza kufungua roho yake na kwa kujinyima awatolee wengine mwangaza na nuru ambayo amepata kutoka kwa uzoefu wake wa hakika mbele za Mungu. Hivi ndivyo anavyodhihirisha upendo wake kwa Mungu na kuridhisha mapenzi ya Mungu. Wengine wote wanapokuwa wanamkashifu na kumdhihaki, ana uwezo wa kutoelekezwa na watu wa nje, matukio, au vitu, na bado anaweza kutulia mbele za Mungu. Mtu wa aina hii inavyooneka yuko na utambuzi wake mwenyewe wa pekee. Bila kujali wengine, moyo wake kamwe haumwachi Mungu. Wengine wanapokuwa wakizungumza kwa furaha na kwa vichekesho, moyo wake bado unasalia mbele za Mungu, kutafakari neno la Mungu au kusali kwa kimya kwa Mungu aliye moyoni mwake, akitafuta makusudi ya Mungu. Kamwe hafanyi udumishaji wa uhusiano wao na wengine lengo lake la msingi. Mtu wa aina hii inavyoonekana hana falsafa ya maisha. Kwa nje, mtu huyu ni mchangamfu, anayependwa, asiye na hatia, lakini pia anamiliki hisia ya utulivu. Huu ni mfano wa mtu ambaye Mungu anamtumia. Mambo kama falsafa ya maisha au “mantiki ya kawaida” hayawezi kupenya kwa mtu wa aina hii; mtu wa aina hii ameutoa moyo wake wote kwa neno la Mungu, ambaye anaonekana kuwa na Mungu tu katika moyo wake. Hii ni aina ya mtu ambaye Mungu anamrejelea kama mtu “bila mantiki,” naye tu ni mtu ambaye anatumiwa na Mungu. Alama ya mtu ambaye anatumiwa na Mungu ni: Haijalishi ni lini au wapi, moyo wake daima uko mbele za Mungu, na haijalishi jinsi gani wengine ni wenye anasa, jinsi gani wanavyoshiriki katika tamaa, wanajiingiza katika anasa za kimwili—moyo wake kamwe haumwachi Mungu, naye hafuatani na umati. Aina hii ya mtu pekee ndiye anafaa kwa ajili ya matumizi ya Mungu, naye hasa ni yule ambaye amekamilika na Roho Mtakatifu. Ikiwa huwezi kufikia hatua hii, basi hustahili kupatwa na Mungu, ili kukamilishwa na Roho Mtakatifu.

Ikiwa unataka kuwa na uhusiano wa kufaa na Mungu, lazima moyo wako umgeukie Mungu, na juu ya msingi huu, pia utakuwa na uhusiano wa kufaa na watu wengine. Iwapo huna uhusiano unaofaa na Mungu, haijalishi unachofanya kudumisha uhusiano wako na watu wengine, haijalishi jinsi gani unafanya kazi kwa bidii au ni nguvu kiasi gani unaweka ndani yake, bado ni ya falsafa ya mwanadamu ya maisha. Unadumisha nafasi yako miongoni mwa watu kupitia mtazamo wa mwanadamu na falsafa ya mwanadamu ili kwamba wakupe wewe sifa. Hauundi uhusiano unaofaa na watu kulingana na neno la Mungu. Iwapo hutilii maanani uhusiano wako na watu lakini unadumisha uhusiano unaofaa na Mungu, ikiwa uko tayari kumpa Mungu moyo wako na ujifunze kumtii, kwa kawaida sana, uhusiano wako na watu wote utakuwa unaofaa. Kwa njia hii, uhusiano huu haujengwi kwa mwili, bali juu ya msingi wa upendo wa Mungu. Kwa kiasi kikubwa hakuna ushirikiano uliojengwa juu ya mwili, lakini katika roho kuna ushirikiano na vilevile upendo, starehe, na kutoleana kwa wenza. Haya yote yanafanywa kwa msingi wa moyo unaomridhisha Mungu. Uhusiano huu haudumishwi kwa kutegemea falsafa ya mwanadamu ya maisha, bali unaundwa kwa kawaida kupitia mzigo wa Mungu. Hauhitaji jitihada za binadamu—unawekwa katika matendo kupitia maadili ya neno la Mungu. Je, unayo hiari ya kuwa mwenye kufikiria mapenzi ya Mungu? Je, uko tayari kuwa mtu “bila mantiki” mbele za Mungu? Je, uko tayari kuutoa moyo wako kwa Mungu kabisa, na kutofikiri kuhusu msimamo wako kati ya watu? Kati ya watu wote ambao una mawasiliano nao, ni gani ambao kati yao unayo mahusiano bora zaidi? Wepi kati yao ambao unayo mahusiano mabaya zaidi nao? Je, mahusiano yako na watu ni ya kufaa? Je, unawachukulia watu wote kwa usawa? Je, uhusiano wako na wengine umeimarishwa kwa mujibu wa falsafa yako ya maisha, ama umejengwa kwenye msingi wa upendo wa Mungu? Wakati mtu hautoi moyo wake kwa Mungu, basi roho yake inakuwa butu, inakufa ganzi na kutofahamu. Aina hii ya mtu kamwe hataelewa maneno ya Mungu na kamwe hatakuwa na uhusiano wa kufaa na Mungu; aina hii ya mtu kamwe hatabadilisha tabia yake. Kubadilisha tabia ya mtu ni mchakato wa mtu kuutoa kabisa moyo wake kwa Mungu, na wa kupokea nuru na mwangaza kutoka kwa maneno ya Mungu. Kazi ya Mungu inaweza, kumruhusu mtu kuingia kwa utendaji, na pia kumwezesha kuepuka masuala yake hasi baada ya kupata maarifa. Unapoweza kuutoa moyo wako kwa Mungu, utaweza kuhisi kila harakati yenye hila ndani ya roho yako, nawe utajua kila nuru na mwangaza upokelewao kutoka kwa Mungu. Shikilia hili, nawe utaingia katika njia ya kukamilishwa na Roho Mtakatifu hatua kwa hatua. Kadri moyo wako unavyoweza kuwa mtulivu mbele za Mungu, ndivyo roho yako itakavyokuwa makini zaidi na wa kutaka uangalifu mkubwa, na kadri roho yako itakavyoweza kutambua kuchochewa na Roho Mtakatifu, kisha uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kufaa zaidi na zaidi. Uhusiano unaofaa kati ya watu unaundwa juu ya msingi wa kumpa Mungu moyo wako; haufanikishwi kupitia jitihada za binadamu. Bila Mungu mioyoni mwao, uhusiano kati ya watu ni uhusiano wa mwili tu. Sio uhusiano unaofaa, bali ni kujiingiza katika tamaa za mwili—ni uhusiano ambao Mungu anachukia, Asioupenda. Ukisema kuwa roho yako imeguzwa, lakini daima unataka kuwa na ushirika na watu wanaokupendeza, na wale unaowachukulia kwa hali ya juu, na iwapo kuna mtafutaji mwingine ambaye hakupendezi, ambaye huna upendeleo kwake na huwezi kujihusisha naye, huu ni ushahidi zaidi kuwa wewe ni mtu mwenye hisia na kuwa huna uhusiano unaofaa na Mungu kamwe. Unajaribu kumdanganya Mungu na kuficha ubaya wako mwenyewe. Hata ingawa unaweza kushirikisha uelewano kiasi lakini unabeba ubaya moyoni mwako, kila kitu unachofanya ni kizuri tu kwa kiwango cha mwanadamu. Mungu hatakusifu—unatenda kulingana na mwili, sio kulingana na mzigo wa Mungu. Iwapo unaweza kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu na kuwa na ushirikiano wa kufaa na wale wote wanaompenda Mungu, ni hapo tu ndipo utakuwa uko tayari kwa matumizi ya Mungu. Kwa njia hii, haijalishi jinsi unavyopatana na wengine, haitakuwa kulingana na falsafa ya maisha, lakini itakuwa kuishi mbele ya Mungu, kuufikiria mzigo Wake. Je, ni watu wangapi wa aina hii wapo miongoni mwenu? Je, mahusiano yako na watu wengine yanafaa kweli? Yamejengwa katika msingi upi? Je, ni falsafa ngapi za maisha zimo ndani mwako? Je, zimetupiliwa mbali? Ikiwa moyo wako hauwezi kumgeukia Mungu kabisa, basi wewe si wa Mungu—unatoka kwa Shetani, na mwishowe utarudishwa kwa Shetani. Wewe hustahili kuwa mmoja wa watu wa Mungu. Yote haya yanahitaji kufikiria kwako kwa makini.

Tanbihi:

a. “Foili” inahusu mtu au kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING