Mtu Ambaye Hupata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Radhi Kutenda Ukweli
Mtu Ambaye Hupata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Radhi Kutenda Ukweli
13 Oct
Mtu Ambaye Hupata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Radhi Kutenda Ukweli
Hapo awali sana, umuhimu wa kuwa na maisha sahihi ya kanisa ulitajwa katika mahubiri. Kwa hivyo ni kwa nini maisha ya kanisa hayajaboreka bado, na bado ni kile kitu kimoja tu cha zamani? Mbona hakuna njia mpya na tofauti kabisa ya maisha? Je, inaweza kuwa sahihi kwa mtu wa miaka ya tisini kuishi kama mfalme wa enzi iliyopita? Ingawa chakula na vinywaji vinaweza kuwa vyakula vitamu vilivyoonjwa mara chache katika enzi zilizopita, hapajakuwa na mabadiliko makubwa katika hali kanisani. Imekuwa kama kuweka divai ya kale katika kiriba kipya. Je, kuna haja gani basi ya Mungu kusema sana? Makanisa katika maeneo mengi hayajabadilika kabisa. Mimi nimeliona kwa macho Yangu na ni wazi katika moyo Wangu; Hata kama sijapata uzoefu wa maisha ya kanisa Mimi Mwenyewe, Nazijua hali za mikusanyiko ya kanisa kama mgongo wa mkono Wangu. Hawajafanya maendeleo mengi. Inarejelea msemo—ni kama kutia divai ya kale katika kiriba kipya. Hakuna kilichobadilika, siyo hata kidogo! Wakati mtu anapowachunga wao huwaka kama moto, lakini wakati hakuna mtu hapo kuwafadhili, wao ni kama pande kubwa la barafu. Si wengi wanaoweza kuzungumza juu ya mambo ya vitendo, na ni mara chache mtu yeyote anaweza kushika usukani. Ingawa mahubiri ni ya juu, imekuwa nadra kwa mtu yeyote kupata kuingia. Watu wachache hutunza neno la Mungu. Wao hujawa na machozi wanapolikubali neno la Mungu na kuwa wachangamfu wanapoliweka kando; Wao husononeka na kuwa wenye huzuni wanapoliondokea. Kwa kusema kweli, nyinyi hamlitunzi neno la Mungu, na hamyaoni kamwe maneno kutoka kinywa Chake mwenyewe kama hazina. Nyinyi huwa na wasiwasi tu mnapolisoma neno Lake, na kuhisi kuchoka mnapolikariri, na inapofika kuliweka neno Lake katika matendo, ni kama kukabiliana na kazi inayohitaji nguvu nyingi kukamilika—hamwezi kuifanya. Nyinyi daima huwa mnachangamka mnaposoma neno la Mungu, lakini mnasahau mnapolitenda. Kwa hakika, maneno haya si lazima yazungumzwe kwa jitihada sana na kurudiwa kwa uvumilivu sana; watu husikiliza tu lakini hawayaweki katika matendo, kwa hiyo kimekuwa kizuizi kwa kazi ya Mungu. Mimi siwezi kukosa kulileta jambo hili kwa mjadala, Mimi siwezi kukosa kulizungumzia. Mimi ninalazimika kufanya hivyo; Siyo kwamba Mimi hufurahia kufunua udhaifu wa wengine. Mnafikiri kwamba matendo yenu yanafaa tu na mnadhani kwamba wakati ufunuo uko kileleni, kwamba mmeingia katika kilele pia? Je, ni rahisi hivyo? Hamchunguzi kamwe msingi ambao uzoefu wenu hatimaye umejengwa juu yake! Kwa wakati huu, mikusanyiko yenu haiwezi kuitwa maisha mazuri ya kanisa kabisa, wala kuwa maisha yafaayo ya kiroho kamwe. Ni mkusanyiko tu wa kundi la watu ambao hufurahia kuzungumza na kuimba. Kusema kweli, hakuna uhalisi mwingi ndani yake. Kulisema kwa dhahiri zaidi, kama hutendi ukweli, u wapi uhalisi? Je, huko siko kujigamba kusema kwamba una uhalisi? Wale ambao daima hufanya kazi ni wa kujigamba na wenye majivuno, wakati ambapo wale ambao hutii daima hutulia na kuinamisha vichwa vyao chini, bila nafasi yoyote ya mazoezi. Watu ambao hufanya kazi huwa hawafanyi chochote ila kuzungumza, kuendelea zaidi na zaidi na mazungumzo yao yenye kuvutia, na wafuasi husikiliza tu. Hakuna mabadiliko ya kuzungumzia; Hizi ni njia tu za zamani! Leo, kuweza kwako kunyenyekea na kutothubutu kuingilia au kutenda makusudi ni kutokana na kuwasili kwa amri za kiutawala za Mungu; siyo mabadiliko uliyoyapata kupitia uzoefu. Ukweli kwamba kuna mambo mengi ambayo huwezi kuyafanya leo ambayo ungeweza kuyafanya jana ni kwa sababu kazi ya Mungu ni dhahiri kiasi kwamba imeshinda watu. Acha Nimuulize mtu fulani, ni kiasi gani cha ufanikishaji wako leo kilichopatikana kwa jasho la kazi ngumu yako mwenyewe? Ni kiasi gani ulichoambiwa moja kwa moja na Mungu? Ungejibu vipi? Je, ungepigwa na bumbuwazi na kutoweza kunena? Ungekosa adabu? Ni kwa nini wengine wanaweza kuzungumza juu ya mengi ya uzoefu wao halisi ili kukuruzuku, wakati ambapo unafurahia tu chakula ambacho wengine wamepika? Je, huoni haya? Je, hutahayari?
Mnaweza kutekeleza uchunguzi wa kutafuta ukweli, kuchunguza watu wengine ambao kwa kulinganisha hufuatilia ukweli: Unaelewa ukweli kiasi gani? Je, ni kiasi gani ambacho wewe hatimaye huweka katika mazoezi? Ni nani unayempenda zaidi, Mungu au wewe mwenyewe? Je, wewe hutoa mara nyingi zaidi, au hupokea mara nyingi zaidi? Je, ni mara ngapi wakati lengo lako lilikuwa lenye kosa umetelekeza nafsi yako ya zamani na kuyaridhisha mapenzi ya Mungu? Maswali haya machache tu yatawakanganya watu wengi. Kwa watu wengi sana, hata kama wakitambua kuwa nia yao si sahihi, bado hufanya makosa makusudi, nao hata hawajakaribia kuinyima miili yao wenyewe. Watu wengi sana huruhusu dhambi kuenea kote ndani yao, wakiruhusu hali ya dhambi kuongoza kila tendo lao. Hawawezi kushinda dhambi zao, na huendelea kuishi katika dhambi. Baada ya kufika kwenye hatua hii ya sasa, ni nani asiyejua ni matendo mangapi mabaya ameyafanya? Ukisema hujui, basi Mimi ningesema kwamba unasema uongo. Kusema ukweli, yote ni kutotaka kutelekeza nafsi yako ya zamani. Je, kuna maana gani ya kusema “maneno mengi kutoka kwa moyo” ya kutubu ambayo hayafai? Je, hili lingekusaidia kukua katika maisha yako? Inaweza kusemwa kwamba kujijua mwenyewe ni kazi yako ya kudumu. Mimi huwafanya watu wakamilifu kupitia utii wao na kutenda kwao kwa maneno ya Mungu. Ukivaa tu neno la Mungu kama jinsi ungevaa nguo zako, ili kuwa tu nadhifu na maridadi, je, hujidanganyi mwenyewe na kuwadanganya wengine? Ikiwa yote uliyonayo ni kuongea na kamwe huyaweki katika matendo, ni kitu gani utakachokifikia?
Watu wengi wanaweza kuzungumza kidogo juu ya matendo na wanaweza kuzungumza kuhusu fikira zao za kibinafsi, lakini mengi yayo ni mwanga kutoka kwa maneno ya wengine. Haijumuishi chochote kutoka kwa matendo yao binafsi kamwe, wala kujumuisha kile wanachokiona kutokana na uzoefu wao. Nimechangua suala hili mapema; usifikiri kwamba sijui chochote. Wewe ni tishio la bure tu, na bado unaongea juu ya kumshinda Shetani, juu ya kutoa ushahidi wa ushindi, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa Mungu? Huu wote ni upuuzi! Je, unadhani kwamba maneno yote ambayo Mungu ameyasema leo ni yako kupendezwa nayo? Kinywa chako hunena juu ya kutelekeza nafsi yako ya zamani na kuweka ukweli katika matendo, lakini mikono yako inafanya vitendo vingine na moyo wako unapanga hila zingine—wewe ni mtu wa aina gani? Kwa nini moyo wako na mikono yako si kitu kimoja? Kuhubiri kwingi sana kumekuwa maneno matupu; si hili ni la kuvunja moyo? Ikiwa umeshindwa kuweka neno la Mungu katika matendo, inathibitisha kuwa bado hujaingia katika njia ambayo Roho Mtakatifu hufanya kazi, bado haujapata kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ndani yako, na bado haujapata mwongozo Wake. Ukisema kuwa unaweza tu kuelewa neno la Mungu lakini umeshindwa kuliweka katika matendo, basi wewe ni mtu asiyependa ukweli. Mungu huwa haji kumwokoa mtu wa aina hii. Yesu alipatwa na maumivu makubwa wakati Yeye aliposulubiwa ili kuwaokoa wenye dhambi, kuwaokoa maskini, kuwaokoa hao watu wanyenyekevu. Kusulubiwa Kwake kulileta sadaka ya dhambi. Ikiwa huwezi kutenda neno la Mungu, basi unapaswa kuondoka haraka unavyoweza; usijikalie pote katika nyumba ya Mungu kama doezi. Watu wengi hata huona vigumu kujizuia kufanya mambo ambayo humpinga Mungu kwa dhahiri. Je, si wanauliza kifo? Wanawezaje kuongea juu ya kuingia katika ufalme wa Mungu? Je, wangekuwa na ujasiri wa kuuona uso Wake? Kula chakula ambacho Yeye hukupa, kufanya mambo ya uhalifu ambayo humpinga Mungu, kuwa mwenye nia mbaya, mwenye kudhuru, na mwenye hila, hata wakati Mungu anakuruhusu kufurahia baraka ambazo Yeye amekupa—je, huzihisi zikiichoma mikono yako unapozipokea? Je, huuhisi uso wako ukigeuka kuwa mwekundu? Baada ya kufanya kitu kinyume na Mungu, baada ya kufanya hila ili “kuwa laghai,” huhisi hofu? Kama huhisi chochote, unawezaje kuzungumza juu ya wakati wowote ujao? Kulikuwa tayari hakuna wakati ujao kwako zamani za kale, kwa hiyo ni matarajio yapi makubwa zaidi unaweza kuwa nayo bado? Ukisema kitu bila haya lakini huhisi hatia, na moyo wako hauna ufahamu, basi haimaanishi kwamba tayari umekataliwa na Mungu? Kuzungumza na kutenda kwa kujiachia na bila kuzuiwa imekuwa asili yako; Je, unawezaje kufanywa mkamilifu na Mungu hivi? Ungeweza kutembea ulimwenguni kote? Ni nani angethibitishiwa na wewe? Wale ambao wanaijua asili yako ya kweli watakaa mbali nawe. Je, si hii ni adhabu ya Mungu? Kwa jumla, ikiwa kuna mazungumzo tu bila matendo, hakuna ukuaji. Ingawa Roho Mtakatifu anaweza kuwa anafanya kazi kwako unapozungumza, kama hutendi, Roho Mtakatifu ataacha kufanya kazi. Ukizidi kuendelea kwa njia hii, kunawezaje kuwa na majadiliano yoyote ya wakati ujao au kutoa nafsi yako yote kwa kazi ya Mungu? Wewe husema tu juu ya kutoa nafsi yako yote, na bado humpi Mungu moyo wako ambao kwa hakika humpenda Yeye. Yote ambayo Mungu amepokea ni moyo wa maneno yako, na siyo moyo wa utendaji wako. Je, hiki kinaweza kuwa ndicho kimo chako cha kweli? Ikiwa ungeendelea kwa jinsi hii, ungefanywa mkamilifu na Mungu lini? Je, huhisi wasiwasi juu ya kesho yako ya giza na majonzi? Je, huhisi kwamba Mungu amepoteza tumaini kwako? Je, hujui kwamba Mungu hutamani kuwapa ukamilisho watu wengi na wapya? Je, vitu vya zamani vingeweza kukacha? Wewe huyazingatii maneno ya Mungu leo: Je, unasubiri kesho?