22 Jul
Maisha Ya Kawaida ya Kiroho Huwaongoza Watu Kwenye Njia Sahihi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mmetembea tu sehemu ndogo sana ya njia ya muumini katika Mungu, na bado hamjaingia kwenye njia sahihi, kwa hiyo bado mko mbali na kutimiza kiwango cha Mungu. Hivi sasa, kimo chenu hakitoshi kuyakidhi mahitaji Yake. Kwa sababu ya ubora wenu wa tabia na vilevile asili yenu ya maumbile ya upotovu, nyinyi daima huichukulia kazi ya Mungu kwa uzembe na hamuichukulii kwa uzito. Hii ni dosari yenu kubwa zaidi. Zaidi ya hayo, hamwezi kuipata njia ya Roho Mtakatifu. Wengi wenu hamuifahamu na hamwezi kuiona kwa dhahiri. Zaidi ya hayo, wengi wenu hamtilii maanani suala hili, na hata hamlichukulii kwa uzito. Mkiendelea kufanya hivi na msipoijua kazi ya Roho Mtakatifu, basi njia ambayo mnaichukua kama muumini katika Mungu itakuwa bure. Hii ni kwa sababu hamfanyi kila liwezekanalo ili kutafuta kutimiza mapenzi ya Mungu, na pia kwa sababu hamshirikiani vizuri na Mungu. Sio kwamba Mungu hajawafanyia kazi, au kwamba Roho Mtakatifu hajawasisimua. Ni kuwa nyinyi ni wazembe sana kiasi kwamba hamuichukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa uzito. Sasa lazima mbadilike mara moja na kutembea njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Hii ndiyo mada kuu ya leo. “Njia hii inayoongozwa na Roho Mtakatifu” ni ili watu wapate nuru katika roho zao, wawe na ufahamu wa neno la Mungu, wapate ufahamu kuhusu njia iliyo mbele yao, na waweze kuingia katika ukweli hatua kwa hatua, na kuja kumwelewa Mungu zaidi na zaidi. Njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu hasa ni kwamba watu wawe na ufahamu zaidi wa neno la Mungu, bila mikengeuko na kuelewa kubaya, ili waweze kutembea ndani yake. Ili kutimiza athari hii, mtahitaji kufanya kazi kwa upatanifu na Mungu, kutafuta njia sahihi ya kutia katika vitendo, na kutembea katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Hii inahusu ushirikiano kwa upande wa mwanadamu, yaani, mnachofanya kutimiza mahitaji ya Mungu kwenu, na jinsi mnavyotenda ili kuingia katika njia sahihi ya imani katika Mungu.

Inaonekana kuwa changamano sana kutembea kwenye njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu, lakini utatambua kuwa mchakato huu ni rahisi zaidi ikiwa njia ya kutenda ni dhahiri kabisa kwako. Ukweli ni kwamba watu wana uwezo wa yote ambayo Mungu anahitaji kutoka kwao—Yeye hajaribu kumfunza nguruwe kuimba. Katika hali zote, Mungu hutafuta kutatua matatizo ya watu na kusuluhisha mahangaiko yao. Nyinyi nyote lazima muelewe hili; msimuelewe Mungu vibaya. Njia ya Roho Mtakatifu ni kulitumia neno la Mungu kuwaongoza watu. Kama ilivyotajwa hapo awali, lazima mpeane mioyo yenu kwa Mungu. Hili ni sharti la kutembea kwenye njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Lazima mfanye hili ili muingie kwenye njia sahihi. Mtu anawezaje kumpa Mungu moyo wake kwa kusudi? Mnapopitia kazi ya Mungu na kumwomba katika maisha yenu ya kila siku, ninyi hufanya hivyo kwa uzembe—ninyi humwomba Mungu huku mkifanya kazi. Je, huku kunaweza kuitwa kumpa Mungu mioyo yenu? Mnafikiria kuhusu mambo ya nyumbani au shughuli za mwili; ninyi daima mna nia mbili. Je, hili linaweza kufikiriwa ni kuituliza mioyo yenu mbele za Mungu? Hii ni kwa sababu moyo wako daima umetawaliwa na tamaa ya mambo ya nje, na hauwezi kumgeukia Mungu. Ikiwa mnataka kweli kuifanya mioyo yenu kuwa na amani mbele za Mungu, lazima mfanye kazi ya ushirikiano kwa makusudi. Hiyo ni kusema, kila mmoja wenu lazima achukue muda kuwa mbali na kila mtu, jambo, na chombo kwa ajili ya ibada zenu binafsi za kiroho, ambapo mtaweza kuleta amani kwa mioyo yenu na kujituliza mbele za Mungu. Mnapaswa kuwa na muhtasari wenu binafsi wa ibada ambapo mnaweza kurekodi ufahamu wenu wa neno la Mungu na jinsi roho zenu zimesisimuliwa, haijalishi kama mnachoandika ni cha kina au ni cha juujuu. Tulizeni mioyo yenu mbele za Mungu kwa kusudi. Ikiwa unaweza kutoa saa moja au mbili kwa maisha ya kiroho ya kweli wakati wa mchana, basi maisha yako siku hiyo yatahisi kusitawishwa na moyo wako utakuwa mchangamfu na bila hatia. Ikiwa unaishi maisha haya ya kiroho kila siku, basi utaweza kumpa Mungu moyo wako zaidi na zaidi, roho yako itakuwa imara zaidi na zaidi, hali yako itakuwa bora zaidi na zaidi, utakuwa na uwezo zaidi wa kutembea katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu, na Mungu atakupa baraka zaidi na zaidi. Lengo la maisha yenu ya kiroho ni kutafuta kwa makusudi na kupata kuwepo kwa Roho Mtakatifu. Sio kuzingatia sheria au kufanya taratibu za dini, bali kutenda kweli pamoja na Mungu na kudhibiti miili yenu. Hiki ndicho mwanadamu anapaswa kufanya, kwa hiyo lazima mtumie juhudi zenu zote ili kufanya hivi. Kadri unavyoshirikiana bora zaidi na kadri unavyojitahidi zaidi, ndivyo utakavyoweza zaidi kugeuza moyo wako kwa Mungu, na ndivyo utakavyozidi kutuliza moyo wako mbele Yake. Mara tu utakapofikia hali fulani, Mungu ataupata moyo wako kabisa. Hakuna atakayeweza kuyumbisha au kuuteka moyo wako, na utakuwa wa Mungu kabisa. Ikiwa unatembea katika njia hii, neno la Mungu litajifichua kwako wakati wote na kukupa nuru kwa kila kitu ambacho huelewei—hii yote inaweza kutimizwa kwa sababu ya ushirikiano wako. Hii ndiyo maana Mungu daima husema, “Wote wanaofanya kazi pamoja na Mimi, Nitawatuza mara mbili.” Lazima muione njia hii kwa dhahiri. Ikiwa mnataka kutembea katika njia sahihi, basi lazima mfanye yote muwezayo kumridhisha Mungu. Lazima mfanye yote muwezayo kufikia maisha ya kiroho. Mwanzoni, huenda usiweze kutimiza mengi katika suala hili, lakini usijiruhusu kurudi nyuma au kugaagaa katika ukanaji—lazima uendelee kufanya kazi kwa bidii! Kadri unavyoishi maisha ya kiroho, ndivyo moyo wako utakavyomilikiwa zaidi na maneno ya Mungu, ukishughulika na mambo haya daima na kuubeba mzigo huu daima. Baada ya hiyo, unaweza kufichua ukweli wako wa ndani kabisa kwa Mungu kupitia maisha yako ya kiroho, mwambie unachotaka kufanya, kile ambacho umekuwa ukifikiri, ufahamu wako na maoni yako mwenyewe ya neno la Mungu. Usizuie chochote, hata kidogo! Jizoeze kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu, mwambie ukweli, na usisite kuzungumza yaliyo moyoni mwako. Kadri unavyofanya hivi, ndivyo utakavyohisi zaidi upendo wa Mungu, na moyo wako utavutiwa zaidi na zaidi kumwelekea Mungu. Wakati ambapo hili litafanyika, utahisi kwamba Mungu ni mpenzi zaidi kwako kuliko mtu mwingine yeyote. Hutawahi kumwacha Mungu kamwe, lolote liwalo. Ikiwa utafanya aina hii ya ibada ya kiroho kila siku na usiiondoe akilini mwako, bali uichukulie kama wito wako katika maisha, basi neno la Mungu litaumiliki moyo wako. Hii ndiyo maana ya kuguswa na Roho Mtakatifu. Itakuwa kana kwamba moyo wako daima umetawaliwa na Mungu, kana kwamba kumekuwa na upendo ndani ya moyo wako daima. Hakuna anayeweza kuliondoa hilo kutoka kwako. Wakati hili litatokea, Mungu ataishi ndani yako kweli na kuwa na nafasi ndani ya moyo wako.

Chanzo: Maisha Ya Kawaida ya Kiroho Huwaongoza Watu Kwenye Njia Sahihi


Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING