Watu wanapozidi kuwa wapokelevu wa maneno ya Mungu, ndivyo wanavyozidi kupata nuru na wanaendelea zaidi kuwa na njaa na kiu ya kufuatilia maarifa ya Mungu. Ni wale tu ambao wanapokea maneno ya Mungu wanaweza kuwa na matukio ya undani zaidi na yenye utajiri zaidi; ni wale tu ambao maisha yao yanakuwa ya kupendeza zaidi na zaidi. Kila mtu ambaye anafuatilia uzima lazima ashughulikie haya kana kwamba ni kazi yake, na ni sharti awe na hisia kuwa hawezi kuishi bila Mungu, na hakuna mafanikio yoyote bila Mungu, na kila kitu ni ubatili bila Mungu. Wanapaswa kuwa na azimio la kutofanya lolote bila uwepo wa Roho Mtakatifu, na kutotaka kutenda lolote kama matendo yao hayazai matunda. Hawapaswi kutenda ili kujiendekeza wenyewe. Matukio ya maisha yanakuja kupitia kupata nuru ya Mungu, na pia ni matunda ya juhudi zenu wenyewe. Mnapaswa kuwa na hitaji la kutokuwa na visingizio kwenu katika kupitia maisha.
Mara nyingine hali zako sio za kawaida—unapoteza uwepo wa Mungu na huwezi kumhisi unapoomba; ni kawaida kuhisi kuogopa nyakati kama hizo. Unapaswa kwa haraka kuanza kutafuta ama Mungu atakuwa mbali nawe, na hutakuwa na Roho Mtakatifu kwa siku moja au mbili, ama mwezi mmoja au miwili, na utakuwa hata zaidi bila kazi Yake. Unapokumbana na hali ya aina hii unakuwa wa kutojali kwa kiasi fulani; unachukuliwa tena mateka na Shetani, na hata unaweza kufanya chochote—kupenda na kuwa na tamanio la pesa, kuwadanganya ndugu, kutazama sinema na video, kucheza “mahjong”, hata kuvuta sigara na kulewa bila kuadhibiwa. Moyo wako unasonga mbali na Mungu, unajaribu kuwa mwenye kujitegemea kwa siri, na unafanya hukumu za kibinafsi juu ya kazi Yake kwa hiari. Katika maswala mengine, ni jambo kubwa kuwa watu wanatenda dhambi na jinsia tofauti bila kuona aibu ama haya. Watu kama hao wanaachwa na Roho Mtakatifu na hata, wamekuwa bila kazi ya Roho Mtakatifu kwa muda mrefu. Yote unayoyaona kwao ni kuwa wanazidi kuwa wenye upotovu, wananyosha mikono yao yenye uovu mbali na mbali, na hatimaye wanakana kuwepo kwa hii njia—wanakuwa mateka wa shetani kupitia kwa dhambi zao. Unapogundua kuwa una uwepo wa Roho Mtakatifu lakini sio kazi Yake, umo kwa hali ya hatari tayari. Unapokosa kuhisi uwepo wa Roho Mtakatifu, umo ukingoni mwa kifo. Unapokosa kutubu bado, utarudishwa kwa Shetani kabisa na kuwa mmojawapo wa wale wanaoondolewa. Kwa hivyo, unapogundua kuwa umo kwa hali ambayo una uwepo wa Roho Mtakatifu (kutotenda dhambi, kushiriki ufisadi, ama kumkataa Mungu waziwazi), lakini unakosa kazi ya Roho Mtakatifu (huguswi kihisia unapoomba, hupati nuru na mwangaza ulio wazi. unapokula na kunywa maneno ya Mungu, wewe una uvivu wa kula na kunywa maneno ya Mungu, unakosa ukuaji maishani, bila mwangaza maalum kwa muda mrefu), nyakati kama hizi lazima uwe mwangalifu. Huwezi kujiendekeza tena ama kuwa mwenye hiari: la sivyo uwepo wa Roho Mtakatifu unaweza kutoweka wakati wowote, kwa hivyo haya matukio ni ya nyakati hatari. Unapokumbana na hali ya aina hii, ni lazima ufanye marekebisho kwa haraka. Kwanza, lazima uombe ili utubu, omba Mungu rehema, omba kwa bidii zaidi; cha mno ni lazima unyamazishe roho yako kwa ajili ya kula na kunywa maneno ya Mungu zaidi, na kwa huu msingi, ni lazima uombe zaidi. Imarisha bidii zako kwa kuimba tenzi za rohoni, kuomba, kula na kunywa maneno ya Mungu, na kufanya wajibu wako. Unapokuwa katika hali ya unyonge zaidi yako; moyo wako unaweza kuingiliwa na Shetani kwa urahisi; kama ni hivyo, moyo wako utaondolewa kutoka kwa Mungu na utarudishwa kwa shetani; baada ya hapo hutakuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu, na itakuwa vigumu zaidi kwako kupata tena kazi ya Roho Mtakatifu. Ni afadhali kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu unapokuwa bado na uwepo Wake, omba Mungu Akupe nuru zaidi, na usimruhusu kuondoka kwako. Unapaswa kuomba, kuimba tenzi za rohoni, kufanya kazi yako, na kula na kunywa maneno ya Mungu ili shetani asiwe na fursa ya kufanya kazi yake. Kwa kufanya hivyo, utafaidika kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Kama hupati urejesho kwa hii njia lakini unangoja tu, utakapopoteza uwepo wa Roho Mtakatifu itakuwa ngumu kupata urejesho, isipokuwa Roho Mtakatifu atembee haswa, akuangazie, na kukupatia nuru; hata hivyo, hali yako haitaweza kuwa na urejesho kwa muda wa siku moja au mbili, ama hata nusu ya mwaka. Hii ni kwa sababu watu wanakuwa na ulegevu na hawana uwezo wa kuendelea katika uzoefu ipasavyo; kwa hivyo, wanaachwa na Roho Mtakatifu. Hata kama umepata urejesho, hutakuwa na uwazi sana kwa kazi ya sasa ya Mungu, kwa sababu, wewe upo nyuma katika kupitia kwako kwa maisha, kana kwamba yameshuka. Si hiki ni kitu cha kuhatarisha maisha? Lakini nawaambia watu kama hao: Hujachelewa sana kutubu sasa, lakini kunalo sharti moja, kuwa lazima ufanye kazi kwa bidii zaidi na huwezi kuwa mvivu. Kama watu wengine wanaomba mara tano kwa siku, unapaswa kuomba mara kumi; kama watu wengine wanakula na kunywa maneno ya Mungu kwa saa mbili kwa siku, unapaswa kuwa na saa nne hadi sita; kama watu wengine wanasikiliza tenzi za rohoni kwa saa mbili, unapaswa angalau kusikiliza kwa siku nusu. Kila mara, jinyamazishe mbele ya Mungu, na kufikiria juu ya upendo wa Mungu; mpaka uguswe kihisia, ili moyo wako ugeuke Kwake, na huthubutu tena kutoka Kwake na kutakuwa na tunda. Ni tu kwa kupitia haya matendo ndipo utaweza kuwa na urejesho wa hali ya kawaida ya hapo awali.
Watu wengine wanatafuta kwa ari, lakini hawawezi kuingia katika njia inayofaa. Hii ni kwa sababu hawajali kabisa na hawamakiniki kwa mambo ya kiroho hata kidogo. Hawajui jinsi ya kuwa na uzoefu wa maneno ya Mungu kamwe, hawajui jinsi uwepo wa Roho Mtakatifu ama kazi ya Roho Mtakatifu ilivyo. Hawa watu wana shauku lakini wamechanganyikiwa; hawafuatilii maisha. Kwa kuwa hawamjui Roho hata kidogo, ama kujua mienendo ya kazi ya Roho Mtakatifu, na hawatambui hali yao ya kiroho. Je, si hii ni aina ya imani iliyochanganyikiwa? Watu kama hawa hawatafaidika na chochote hata kama watatafuta mpaka hatima kabisa. Kiini cha imani ya mwanadamu katika Mungu na kuwa na ukuaji katika maisha kunategemea kuelewa kazi ambayo Mungu anaitenda kupitia kwa uzoefu wako, kuona jinsi Mungu anavyopendeka, na kuelewa mapenzi Yake ili ukaweze kutii mipango yote ya Mungu, na kufanya maneno Yake kutendeka ndani yako kuwa maisha yako, na kumtosheleza Mungu. Na kama una tu na aina ya maisha ya kuchanganyikiwa, humakiniki kwa mambo ya kiroho ama mambo yanayohusu mabadiliko katika tabia za maisha, na hutii bidii kwa ukweli, je, utaweza kupata mapenzi Yake? Kama hutaelewa mahitaji ya Mungu, hutaweza kuwa na uzoefu, na hutapata njia ya utendaji. Lengo la kupitia maneno ya Mungu ni kusisitiza athari ambayo maneno ya Mungu yanatimiza ndani yako, na kumjua Mungu kupitia hayo. Kama unasoma tu maneno ya Mungu na hujui jinsi ya kuwa na uzoefu nayo, je, haionyeshi kuwa huna kuelewa kwa kiroho? Kwa kuwa watu wengine hawawezi kuwa na uzoefu wa maneno ya Mungu sasa, hawajui kazi Yake; Je, si huu ni utendaji wenye kasoro? Kama haya yataendelea, je, uzoefu ulio na utajiri na ukuaji maishani utatimika lini? Je, si itakuwa ni mazungumzo matupu? Kuna wengi kati yenu ambao wanazingatia mafundisho; hawana ufahamu ya mambo ya kiroho, na bado wanataka Mungu awatumie kwa jambo kuu na kubarikiwa na Yeye. Hii haina uhalisi kamwe! Kwa hivyo, mnapaswa kurekebisha kwa ajili ya huu upungufu ili mkaweze kuingia maisha yenu ya kiroho kwa njia ifaayo, kuwa na uzoefu wa kweli, na kwa kweli kuingia kwa uhalisi wa maneno ya Mungu.