Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?
Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?
12 Nov
Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?
Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, umepokea utukufu mkuu na wokovu wa Mungu kabisa. Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu wake kutoka kwa Israeli, watu wake wateule, hadi kwako, ili kufanya kusudio lake lijidhihirishe kwenu kama kundi. Kwa hiyo, ninyi ndio mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu. Pengine utayakumbuka maneno haya: “Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.” Zamani, mlisikia msemo huu, lakini hakuna aliyeelewa maana kamili ya maneno yale. Leo, unajua vyema umuhimu wa maneno yale. Maneno haya ndiyo yatakayotimizwa na Mungu katika enzi za mwisho. Yatatimia kwa wale walioteswa na joka kuu jekundu katika sehemu linakoishi. Joka kuu jekundu humtesa Mungu na ni adui wa Mungu, kwa hiyo katika nchi hii, wanaomwamini Mungu wanateswa na kudhihakiwa. Ndiyo sababu maneno haya yatakuja kuwa kweli kwenu nyie kundi la watu. Kazi inapotekelezwa katika nchi inayompinga Mungu, kazi Yake yote inakabiliwa na vizuizi vya kupita kiasi, na mengi ya maneno Yake hayawezi kutimizwa katika wakati ufaao: ndiyo maana, watu husafishwa kwa ajili ya neno la Mungu. Hiki pia ni kipengele cha mateso. Ni vigumu kabisa kwa Mungu kutekeleza kazi yake katika nchi yenye joka kuu jekundu, lakini ni kupitia ugumu huu ndipo Mungu Hupiga hatua katika kazi Yake ili kudhihirisha hekima Yake na matendo Yake ya ajabu. Mungu Huchukua fursa hii kuwakamilisha watu hawa wa kikundi hiki. Kwa ajili ya mateso ya watu, tabia yao na hulka ya kishetani ya watu katika nchi hii najisi, Mungu Anafanya kazi Yake ya kutakasa na ushindi, ili, kutokana na hili, apokee utukufu na kuwapata wale wote wanaoshuhudia matendo Yake. Huu ndio umuhimu wa kujitoa kwa Mungu kwa ajili ya kikundi hiki cha watu. Ina maana kuwa Mungu hufanya kazi ya ushindi kupitia wale wanaompinga. Kufanya vile tu ndiko kunaweza kudhihirisha nguvu kuu za Mungu. Kwa maneno mengine, ni wale tu walio katika nchi najisi ndiyo wanaostahili kuurithi utukufu wa Mungu na ni hili tu ambalo litafanya nguvu kuu za Mungu kuwa maarufu. Ndiyo maana Nasema kuwa utukufu wa Mungu unapatikana katika nchi najisi na kwa wale wanaoishi humo. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu. Hii ni kama tu ilivyokuwa katika kazi ya Yesu; Angetukuzwa tu kati ya Mafarisayo waliomdhihaki. Isingelikuwa mateso na usaliti wa Yuda, Yesu asingelidhihakiwa na kudharauliwa, na hata zaidi kusulubiwa, na hivyo asingelipokea utukufu. Kila mara Mungu Anapofanya kazi katika wakati fulani na kila mara anapofanya kazi Yake kwa kupitia mwili, huwa Anapokea utukufu na papo hapo huwapata Anaotaka kuwapata. Huu ndio mpango wa kazi ya Mungu na hivi ndivyo anavyosimamia kazi Yake.
Katika mpango wa Mungu wa miaka elfu kadhaa, kazi inayofanywa ndani ya mwili ni katika sehemu mbili: Kwanza ni kazi ya kusulubiwa, ambayo kwayo anatukuzwa; nyingine ni kazi ya ushindi na ukamilifu katika nyakati za mwisho, ambayo kwayo pia Atapokea utukufu. Huu ni usimamizi wa Mungu. Hivyo basi, usichukulie kazi ya Mungu au agizo Lake kwako kuwa rahisi sana. Ninyi ndio warithi wa uzito wa milele wa utukufu wa Mungu, hili liliteuliwa na Mungu. Katika sehemu hizo mbili za utukufu wa Mungu, moja inafichuliwa ndani yako; ukamilifu wa sehemu moja ya utukufu Wake umepewa ili uwe urithi wako. Huku ndiko kutukuzwa kutoka kwa Mungu na mpango wake uliopangwa kitambo. Kutokana na ukuu wa kazi aliyoifanya Mungu katika nchi ambako joka kuu jekundu linaishi, kazi kama hii, ikipelekwa katika sehemu nyingine, ingezaa tunda zuri kitambo na ingekubaliwa na mwanadamu kwa urahisi. Na kazi kama hii ingekuwa rahisi sana kukubaliwa na viongozi wa dini wa Magharibi wanaomwamini Mungu, kwani kazi ya Yesu ni kama kielelezo. Ndio maana Hawezi kutekeleza hatua hii ya kazi ya utukufu mahali pengine; yaani, kwa kuwa kuna uungaji mkono kwa watu wote na utambulisho wa mataifa yote, hamna mahali ambapo utukufu wa Mungu unaweza “kupumzikia.” Na huu ndio umuhimu wa kipekee wa hatua hii ya kazi katika nchi hii. Kati yenu, hamna mtu mmoja anayepokea ulinzi wa sheria; badala yake, unaadhibiwa na sheria, na ugumu mkubwa zaidi ni kuwa hapana mtu anayekuelewa, awe ni jamaa yako, wazazi wako, marafiki wako, ama watendakazi wenzako. Hakuna anayekuelewa. Mungu “Anapokukataa,” hapana uwezekano wako kuendelea kuishi duniani. Hata hivyo, watu hawawezi kumwacha Mungu; huu ndio umuhimu wa ushindi wa Mungu kwa watu, na huu ni utukufu wa Mungu. Kile ambacho umerithi wakati huu, kimepiku walichorithi mitume na manabii na ni kikuu zaidi kuliko alichopokea Musa na Petro. Baraka haziwezi zikapokewa kwa siku moja au mbili; sharti zipatikane kwa kujitolea kwingi. Yaani, lazima uwe na upendo uliosafishwa, imani kuu, na ukweli mwingi ambao Mungu Anakuagiza uufikie; zaidi ya hayo, sharti uelekeze uso wako kwa haki wala usikubali kushindwa, na lazima uwe na upendo usiofikia kikomo kwa ajili ya Mungu. Azimio linahitajika kutoka kwako, na vilevile mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Upotovu wako lazima utibiwe, na lazima ukubali mipango ya Mungu pasipo kulalamika, na hata uwe mtiifu hadi kifo. Hicho ndicho unachopaswa kutimiza. Hili ndilo lengo la mwisho la kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu kwa watu wa kundi hili. Anapokukarimia mengi, anakutaka wewe badala yake na kukufanyia matakwa yanayokufaa. Kwa hiyo, kazi yote ya Mungu haipo bila sababu, na kutokana na hili inaonekana ni kwa nini Mungu kila mara hufanya kazi ya hali ya juu na yenye mahitaji makali. Ndiyo maana unafaa kujawa na imani katika Mungu. Kwa ufupi, kazi yote ya Mungu hufanywa kwa ajili yako, ili kwamba uweze kupokea urithi Wake. Hii sio kwa ajili ya utukufu wa Mungu bali ni kwa ajili ya wokovu wako na kufanya kundi hili la watu walioteswa na nchi najisi kuwa wakamilifu. Sharti uelewe mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo Nawahimiza wale wote wasiojua, wasio na hisia na ufahamu: Usimjaribu Mungu wala kumpinga tena. Mungu Ameshavumilia mateso yote ambayo mwanadamu hajaweza kupitia, na hapo awali Ameteseka na kudhihakiwa kwa niaba ya mwanadamu. Je, nini kingine ambacho huwezi kukiachilia? Je, ni nini muhimu zaidi kuliko mapenzi ya Mungu? Ni nini zaidi kuliko upendo wa Mungu? Ni kazi ambayo ina ugumu mara mbili zaidi kwa Mungu kufanya katika nchi najisi. Ikiwa mtu atatenda dhambi kimakusudi na akifahamu, kazi ya Mungu itaendelezwa kwa muda mrefu zaidi. Katika tukio lolote, hili silo pendeleo la yeyote wala si la maana kwa yeyote. Mungu Hafungwi na wakati; kazi Yake na utukufu Wake huchukua mstari wa mbele. Kwa hiyo, hata ikichukua muda mrefu, Hataacha kutoa dhabihu yoyote ikiwa ni kazi Yake. Hii ndiyo silika ya Mungu: Hatapumzika hadi pale kazi Yake itakapokamilika. Ni pale tu ambapo wakati unapowadia na anapokea sehemu ya pili ya utukufu wake ndipo kazi Yake itakapokwisha. Mungu Asipokamilisha sehemu ya pili ya utukufu wake ulimwenguni, Siku Yake haitawadia, mkono wake hauwezi kuwaachilia wateule wake, utukufu wake hautashuka juu ya Israeli na mpango wake kamwe hauwezi kukamilishwa. Mnapaswa kuona mapenzi ya Mungu na kuona kwamba kazi ya Mungu si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Kwa sababu kazi ya leo ni kubadilisha wale waliopotoshwa, wale waliokufa ganzi, na kutakasa walioumbwa kisha kushughulikiwa na Shetani, si kuumba Adamu na Hawa, ama hata kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake. Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake. Huu ndio undani wa hadithi ya hatua hii ya kazi ya Mungu. Lazima ufahamu wala usirahisishe mambo. Kazi ya Mungu ni tofauti na kazi nyingine. Uzuri wake hauwezi kutambuliwa na akili za mwanadamu wala hekima Yake kupatikana vile. Wakati wa hatua hii ya kazi Yake, Mungu Haumbi kila kitu wala kuharibu kila kitu. Bali, Anabadilisha viumbe vyote na kutakasa vyote vilivyonajisiwa na Shetani. Kwa hiyo, Mungu Ataanzisha kazi kuu, na huu ndio umuhimu wa kazi ya Mungu. Baada ya kusoma maandishi haya, je, unaamini kuwa kazi ya Mungu ni rahisi vile?