Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumkamilisha binadamu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia katika neno, binadamu anajua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha binadamu, na kile ambacho binadamu anastahili kuingia ndani yake. Kupitia katika neno, kazi yote ambayo Mungu angependa kufanya katika Enzi ya Neno inatimizwa. Kupitia katika neno, binadamu anafichuliwa, anaondolewa, na kujaribiwa. Binadamu ameliona neno, amelisikia neno, na akapata habari ya uwepo wa neno. Kutokana na haya, binadamu anaamini katika uwepo wa Mungu; binadamu anaamini katika uwezo na hekima za Mungu, pamoja na moyo wa upendo wa Mungu kwa binadamu na tamanio Lake la kumwokoa binadamu. Ingawa neno “neno” ni rahisi na la kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu mwenye mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Kuanzia wakati huu kuendelea, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, wakichungwa na kuruzukiwa na neno. Binadamu wote wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata kuna binadamu zaidi wanaoishi chini ya hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kwa minajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa minajili ya kubadilisha sura asilia ya ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, na pia hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa. Katika Enzi nzima ya Ufalme, Mungu hutumia neno kufanya kazi Yake na kutimiza matokeo ya kazi Yake; Hafanyi maajabu au kutenda miujiza; Anafanya tu kazi Yake kupitia kwa neno. Kwa sababu ya neno, binadamu anastawishwa na kuruzukiwa; kwa sababu ya neno, binadamu hupokea maarifa na kupata uzoefu wa kweli. Binadamu katika Enzi ya Neno amepokea kwa kweli baraka za kipekee. Binadamu huwa hapati maumivu ya mwili na hufurahia tu ruzuku nyingi ya neno la Mungu; hawahitaji tena kutafuta au kushika safari, na kwa utulivu huona kuonekana kwa Mungu, wanamsikia Yeye akiongea binafsi, wanapokea ujazo Wake, na kumwona Yeye binafsi akifanya kazi Yake. Haya ndiyo mambo ambayo binadamu katika enzi zilizopita hawakuweza kufurahia, na hizi ndizo baraka ambazo wasingewahi kupokea.
Mungu anadhamiria kumfanya binadamu kuwa kamili. Haijalishi ni mtazamo gani anaoongelea Yeye, yote ni kwa minajili ya kuwakamilisha watu hawa. Maneno yaliyotamkwa kutoka kwenye mtazamo wa Roho ni magumu kwa binadamu kuelewa, na binadamu hawezi kupata njia ya kutenda kwake, kwani binadamu ana uwezo finyu wa kupokea. Kazi ya Mungu hutimiza athari tofauti, na katika kuchukua kila hatua ya kazi Yeye ana kusudio Lake. Aidha, ni jambo la lazima kwamba Aongee kutoka mitazamo tofauti kwa kuwa ni kwa kufanya hivyo tu ndiyo Anaweza kumkamilisha binadamu. Kama Angetoa sauti Yake kutoka kwenye mtazamo wa Roho pekee, hakungekuwa na njia ya kukamilisha hatua hii ya kazi ya Mungu. Kutokana na toni wa sauti Yake, unaweza kuona Anadhamiria kufanya kundi hili la watu kamilifu. Kwa kila mmoja wa wale ambao wangependakukamilishwa na Mungu, ni hatua gani ya kwanza ambayo lazima uchukue? Lazima kwanza ujue kazi ya Mungu. Sasa mbinu mpya zimeletwa katika kazi ya Mungu, na enzi imebadilika, jinsi ambavyo Mungu hufanya kazi pia imebadilika, na njia ambayo Mungu huongea ni tofauti pia. Sasa, si mbinu tu za kazi Yake zilizobadilika, lakini pia enzi yenyewe. Sasa ni Enzi ya Ufalme, kionjo cha Enzi ya Ufalme wa Milenia—ambayo pia ni Enzi ya Neno—yaani, enzi ambamo Mungu hutumia njia nyingi za kuongea ili kumfanya binadamu kuwa kamili, na Huongea kutoka kwa mitazamo tofauti ili kumruzuku binadamu. Punde tu nyakati zinapopita hadi katika Enzi ya Ufalme wa Milenia, Mungu ataanza kutumia neno ili kumkamilisha binadamu, kumwezesha binadamu kuingia katika uhalisi wa maisha na kumwongoza binadamu hadi kwenye njia sahihi. Binadamu amepitia hatua nyingi sana za kazi Yake na ameona kwamba kazi ya Mungu haibakii vilevile. Badala yake, inabadilika na kuwa yenye kina bila kukoma. Baada ya muda mrefu sana wa uzoefu, kazi imegeuka kwa kurudia na kubadilika tena na tena, lakini haijalishi inabadilika kwa kiasi gani, kamwe haitoki kwa lengo la Mungu la kumfinyanga binadamu. Hata kupitia mabadiliko elfu kumi, kamwe haipotei kutoka kwa kusudio la sili, wala haiondoki kamwe kutoka kwenye ukweli au uzima. Mabadiliko kwenye mbinu ambazo kazi inafanywa yanahusisha mabadiliko tu katika mpangilio wa kazi na mtazamo wa kuongea, na wala si badiliko kwenye lengo kuu la kazi Yake. Mabadiliko katika toni ya sauti na mbinu za kufanya kazi yanafanywa ili kutimiza athari fulani. Mabadiliko katika toni ya sauti hayamaanishi mabadiliko katika kusudio au kanuni ya kazi. Katika kumwamini Mungu, lengo kuu la binadami ni kutafuta uzima. Kama unasadiki katika Mungu lakini hutafuti uzima au ukweli au maarifa ya Mungu, basi hii sio imani katika Mungu! Kwamba unaendelea kutafuta kuingia katika ufalme kuwa mfalme—hili ni jambo la uhalisi? Kufanikisha upendo wa kweli kweli kwa Mungu kupitia kutafuta uzima—huu pekee ndio uhalisi; ufuatiliaji nautendaji wa ukweli—hivi vyote ni uhalisi. Pitia maneno ya Mungu wakati ukisoma maneno Yake; kwa njia hii utaweza kung’amua maarifa ya Mungu kupitia kwa uzoefu halisi. Hii ni aina ya ufuatiliaji halisi.
Sasa ni Enzi ya Ufalme. Iwapo maisha yako yameingia katika enzi hii mpya inategemea na kama umeingia kwenye uhalisi wa maneno ya Mungu na kama maneno Yake yamekuwa imani yako, upendo wako na uhalisi wa maisha yako. Neno la Mungu linajuzwa kwa wote, ili hatimaye, binadamu wote waweze kuishi katika ulimwengu wa neno na neno la Mungu litawapa nuru na kuangaza ndani ya kila mtu. Kama katika kipindi hiki cha muda, una haraka na uzembe katika kusoma neno la Mungu, na huna kivutio katika neno Lake, yaonyesha kwamba kuna jambo baya na hali yako. Kama huwezi kuingia katika Enzi ya Neno, basi Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yako; kama umeingia katika enzi hii, Atafanya kazi Yake. Ni nini unachoweza kufanya wakati Enzi hii ya Neno inaanza ili kupata kazi ya Roho Mtakatifu? Katika enzi hii, Mungu ataleta uhalisi huu miongoni mwenu ili kwamba kila binadamu aweze kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, aweze kutia ukweli katika matendo, na kumpenda Mungu kwa dhati; kwamba binadamu wote waweze kutumia neno la Mungu kama msingi na uhalisi wao na kuwa na mioyo ya kumcha Mungu; na kwamba, kupitia kwa kutenda neno la Mungu, binadamu basi ataweza kutawala pamoja na Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu atatimiza. Unaweza kuendelea na maisha bila ya kusoma neno la Mungu? Kuna wengi sasa wanaohisi kwamba hawawezi kukaa hata siku moja au mbili bila ya kusoma neno la Mungu. Lazima wasome neno Lake kila siku, na kama muda hauruhusu, kusikiliza neno Lake kunatosha. Hii ndiyo hisia ambayo Roho Mtakatifu anampa binadamu na hii ndiyo namna ambavyo Anaanza kumbadilisha binadamu. Yaani, Hutawala binadamu kupitia kwa maneno ili binadamu aweze kuingia katika uhalisi wa neno la Mungu. Iwapo, baada ya siku moja tu bila kula na kunywa neno la Mungu, unahisi giza na kiu na unaonakuwa halikubaliki, hili linaonyesha kwamba umeguswa na Roho Mtakatifu, na kwamba hajakupa kisogo. Basi wewe ndiye mmoja aliye katika mkondo huu. Hata hivyoiwapo baada ya siku moja au mbili bila kula na kunywa neno la Mungu huhisi chochote, na huna kiu, wala hujaguswa hata kidogo, hili linaonyesha kwamba Roho Mtakatifu amakupa kisogo. Hii inamaanisha, basi, kuwa hali iliyo ndani yako si sahihi; bado hujaingia katika Enzi ya Neno, na wewe ni mmoja aliyebaki nyuma. Mungu hutumia neno ili kumtawala binadamu; unahisi vyema ukila na kunywa neno la Mungu, na kama huhisi hivyo, hutakuwa na njia yoyote ya kufuata. Neno la Mungu linakuwa chakula cha binadamu na nguvu zinazomwendesha. Biblia inasema kwamba “Mwanadamu hataishi kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu”. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu ataikamilisha leo. Atafanikisha ukweli huu ndani yenu. Ikoje kwamba binadamu katika siku za kale angekaa siku nyingi bila ya kusoma neno la Mungu lakini angeendelea kula na kufanya kazi? Na kwa nini hali sivyo hivi sasa? Katika enzi hii, Mungu hutumia kimsingi neno ili kutawala yote. Kupitia kwa neno la Mungu, binadamu anahukumiwa na kukamilishwa, kisha hatimaye kupelekwa katika ufalme. Ni neno la Mungu tu linaloweza kuruzuku maisha ya binadamu, na ni neno la Mungu tu ndilo linaloweza kumpa binadamu nuru na njia ya kutenda, hasa katika Enzi ya Ufalme. Mradi tu kila siku unakula na kunywa neno Lake na huachi uhalisi wa neno la Mungu, Mungu ataweza kukukamilisha.
Mtu hawezi kuwa na haraka kutimiza ufanisi wakati anapotafuta uzima; ukuaji katika maisha haufanyiki tu kwa siku moja au mbili. Kazi ya Mungu ni kawaida na ya utendaji, na lazima ipitie mchakato unaohitajika. Ilimchukua Yesu mwenye mwili miaka thelathini na mitatu na nusu ili kukamilisha kazi Yake ya kusulubishwa: Hili linaweza kuwa kweli zaidi kiasi gani kuhusu kumtakasa mwanadamu na kubadilisha maisha yake! Kazi hii ina ugumu mkubwa sana. Si kazi rahisi pia kumuumba binadamu wa kawaida anayemdhihirisha Mungu. Hali hasa iko hivi kwa watu waliozaliwa katika taifa la joka kuu jekundu, ambao ni wenye ubora wa chini wa tabia na wanahitaji kipindi kirefu cha neno na kazi ya Mungu. Hivyo basi usiwe na haraka kuyaona matokeo. Lazima ushughulike katika kula na kunywa maneno ya Mungu, na kutia jitihada katika maneno ya Mungu. Baada ya kuyasoma maneno Yake, lazima uweze kuyatia katika matendo kwa uhalisi, na katika maneno ya Mungu, uweze kupata maarifa, maono, utambuzi, na hekima. Kupitia haya, utabadilika bila kutambua. Kama unaweza kuchukua kama kanuni zako kula na kunywa na neno la Mungu, kulisoma neno Lake, kulijua kwa undani, kulipitia, na kulitia katika matendo, basi utakua bila kutambua. Baadhi husema kwamba hawawezi kulitia neno la Mungu katika matendo hata baada ya kulisoma! Haraka yako ni ya nini? Unapofikia kimo fulani, utaweza kulitia katika matendo neno Lake. Je, mtoto wa umri wa miaka minne au mitano anaweza kusemaje kwamba hawezi kuwapa msaada au kuwaheshimu wazazi wake? Unafaa kujua sasa kimo chako ni kipi. Tia katika matendo kile unachoweza, na usiwe kwamba wewe ndiwe unayekatiza usimamizi wa Mungu. Kula na unywe tu maneno ya Mungu, na tukisonga mbele, chukulia suala hilo kama kanuni yako. Usiwe na wasiwasi kwa sasa kuhusu kama Mungu anaweza kukufanya kuwa kamili. Usiingilie jambo hilo kwa sasa. Wewe kula na kunywa tu na maneno ya Mungu punde unapokutana nayo, na unahakikishiwa kwamba Mungu ataweza kukufanya kuwa kamili. Hata hivyo, kuna kanuni ambayo kwayo lazima ukule na kunywa neno Lake. Usifanye hivyo bila kufikiria, lakini, kwa upande mmoja, tafuta maneno unayofaa kujua, yaani, yale yanayohusiana na maono, na kwa upande ule mwingine ttafuta kile unachopaswa kutia katika vitendo halisi, yaani, kile unachofaa kuingia kwacho. Kipengele kimoja ni kuhusu maarifa, na kingine kinahusiana na kuingia. Punde utakapoelewa vyote viwili, yaani, utakapoelewa kile unachofaa kujua na kutenda, basi utajua namna ya kula na kunywa neno la Mungu.
Kuanzia sasa kuendelea, kuzungumzia neno la Mungu ni kanuni ambayo kwayo unapaswa kuongea. Kwa kawaida, mnapokuja pamoja, mnafaa kuweza kuingia katika ushirika kuhusu neno la Mungu, kulichukua neno la Mungu kama maudhui ya mikutano yenu; mkizungumza kuhusu kile mnachojua kuhusu neno la Mungu, namna mnavyoitia katika vitendo neno Lake, na namna ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi. Unachohitajika tu kufanya ni kujihusisha katika ushirika kuhusu neno la Mungu, na Roho Mtakatifu atakupa nuru. Kufanya ulimwengu wa neno la Mungu uwepo, huku kunahitaji ushirikiano wa binadamu. Kama huingii ndani ya hili, Mungu hatakuwa na njia ya kufanya kazi Yake. Usiposema lolote na ukose kuzungumza kuhusu neno Lake, hakuna njia ya Mungu kukupa nuru. Kila unapopata nafasi, zungumzia neno la Mungu, na usizungumze tu bila mpango! Acha maisha yako yakajazwe na neno la Mungu—ni hapo tu ndipo utakuwa muumini mwenye kumcha Mungu. Hata kama ushirika wako ni wa juu juu, hiyo ni sawa. Bila ya hali hiyo ya juujuu, hakuwezi kuwa na kina. Kunao mchakato ambao lazima upitiwe. Kupitia kwa mafunzo yako, unatambua kupewa nuru na Roho Mtakatifu, na namna unavyoweza kula na kunywa neno la Mungu kwa njia iliyo na matokeo bora. Baada ya kipindi cha uchunguzi, utaingia katika uhalisi wa neno la Mungu. Ni kama tu utakuwa na uamuzi wa kushirikiana ndipo utakapopokea kazi ya Roho Mtakatifu.
Kuna vipengele viwili katika kanuni za kula na kunywa neno la Mungu: Kimoja kinahusiana na maarifa, na kingine kinahusiana na kuingia. Ni maneno yapi unayofaa kujua? Unafaa kujua maneno yanayohusiana na maono (kama vile, yale yanayohusiana na enzi ambayo kazi ya Mungu imekwisha ingia, ni nini ambacho Mungu Angependa kutimiza sasa, kupata mwili ni nini, na kadhalika. Haya yote yana uhusiano na maono). Ni njia gani ambamo binadamu anafaa kuingia? Hii inarejelea maneno ya Mungu ambayo binadamu anafaa kutenda na kuingia ndani. Hivi ndivyo vipengele viwili vya kula na kunywa neno la Mungu. Kuanzia sasa, kula na unywe neno la Mungu kwa njia hii. Kama unao uelewa kamili wa maneno yanayohusu maono, basi hakuna haja ya kuendelea kusoma kila wakati. Kilicho na umuhimu mkubwa ni kula na kunywa maneno zaidi yanayohusu kuingia, kama vile kuelekeza moyo wako kwa Mungu, namna ya kutuliza moyo wako mbele ya Mungu, na namna ya kuunyima mwili. Haya ndiyo mambo unayofaa kutenda. Bila ya kujua namna ya kula na kunywa neno la Mungu, ushirika wa kweli hauwezekani. Punde utakapojua namna ya kula na kunywa neno Lake, na umeng'amua kilicho muhimu, ushirika utakuwa huru. Masuala yawayo yote yaulizwapo, unaweza kushiriki kuyahusu na kuelewa uhalisi. Kushiriki kuhusu neno la Mungu bila ya kuwa na uhalisi kunamaanisha huwezi kuelewa kilicho muhimu, na hii inamaanisha kwamba hujui kula na kunywa neno Lake. Wengine huhisi uchovu wakati wanaposoma neno la Mungu, ambayo si hali ya kawaida. Kilicho kawaida ni kutochoka kusoma neno la Mungu, siku zote kuwa na kiu ya neno la Mungu, na kila wakati kuliona neno la Mungu likiwa zuri. Hivi ndivyo mtu ambaye kweli ameingia anakula na kunywa neno la Mungu. Unapohisi kwamba neno la Mungu ni la utendaji kweli na ndilo hasa lile binadamu anafaa kuingia ndani; unapohisi kwamba neno Lake ni lenye manufaa na faida kubwa kwa binadamu, na kwamba ndilo ruzuku ya uzima wa binadamu—ni Roho Mtakatifu anayekupa hisia hii, na ni Roho Mtakatifu anayekugusa. Hii inathibitisha kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako na kwamba Mungu hajakuacha. Watu wengine, wanapoona kwamba Mungu siku zote anaongea, huwa na uchovu wa maneno Yake na kufikiria kwamba hakuna tofauti yoyote kama watasoma maneno Yake au hawatasoma. Hiyo si hali ya kawaida. Hawana mioyo iliyo na kiu ya kuingia katika uhalisi, na binadamu kama hao hawana kiu ya kukamilishwa wala kutilia umuhimu kwa kukamilishwa. Kila unapopata huna kiu ya neno la Mungu, yaonyesha kwamba hali yako si ya kawaida. Zamani, kama Mungu alikuacha iliamuliwa na kama wewe ulikuwa na amani ndani yako na ulipitia furaha. Sasa kilicho muhimu ni kama una kiu ya neno la Mungu, kama neno Lake ndilo uhalisi wako, kama wewe ni mwaminifu, na kama unaweza kufanya kile unachoweza kwa ajili ya Mungu. Kwa maneno mengine, binadamu huhukumiwa na uhalisi wa neno la Mungu. Mungu huelekeza neno Lake kwa watu wote. Kama uko radhi kulisoma, Atakupa nuru, lakini kama huko radhi, Hatakupa nuru. Mungu huwapa nuru wale walio na njaa na kiu ya haki, na wale wanaomtafuta Yeye. Baadhi husema kwamba Mungu hakuwapa nuru hata baada ya wao kusoma neno Lake. Lakini uliyasoma maneno haya kwa njia ipi? Ukisoma neno Lake kama kutazama maua mgongoni mwa farasi na hukutilia umuhimu katika uhalisi, Mungu angekupa nuru vipi? Ni vipi ambavyo mtu asiyethamini neno la Mungu anaweza kukamilishwa na Yeye? Kama huthamini neno la Mungu, basi hutakuwa na ukweli wala uhalisi. Kama unathamini neno Lake, basi utaweza kutia ukweli katika matendo; ni hapo tu ndipo utakapokuwa na uhalisi. Hivyo basi lazima ule na kunywa neno la Mungu licha ya hali yoyote ile, kama una shughuli au la, kama hali ni mbaya au la, na kama unajaribiwa au la. Kwa jumla, neno la Mungu ndilo msingi wa uwepo wa mwanadamu. Hakuna yule anayeweza kuliacha neno Lake na lakini lazima ale neno Lake kama anavyokula milo mitatu ya siku. Linaweza kuwa suala rahisi hivyo kukamilishwa na kupatwa na Mungu? Iwapo unaelewa au huelewi kwa sasa au kama una utambuzi wa kazi ya Mungu, lazima ule na kunywaneno la Mungu zaidi iwezekanavyo. Huku ndiko kuingia katika njia makini ya utendaji. Baada ya kulisoma neno la Mungu, harakisha kukitia katika matendo kile unachoweza kuingia ndani, na utenge kwa wakati huu kile huwezi kuingia ndani. Huenda kukawa na mambo mengi katika neno la Mungu ambayo huwezi kuyaelewa mwanzoni, lakini baada ya miezi miwili au mitatu, pengine hata mwaka mmoja, utaweza. Hili linawezekanaje? Hii ni kwa sababu Mungu hawezi kumfanya binadamu kuwa kamili kwa siku moja au mbili. Wakati mwingi, unapolisoma neno Lake, pengine huwezi kuelewa kwa wakati huo. Wakati huo, yaweza kuonekana kama maandishi tu, na ni baada ya kupitia tu kipindi cha uzoefu ndipo unapoweza kuelewa. Mungu ameongea mengi, hivyo basi unafaa kufanya yale mengi zaidi unayoweza ili kula na kunywa neno Lake. Bila ya kutambua, utakuja kuelewa, naye Roho Mtakatifu atakupa nuru bila ya wewe kujua. Wakati Roho Mtakatifu humpa nuru binadamu, mara nyingi huwa bila ya ufahamu wa binadamu. Hukupa nuru na kukuongoza unapokuwa na kiu na unapotafuta. Kanuni ambayo kwayo Roho Mtakatifu hufanya kazi imekita mizizi katika neno la Mungu ambalo unakula na kunywa. Wale wote ambao hawatilii umuhimu katika neno la Mungu na siku zote wana mwelekeo mwingine katika neno Lake, mwelekeo ule wa uzembe na kusadiki kwamba hakuna tofauti yoyote kama watalisoma neno Lake, ndio wale wasiokuwa na uhalisi. Si kazi ya Roho Mtakatifu wala nuru kutoka Kwake vinavyoweza kuonekana ndani ya mtu kama huyo. Watu kama hao wanasairi tu, na ni wanafiki wasiokuwa na kufuzu kwa ukweli, kama Bw. Nanguo wa hadithi ya mafumbo.[a]
Bila ya neno la Mungu kama uhalisi wako, huna kimo halisi. Wakati ukiwadia wa kujaribiwa, bila shaka utaanguka, na hapo ndipo kimo chako cha kweli kitakapoonyeshwa. Lakini kwa wakati wa kujaribiwa, wale wanaotafuta mara kwa mara kuingia katika uhalisi wataelewa kusudio la kazi ya Mungu. Mtu anayemiliki dhamiri na ana kiu ya Mungu anafaa kuchukua hatua ya kimatendo ili kumlipia Mungu kwa upendo Wake. Wale wasiokuwa na uhalisi hawawezi kusimama imara wanapokumbwa hata na masuala madogo. Kunayo tofauti kati ya wale walio na kimo halisi na wale wasiokuwa nacho. Ni kwa nini, hata ingawa baadhi yao wanaweza kuwa sawa katika kula na kunywa neno la Mungu, lakini baadhi yao wanaweza kusimama imara katika jaribio huku nao wengine wanalitoroka? Utofauti ulio wazi ni kwamba wanakikosa kimo halisi; hawana neno la Mungu kama uhalisi wao, na neno Lake halijakita mizizi ndani yao. Punde tu wanapojaribiwa, hakuna njia kwao. Kwa nini, hivyo basi, wengine hawawezi kusimama imara kwa hili? Hii ni kwa sababu wanayo maono makubwa, au neno la Mungu limekuwa uzoefu wao ndani yao, na kile ambacho wameona katika uhalisi kimekuwa msingi wa uwepo wao. Kwa njia hii, wanaweza kusimama imara katika majaribio. Hiki ni kimo halisi, na haya ni maisha pia. Baadhi wanaweza pia kusoma neno la Mungu lakini hawawezi katu kulitia katika matendo au wao hawana ari kulihusu. Wale wasio na ari hawaweki umuhimu wowote katika kutenda. Wale wasiokuwa na neno la Mungu kama uhalisi wao ndio wale wasiokuwa na kimo halisi.
Watu kama hao hawawezi kusimama imara katika majaribio. Wakati Mungu anapoongea, unafaa kupokea mara moja maneno Yake na kuyala na kuyanywa. Haijalishi ni kiwango kipi unachoelewa, mtazamo ambao lazima ushikilie imara ni kulila na kulinywa, kulijua, na kulitenda neno Lake. Hili ni jambo unalofaa kufanya. Usiwe na wasiwasi kuhusu kimo chako kinaweza kua kikubwa vipi; zingatia tu katika kula na kunywa neno Lake. Hivi ndivyo binadamu anavyofaa kushirikiana. Maisha yako ya kiroho kimsingi ni kujaribu kuingia katika uhalisi pale ambapo unakula na kunywa maneno ya Mungu na kuyatia katika matendo. Hufai kuzingatia jambo lolote jingine. Viongozi wa kanisa wanafaa kuwaongoza ndugu wote katika namna ya kula la kunywa neno la Mungu. Huu ndio wajibu wa viongozi wote wa kanisa. Wawe vijana au wazee, wote wanafaa kuchukulia kula na kunywa maneno ya Mungu kwa umuhimu na kuyatia maneno Yake katika mioyo yao. Kuingia katika uhalisi huu kunamaanisha kuingia katika Enzi ya Ufalme. Siku hizi, wengi huhisi kwamba hawawezi kuishi bila kula na kunywa neno la Mungu, na haijalishi ni wakati gani, wanahisi kwamba neno Lake ni jipya. Hii ina maana kwamba binadamu ameanza kuendenda katika njia sahihi. Mungu hutumia neno Lake katika kufanya kazi na kumruzuku binadamu. Wakati kila mtu anatamani na kuwa na kiu ya neno la Mungu, binadamu wataingia katika ulimwengu wa neno Lake.
Mungu ameongea pakubwa. Unayo maarifa kiasi kipi kuyahusu? Umeingia hadi kiwango kipi? Kama kiongozi wa kanisa bado hajawaongoza ndugu katika uhalisi wa neno la Mungu, basi atakuwa amekuwa mzembe katika wajibu wake na kushindwa kukamilisha majukumu yake! Haijalishi kina cha kula na kunywa kwako kwa neno, au ni kiasi kipi unachoweza kupokea, lazima ujue namna ya kula na kunywa neno Lake; lazima uchukulie neno Lake kwa umuhimu na uelewe umuhimu na haja ya kushiriki kama huko. Mungu ameongea sana, kama hutakula na kunywa neno Lake, au kutolitafuta ama kulitia neno Lake katika matendo, huku hakuwezi kuchukuliwa kama kumwamini Mungu. Kwa sababu unamsadiki Mungu, lazima ule na kunywa neno Lake, upitie neno Lake, na uishi kwa kudhihirisha neno Lake. Huku tu ndiko kunaweza kuitwa imani katika Mungu! Kama unasema unamsadiki Mungu na kinywa chako ilhali huwezi kutia maneno Yake yoyote katika vitendo, au kutoa uhalisi wowote, huku hakuitwi kumwamini Mungu. Badala yake, ni “kuutafuta mkate ili kuikabili njaa.” Kuzungumzia tu ushuhuda mdogo mdogo, masuala ya upuuzi na masuala ya juujuu, bila hata kuwa na kiwango kidogo cha uhalisi: haya hayamaanishi imani katika Mungu, na hasa bado hujang'amua njia sahihi ya kumwamini Mungu. Kwa nini lazima ule na kunywa zaidi ya maneno ya Mungu? Usipokula na kunywa maneno Yake bali utafute tu kupaa mbinguni, je, huko ni kumwamini Mungu? Ni nini hatua ya kwanza kwake yule anayesadiki neno Lake Mungu? Ni katika njia gani ndiyo Mungu humkamilisha binadamu? Unaweza kufanywa kuwa mtimilifu bila ya kula na kunywa neno la Mungu? Unaweza kuchukuliwa kuwa mtu wa ufalme bila ya neno la Mungu kuwa uhalisi wako? Imani katika Mungu inamaanisha nini hasa? Wanaomwamini Mungu wanafaa kumiliki tabia nzuri kwa nje, angalau, na kilicho na umuhimu mkubwa zaidi ni kuwa na neno la Mungu. Haijalishi ni nini, huwezi kuligeuka neno la Mungu. Kumjua Mungu na kutimiza mapenzi Yake vyote vinafanikishwa kupitia kwa neno Lake. Kila taifa, dhehebu, dini, na sekta zitashindwa kupitia kwa neno katika siku za usoni. Mungu ataongea moja kwa moja, na watu wote watashikilia neno la Mungu katika mikono yao; kupitia haya wanadamu watakamilishwa. Ndani na nje, neno la Mungu limeenea kotekote: Binadamu huongelea neno la Mungu kwa vinywa vyao, kutenda kulingana na neno la Mungu, na kulishika neno la Mungu ndani mwao kwa ndani na hata kwa nje, wanarowekwa katika neno la Mungu. Hivi ndivyo binadamu watakamilishwa. Wale wanaotimiza mapenzi ya Mungu na wanaweza kumshuhudia Yeye ndio wale walio na neno la Mungu kama uhalisi.
Kuingia katika Enzi ya Neno, yaani, Enzi ya Ufalme wa Milenia, ndiyo kazi ambayo inakamilishwa sasa. Kuanzia sasa, fanya mazoezi ya kushiriki kuhusu neno la Mungu. Ni kupitia tu kula na kunywa neno Lake na kulipitia ndipo utakapoweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu kihalisi. Lazima utoe uzoefu fulani kwa vitendo ili kuwashawishi wengine. Kama huwezi kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa neno la Mungu, hakuna atakayeshawishika! Wale wote wanaotumiwa na Mungu ni watu wenye uhalisi wa kupitia neno la Mungu. Kama huwezitoa uhalisi huu, hii ingeonyesha kwamba Roho Mtakatifu bado hajafanya kazi ndani yako na ungali bado hujakamilishwa. Huu ndio umuhimu wa neno la Mungu. Je, unao moyo ulio na kiu ya neno la Mungu? Wale walio na kiu ya neno la Mungu huwa na kiu ya ukweli, na binadamu kama hao tu ndio wanaobarikiwa na Mungu. Katika siku za usoni, kunayo maneno mengi zaidi ambayo Mungu atanena kwa dini zote na madhehebu yote. Kwanza anaongea na kutoa sauti Yake miongoni mwenu na kuwafanya kuwa kamili kabla ya kusonga mbele na kuongea na kutoa sauti Yake kwa Mataifa na kuwashinda. Kupitia kwa neno, wote wataweza kushawishika kwa uaminifu na kwa kikamilifu. Kupitia neno la Mungu na ufunuo Wake, tabia iliyopotoka ya binadamu imepungua, wote wanao wajihi wa binadamu, na tabia asi ya binadamu imelegea vilevile. Neno linafanya kazi kwa binadamu kupitia kwa mamlaka na linamshinda binadamu ndani ya nuru ya Mungu. Kazi ambayo Mungu atafanya katika enzi ya sasa, pamoja na jambo kuu katika kazi Yake vyote vinaweza kupatikana ndani ya neno Lake. Kama hulisomi neno Lake, hutaelewa chochote. Kupitia kula na kunywa kwako mwenyewe kwa neno Lake, na kupitia kuwa na ushirika na ndugu, na kile utakachopitia kwa uhalisi, maarifa yako ya neno la Mungu yatakuwa pana. Na hapo tu ndipo utakapoweza kuishi kwa kulidhihirisha kwa kweli katika uhalisi.