16 Jul
Neno la Mwenyezi Mungu | Njia … (7)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu | Njia … (7)

Sote tunaweza kuona katika uzoefu wetu wa utendaji kwamba kuna nyakati nyingi ambazo Mungu binafsi ametufungulia njia ili tuwe tunakanyaga njia iliyo imara zaidi, ya kweli zaidi. Hii ni kwa sababu hii ndiyo njia ambayo Mungu alitufungulia tangu mwanzo wa wakati na imepitishwa kwa kizazi chetu baada ya makumi ya maelfu ya miaka. Kwa hiyo tunarithi watangulizi wetu ambao hawakutembea njia hii mpaka mwisho wake; sisi ndio tumechaguliwa na Mungu kutembea sehemu ya mwisho ya njia hii. Hivyo, imetayarishiwa hasa sisi, na haijalishi ikiwa tutapokea baraka au kupata taabu, hakuna mwingine anayeweza kutembea njia hii. Naongeza utambuzi Wangu kwa hili: Usifanye mipango ya kutorokea mahali pengine au kupata njia nyingine, ukitamani hadhi, au kuanzisha ufalme wako mwenyewe; haya yote ni uongo. Ikiwa una upendeleo fulani kwa maneno haya, Nakushauri usichanganyikiwe. Ni bora zaidi ikiwa utayafikiria sana, usijaribu kuwa mwerevu sana au ukose kubainisha mema na mabaya. Mpango wa Mungu unapotimizwa, utajuta kwa hilo. Hiyo ni kusema, ufalme wa Mungu ukija Atavunjavunja mataifa ya dunia, na wakati huo utaona kwamba mipango yako wewe pia imefutiliwa mbali na wale ambao wameadibiwa ni wale ambao wamevunjwa. Wakati huo Mungu atafichua kabisa tabia Yake. Nafikiria kwamba Napaswa kukwambia juu ya hili kwa vile Ninafahamu vizuri suala hili ili katika siku za usoni usije ukalalamika kunihusu Mimi. Kwamba tumeweza kutembea njia hii mpaka leo iliamriwa na Mungu, kwa hiyo usifikirie kwamba wewe ni kitu cha kipekee au kwamba huna bahati—mtu yeyote asifanye madai kuhusu kazi ya sasa ya Mungu usije ukavunjwavunjwa kwa vipande. Nuru imenijia kupitia kazi ya Mungu, na lolote litokealo, Mungu atafanya kuwa kamili kundi hili la watu na kazi Yake haiwezi kubadilishwa—Atawafikisha watu hawa mwisho wa njia na kukamilisha kazi Yake duniani. Hiki ni kitu ambacho sote tunapaswa kuelewa. Wengi wa watu huwa “wanatazama mbele” siku zote na kutoridhika; wote wanakosa ufahamu wa kusudi la dukuduku la sasa la Mungu, kwa hiyo wao huwa na mawazo ya kutoroka. Wao kila mara hutaka kwenda jangwani kuzurura kama farasi wa kukurupuka ambaye ametupilia mbali vizuizi vyake, lakini ni adimu kwamba kuna watu wanaotaka kuishi katika nchi nzuri ya Kanaani kutafuta njia ya maisha ya binadamu. Wakati wameingia katika nchi inayotiririka maziwa na asali, hawatafikiria tu juu ya kuifurahia? Kusema kweli, nje ya nchi nzuri ya Kanaani kila mahali ni jangwa. Hata watu wakishaingia mahali pa pumziko hawawezi kutetea kazi yao; hao si makahaba tu? Ikiwa umepoteza nafasi ya Mungu kukufanya mkamilifu katika mazingira hayo, kitakuwa kitu ambacho utatubu kwa siku zako zote zilizobaki; utahisi kujutia kupita kiasi. Utaishia kuwa kama Musa aliyetazama tu nchi ya Kanaani lakini hakuweza kuifurahia, akikaza sana ngumi tupu na kufa akiwa amejaa majuto—hufikirii kwamba hilo ni jambo la aibu? Hufikirii kwamba kudhihakiwa na wengine ni jambo la kuaibisha? Uko radhi kufedheheshwa na wengine? Je, huna moyo wa kujitahidi kujitendea mema? Hutaki kuwa mtu wa heshima na mwenye siha ambaye amefanywa kamili na Mungu? Je, wewe kweli ni mtu anayekosa azimio lolote? Huko radhi kufuata njia zingine lakini huko radhi pia kufuata njia ambayo Mungu amekuamria? Unathubutu kwenda dhidi ya mapenzi ya Mbinguni? Haijalishi ujuzi wako ni mkuu vipi, unaweza kweli kukosea Mbinguni? Naamini kwamba ni bora kwetu kujijua vizuri—sehemu moja ndogo tu ya neno la Mungu inaweza kubadilisha mbingu na nchi, kwa hiyo mtu mdogo aliyekonda ni nini machoni pa Mungu?

Nikiangalia kutoka kwa uzoefu Wangu mwenyewe, kadri unavyokabiliana na Mungu, ndivyo Mungu atakuonyesha tabia Yake ya uadhama zaidi, na ndivyo kuadibu “Anakokugawia” kutakosa huruma zaidi. Kadri unavyomtii Mungu, ndivyo atakavyokupenda na kukuhifadhi zaidi. Tabia ya Mungu ni sawasawa na chombo cha mateso Ukitii utakuwa salama salimini. Usipotii lakini kila mara unataka kuwa maarufu na kufanya hila, tabia Yake itabadilika ghafla Kama tu jua siku ya mawingu, Atajificha kutoka kwako na kukuonyesha ghadhabu. Pia ni kama hali ya hewa katika mwezi wa Juni, ikiwa na anga tulivu kwa maili nyingi na mawimbi ya samawati yakiwa na viwimbi juu ya maji, mpaka maji ghafla yanapata nguvu na mawimbi ya kuogofya yanafurika. Kutokana na tabia hii ya Mungu, unathubutu kutenda ovyo ovyo na kwa hiari? Ndugu wengi wameona katika uzoefu wao kwamba Roho Mtakatifu anapofanya kazi katika siku wanajawa ujasiri, lakini kisha Roho wa Mungu huwatelekeza ghafla bila wao kujua lini, Akiwaacha wasiotulia na wakikosa usingizi usiku, wakitafutatafuta upande ambao Roho Mtakatifu alipotelea. Lakini lolote litokealo hawawezi kutambua mahali Roho Mtakatifu alienda; na Yeye hujitokeza kwao tena bila wao kujua lini, na kama wakati ambao Petro ghafla alimwona Bwana wake Yesu tena, alijaa furaha na akaonekana kupiga yowe kwa furaha ya kuchanganyikiwa. Unaweza kweli kusahau kupitia tukio hili baada ya mara nyingi hivyo? Bwana Yesu Kristo, aliyepata mwili, Alipigwa misumari msalabani, na kisha akafufuliwa na kupaa mbinguni, huwa kila mara Amefichika kwako kwa kipindi fulani, kisha Hujitokeza kwako kwa kipindi fulani. Yeye hujifichua kwako kwa sababu ya uadilifu wako, na Yeye hukasirika na kutoka kwako kwa sababu ya dhambi zako, kwa hiyo mbona usimsihi zaidi? Hukujua kwamba tangu Pentekoste, Bwana Yesu Kristo ana agizo jingine duniani? Yote unayojua ni kuwa ni kweli kwamba Bwana Yesu Kristo alipata mwili, akaja duniani, na akapigwa misumari msalabani, lakini hujawahi kujua kwamba Yesu uliyemwamini awali aliaminia kazi hii kwa mtu mwingine zamani sana. Kazi Yake ilikamilishwa zamani sana, kwa hiyo Roho wa Bwana Yesu Kristo amekuja duniani tena katika umbo la mwili kufanya sehemu nyingine ya kazi Yake. Ningependa kuingiza jambo fulani hapa—licha ya kuwa mko sasa katika mkondo huu, Nathubutu kusema kwamba wachache wa watu miongoni mwenu mnaamini kwamba mtu huyu Ndiye mliyepewa na Bwana Yesu Kristo. Yote mnayojua ni kumfurahia lakini hamkubali kwamba Roho wa Mungu amekuja tena duniani, na hamkubali kwamba Mungu wa leo ni Yesu Kristo wa kutoka maelfu ya miaka ya zamani. Hii ndiyo maana Nasema kwamba nyote mnatembea na macho yenu yakiwa yamefumbwa. Mnakubali tu popote mnapojikuta—hamko makini kulihusu kamwe. Ni kwa sababu hii ndiyo mnaamini katika Yesu kwa neno, lakini mnathubutu kupinga dhahiri Yule ambaye anashuhudiwa na Mungu leo. Wewe si mpumbavu? Mungu wa leo hajali kuhusu makosa yako; Yeye hakushutumu. Unasema kwamba unaamini katika Yesu, kwa hiyo Bwana wako Yesu Kristo angeweza kukusamehe? Unadhani kwamba Mungu ni mahali pa wewe kudhihirisha hisia au kudanganya? Bwana wako Yesu Kristo atakapojifichua tena, Ataamua ikiwa wewe ni mwadilifu au ikiwa wewe ni mwovu kulingana na vile unavyotenda sasa. Watu wengi huishia kuwa na fikira kuhusu kile Ninachoita “Ndugu Zangu”; wanaamini kwamba njia ya Mungu ya kufanya kazi itabadilika. Je, watu hawa hawakaribishi tu kifo? Mungu anaweza kumshuhudia Shetani kama Mungu Mwenyewe? Je, humshutumu tu Mungu? Unadhani kwamba mtu yeyote anaweza tu kutenda kwa kawaida kama Mungu Mwenyewe? Ikiwa kweli ungekuwa na ufahamu , basi usingekuza fikira. Kuna kifungu kifuatacho katika Biblia: “Vitu vyote ni kwa ajili Yake, na vitu vyote vinatoka Kwake. Atawaleta wana wengi kwa utukufu na Yeye ni Nahodha wetu. ... Kwa hivyo, Haoni haya kutuita ndugu. Unaweza kuyakariri maneno kwa urahisi moyoni lakini huelewi maana yake hasa; je, huamini katika Mungu na macho yako yakiwa yamefumbwa?

Nasadiki kwamba kizazi chetu kimebarikiwa kwa kuweza kufuata njia ambayo haijakamilishwa na watu wa vizazi vya awali, na kuweza kuendeleza kuonekana tena kwa Mungu baada ya miaka elfu kadhaa—Mungu aliye hapa miongoni mwetu, na pia anayepatikana katika vitu vyote. Usingewahi kufikiria kwamba ungeweza kutembea kwenye njia hii: Unaweza kufanya hivyo? Njia hii inaongozwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu, inaongozwa na Roho aliyezidishwa mara saba wa Bwana Yesu Kristo, na ndiyo njia ambayo imefunguliwa kwako wewe na Mungu wa leo. Hata katika ndoto zako za kipekee usingewahi kufikiria kwamba Yesu wa miaka elfu kadhaa iliyopita angeonekana tena mbele yako. Je, huhisi kuwa mwenye shukrani? Ni nani anayeweza kuja ana kwa ana na Mungu? Mara nyingi huwa ninaombea kundi letu ili liweze kupokea baraka zaidi kutoka kwa Mungu ili tuweze kupata kibali kutoka kwa Mungu na kupatwa na Yeye, lakini kumekuwa na nyakati zisizohesabika ambapo nimetokwa na machozi kwa ajili yetu, nikiomba kwamba Mungu atupe nuru sisi, na kuturuhusu kuwa na ufunuo mkubwa zaidi. Nionapo kwamba watu wanajaribu kumpumbaza Mungu kila mara na bila azimio, kufikiria mwili au kung'ang'ana ili umaarufu na bahati viwe katikati ya jukwaa, Ningekosaje kuhisi uchungu mwingi ndani ya moyo Wangu? Watu wanawezaje kuwa wapumbavu hivi? Ni kweli kwamba kile Nifanyacho hakizai matunda? Ikiwa watoto wako wote wangekuwa waasi na wasio na upendo kwako, bila dhamiri, wa kujijali wenyewe tu, wakakosa kamwe uwezo wa kuhisi hisia zako, na wakakutupa tu nje ya nyumba baada ya wao kukua, ungehisi vipi wakati huo? Hungejawa na machozi na kukumbuka ya kale kuhusu gharama kuu uliyolipa kuwakuza? Hii ndiyo maana Nimemwomba Mungu mara nyingi: “Mpendwa Mungu! Ni wewe tu ujuaye ikiwa Nina mzigo wowote au la katika kazi Yako. Katika sehemu zozote ambapo matendo Yangu hayalingani na mapenzi Yako, Unanifunza nidhamu, Unanikamilisha, na Unanifanya Nifahamu. Ombi Langu la pekee Kwako ni kwamba Uwasisimue watu hawa zaidi ili hivi punde Upate utukufu na watu hawa wapatwe na Wewe, na kwamba kazi Yako itimize kile ambacho ni mapenzi Yako na uweze kukamilisha mpango Wako hivi punde.” Mungu hataki kuwashinda watu kupitia kuadibu; Hataki kila mara kuwatawala watu kabisa. Anataka watu watii maneno Yake na kufanya kazi kwa mtindo wa nidhamu, na kupitia hili kuridhisha mapenzi Yake. Lakini watu hawana aibu na kila mara huasi dhidi Yake. Naamini kwamba ni bora zaidi kwetu kutafuta njia rahisi sana ya kumridhisha Yeye, yaani, kutii mipango Yake yote, na ikiwa utatimiza hili kwa kweli utakamilishwa. Je, hili si jambo rahisi, la kufurahisha? Fuata njia unayopaswa kufuata bila kufikiria kile ambacho wengine wanasema au kufikiria sana. Je, una siku zako za baadaye na jaala yako mikononi mwako? Wewe kila mara hukimbia na kutaka kufuata njia ya kidunia, lakini mbona usitoke nje? Kwa nini wewe huyumbayumba katika njia panda kwa miaka mingi na kisha unaishia kuichagua njia hii tena? Baada ya kutangatanga kwa miaka mingi, ni kwa nini umerudi sasa katika nyumba hii ingawa hukutarajia kufanya hivyo? Je, hili ni jambo lako mwenyewe tu? Kwa ninyi mlio katika mkondo huu, msipoamini hili, basi Nisikizeni tu Nikisema hili: Ikiwa unapanga kuondoka, ngoja tu uone ikiwa Mungu atakuruhusu, na uone vile Roho Mtakatifu atakusisimua—jionee mwenyewe. Kusema kweli, hata ukipata taabu, lazima uivumilie ndani ya mkondo huu, na ikiwa kuna mateso, lazima uteseke hapa leo na huwezi kwenda penginepo. Unaliona kwa dhahiri? Ungeenda wapi? Hii ni amri ya Mungu ya usimamizi. Unafikiria haina maana kwa Mungu kuchagua kundi hili la watu? Katika kazi ya Mungu leo, Yeye hakasiriki kwa urahisi, lakini watu wakitaka kuvuruga mpango Wake Anaweza kubadilisha sura Yake mara moja na kuigeuza kutoka kuwa yenye kung’aa hadi ya kuhuzunisha. Kwa hiyo, Nakushauri kutulia na kutii mipango ya Mungu, mruhusu akufanye uwe mkamilifu. Hii ndiyo njia pekee ya kuwa mtu stadi.

Chanzo: Neno la Mwenyezi Mungu | Njia … (7)


Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING