29 Sep
Neno la Mungu | “Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee” (Dondoo 1)

Neno la Mungu | “Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee” (Dondoo 1)

Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe. Huzuni iliyoje! Kuokolewa kwa mwanadamu hakuwezi kutenganishwa na usimamizi wa Mungu, aidha hakuwezi kutenganishwa na mipango ya Mungu. Na bado mwanadamu hafikirii chochote kuhusu usimamizi wa Mungu, na hivyo anaendelea kujitenga mbali na Mungu. Kutokana na hayo, idadi ya watu wanaomfuata Mungu inaendelea kuongezeka bila kujua mambo yanayohusiana na kuokolewa kwa mwanadamu kama vile uumbaji ni nini, kuamini kwa Mungu ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na kadhalika. Kufikia sasa, basi, lazima tuzungumze kuhusu usimamizi wa Mungu, ndiposa kila mfuasi ajue wazi umuhimu wa kumfuata Mungu na kumwamini. Watakuwa na uwezo wa kuchagua njia watakayoifuata ipasavyo, badala ya kumfuata Mungu tu ili kupata baraka, au kuepukana na majanga, au kuwa na mafanikio.

Unaweza Pia Kupenda: Wokovu ni nini? Mapenzi ya Bwana Yesu kuhusu kusulubiwa kwake ni yepi? Katika sehemu hii, utapata maarifa ya kina ya wokovu wa Yesu Kristo.

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING