29 Jul
Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Kwanza

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Kwanza


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.

Maudhui ya video hii:

Kwa Kupinga Mungu kwa Ukaidi, Binadamu Anaangamizwa na Hasira za Mungu

Kupotoka kwa Sodoma: Kunakasirisha Binadamu, Kunaghadhibisha Mungu

Sodoma Yaangamizwa kwa Kukosea Hasira za Mungu

Baada ya Ukinzani wa Mara kwa Mara wa Sodoma na Ukatili Wao Dhidi Yake, Mungu Anaufuta Kabisa

Kwanza, hebu tuweze kuangalia mafungu mbalimbali ya maandiko yanayofafanua “kuangamizwa kwa Sodoma na Mungu.”

Mwa 19:1-11 Na jioni malaika wawili walikuja Sodoma; naye Lutu aliketi katika lango la Sodoma: na baada ya Lutu kuwaona aliinuka kwenda kuwakaribisha; na akasujudu; Naye akasema, Tazama saa hii, bwana zangu, ingieni ndani, nawaomba, ndani ya nyumba ya mtumishi wenu, na mbaki usiku mzima, na msafishe miguu yenu, na mtaamka mapema, na mshike njia zenu. Nao wakasema, La; lakini tutaketi katika uwanja usiku mzima. Na akawaomba sana; na wakamjia na kuingia katika nyumba yake; na akawaandalia karamu, na kupika mikate bila chachu, na wakala. Lakini kabla ya wao kujilaza, watu kutoka mjini, hata wenyeji wa Sodoma, waliizunguka nyumba hiyo, wazee na pia vijana, watu wote kutoka kila sehemu: Na wakamwita Lutu, na kumwambia, Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua. Naye Lutu akatoka mlangoni mahali walipokuwa, na akafunga mlango nyuma yake, Na kusema, nawaomba, ndugu, msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu. Na walisema. Toka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango. Lakini watu wale wakanyosha mbele mkono wao, na kumvuta Lutu katika nyumba walikokuwa, na kuufunga mlango. Na wakawagonga wale watu waliokuwa katika mlango wa nyumba na upofu, wakubwa na wadogo: kiasi kwamba walijichosha kuutafuta mlango.

Swali la 28: Unashuhudia kwamba Bwana Yesu amekwisha kurudi kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili, ambaye huonyesha ukweli wote ambao humtakasa na kumwokoa wanadamu na ambaye hufanya kazi ya hukumu akianzia na familia ya Mungu, hivyo tunafaa kutambuaje sauti ya Mungu na tunafaa kuthibitishaje kwamba Mwenyezi Mungu ndiye hasa Yesu aliyerudi?

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING