Utambulisho wa Asili wa Mwanadamu na Thamani Yake: Je, ni Nini?
Utambulisho wa Asili wa Mwanadamu na Thamani Yake: Je, ni Nini?
10 Jan
Mlitengwa kutoka kwa matope na kwa vyovyote vile, mlichaguliwa kutoka kwa mashapo, wachafu na mliochukiwa na Mungu. Mlikuwa wa Shetani[a] na wakati mmoja mlikanyagwa na kuchafuliwa na yeye. Hii ndiyo maana inasemwa kuwa mlitengwa kutoka kwa matope, na nyinyi si watakatifu, lakini badala yake nyinyi ni vitu visivyo binadamu ambavyo Shetani kwa muda mrefu alikuwa amevifanya vipumbavu. Haya ndiyo maelezo sahihi zaidi yenu. Lazima mtambue kuwa nyinyi ni uchafu unaopatikana katika maji yaliyotuama na matope, kinyume na ushikaji unaofaa kama samaki na uduvi, kwa maana hakuna starehe inayoweza kupatikana kutoka kwenu. Kuzungumza waziwazi, nyinyi ni wanachama wa kiwango cha chini sana cha kijamii, wanyama wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Kusema kweli, kuwahutubia kwa istilahi kama hizo si chuku au kutia chumvi, lakini ni njia ya kurahisisha suala hilo. Kuwahutubia kwa istilahi kama hizo kwa kweli ni njia ya kuwapa heshima. Utambuzi wenu, hotuba, mwenendo kama watu, na vitu yote katika maisha yenu—ikiwa ni pamoja na hali yenu katika matope—vinatosha kuthibitisha kwamba utambulisho wenu ni “wa kipekee.”
Matamshi ya Mwenyezi Mungu hutoa ushuhuda wa mamlaka Yake, tabia yenye haki, kiini kitakatifu, kupelekea binadamu kumwelewa Mungu Mwenyewe wa peke na kuanza kutembea kwenye njia ya kumjua!