10 Jul
sauti ya Mungu | Njia … (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

sauti ya Mungu | Njia … (1)

Katika maisha yake, hakuna mtu anayejua ni aina gani ya vipingamizi atakavyoenda kukutana navyo, wala hajui ni aina gani ya kusafishwa ambayo atapata mara kwa mara. Kwa wengine ni katika kazi yao, kwa wengine ni katika matazamio yao ya siku za baadaye, kwa wengine ni katika familia yao ya asili, na kwa wengine ni katika ndoa yao. Lakini kilicho tofauti nayo ni kwamba leo sisi, kundi hili la watu, tunateseka kwa ajili ya neno la Mungu. Yaani, kama mtu anayemtumikia Mungu, tumekumbana na vipingamizi katika njia ya kuamini katika Yeye, na hii ni njia ambayo waumini wote hufuata na ni njia iliyo chini ya miguu yetu yote. Ni kutoka katika kipengele hiki ndipo tunaanza rasmi mwendo wetu wa kuamini katika Mungu, kuanza maisha yetu kama binadamu, na kuingia katika njia sahihi ya maisha. Yaani, ni wakati ambapo tunaingia katika njia sahihi ya Mungu kuishi pamoja na mwanadamu, ambayo watu wa kawaida huifuata. Kama mtu anayesimama mbele ya Mungu na kumhudumia Yeye, yaani, mtu anayevaa mavazi rasmi ya kuhani katika hekalu, aliye na hadhi takatifu na mamlaka na uadhama wa Mungu, Natoa tangazo lifuatalo kwa watu wote. Kulieleza wazi zaidi: Sura tukufu ya Mungu ni utukufu Wangu, mpango wa usimamizi Wake ni kiini Changu. Sitafuti kupata mara mia katika ulimwengu ujao, lakini kuyafanya mapenzi ya Mungu katika ulimwengu huu ili Aweze kufurahia sehemu moja ndogo ya utukufu Wake duniani kwa ajili ya juhudi chache Ninazotoa katika mwili. Hii ndiyo shauku Yangu pekee. Katika maoni Yangu, hii ndiyo riziki Yangu ya pekee ya kiroho; Naamini kwamba haya yanapaswa kuwa “maneno ya mwisho” ya mtu anayeishi katika mwili na ambaye amejawa na hisia. Hii ni njia iliyo chini ya miguu Yangu leo. Naamini kwamba mtazamo huu Wangu ni maneno Yangu ya mwisho katika mwili, na natarajia kwamba watu hawana fikira au mawazo mengine kunihusu Mimi. Ingawa Nimejitoa kikamilifu, bado Sijaweza kuridhisha mapenzi ya Mungu mbinguni. Nina huzuni kupita kiasi—Mbona hiki ni kiini cha mwili? Kwa hiyo, kwa sababu ya mambo Niliyofanya katika siku zilizopita pamoja na kazi ya ushindi ambayo Mungu ametekeleza juu Yangu, ni wakati huu tu ndio Nimepata ufahamu wa kina wa kiini cha wanadamu. Ni tangu wakati huo tu ndipo Nimejiwekea Mwenyewe kiwango cha msingi zaidi: kutafuta tu kuyafanya mapenzi ya Mungu, kujitoa kikamilifu, na kutokuwa na chochote kinachosumbua dhamiri Yangu. Sijishughulishi na masharti gani wengine wanaomhudumia Mungu wamejiwekea wenyewe. Kwa kifupi, Nimeutayarisha moyo Wangu kuyafanya mapenzi Yake. Hili ni ungamo Langu kama mmoja wa viumbe Wake anayehudumu mbele Yake—mtu ambaye ameokolewa na kupendwa na Mungu, na ambaye amevumilia mapigo Yake. Hili ni ungamo la mtu ambaye amelindwa, amehifadhiwa, amependwa, na kutumiwa sana na Mungu. Kuanza sasa na kuendelea, Nitaendelea katika njia hii mpaka Nimalize kazi muhimu iliyokabidhiwa Kwangu na Mungu. Lakini katika maoni yangu, mwisho wa safari uko karibu sana kwa sababu kazi Yake imetimizwa, na kufikia leo watu wamefanya yote wanayoweza kufanya.

Tangu wakati China bara ilipoingia katika mkondo huu wa kupata tena, makanisa yake ya mitaa yalikua polepole, yakiwa katikati ya kazi ya Roho Mtakatifu. Mungu amefanya kazi bila kukoma katika makanisa haya ya mitaa kwa sababu yamekuwa kiini cha Mungu katika familia ya kifalme iliyoanguka. Kwa sababu Mungu ameanzisha makanisa ya mitaa katika familia kama hizo, bila shaka yoyote Amejawa na furaha—ni furaha isiyo na kifani. Baada ya kuanzisha makanisa ya katika China bara na kueneza habari hii nzuri kwa ndugu katika makanisa mengine kote ulimwenguni, Mungu alisisimuka sana—hii ilikuwa hatua ya kwanza ya kazi Aliyotaka kufanya katika China bara. Ingesemwa kwamba hili lilikuwa tendo la kwanza, kwamba Mungu ameweza kuanza hatua ya kwanza ya kazi Yake katika mahali ambapo ni sawa na mji wa pepo wabaya usioshambuliwa na chochote, na mtu yeyote—je, hiyo si nguvu kuu ya Mungu? Ni wazi kwamba ili kupata tena kazi hii, ndugu wasiohesabika wameuawa kishahidi, wakifa kutokana na upanga wa mauaji wa shetani. Kulitaja hili wakati huu kunaleta huzuni nyingi, lakini kwa sehemu kubwa, siku za kuteseka zimepita. Sasa Naweza kumtumikia Mungu, na Nimeweza kufika mahali Nilipo leo yote ni kwa sababu ya nguvu za Mungu. Nina uvutiwaji mkuu kwa wale ambao Mungu aliwachagua kwa ajili ya kifo cha kishahidi—waliweza kuyafanya mapenzi ya Mungu na kujitoa wenyewe mhanga kwa ajili ya Mungu. Kusema kweli, kama isingekuwa kwa neema na fadhili za Mungu, Ningekuwa nimezimia katika matope zamani sana. Shukrani ziwe kwa Mungu! Niko radhi kumpa Mungu utukufu wote, kumruhusu Yeye kuwa na raha. Watu wengine huniuliza Mimi: “Kwa sababu ya cheo chako Hupaswi kufa, kwa hivyo mbona Wewe hufurahi Mungu anapotaja kifo?” Huwa Sitoi jibu la moja kwa moja; Mimi huwapa tabasamu kidogo na kujibu: “Hii ni njia ambayo ni lazima Niifuatilie, ambayo ni lazima Niifuate bila shaka.” Watu huwa hawaelewi jibu Langu, lakini hunitazama Mimi kwa mshangao tu. Wao wanashangazwa kidogo Nami. Kwa hali yoyote, Naamini kwamba kwa vile hii ni njia ambayo Nimeichagua na pia ni uamuzi Nilioweka mbele ya Mungu, basi bila kujali shida zitakuwa kubwa vipi, Natia tu juhudi ili kuendelea kuifuata. Nafikiri kwamba hii ni ahadi inayopaswa kuungwa mkono na mtu anayemhudumia Mungu. Hawezi kuivunja ahadi yake hata kidogo. Hii pia ni amri, kanuni iliyotolewa zamani sana, katika Enzi ya Sheria, kwamba mtu anayeamini katika Mungu anapaswa kufahamu. Katika uzoefu Wangu, maarifa yangu ya Mungu si makubwa na uzoefu Wangu wa utendaji si muhimu, hata hayastahili kutajwa, kwa hivyo siwezi kuzungumza kwa maoni yoyote ya fahari sana. Kwa hali yoyote, maneno ya Mungu ni lazima yaungwe mkono, na hayawezi kukaidiwa. Kusema kweli, uzoefu wa utendaji Wangu mwenyewe si mkubwa, lakini kwa sababu Mungu ana ushuhuda Kwangu na watu kila mara huwa na imani ya upofu Kwangu, Naweza kufanya nini? Naweza tu kujichukulia Mwenyewe kuwa na bahati mbaya. Kwa hali yoyote, bado Natarajia kwamba watu watarekebisha mitazamo yao juu ya kumpenda Mungu. Kwangu binafsi, Mimi si kitu, kwa sababu Mimi pia Ninaandama njia ya imani katika Mungu, na njia Ninayotembea si zaidi ya njia ya imani katika Mungu. Mtu ambaye ni mzuri hapaswi kuwa chombo cha kuabudu—anaweza tu kuwa mfano wa kuigwa. Sijali kile wanachofanya wengine, lakini Mimi huwatangazia watu kwamba Mimi pia humpa Mungu utukufu; Siupi mwili utukufu wa Roho. Natarajia kwamba kila mtu ataweza kuelewa hisia Zangu kuhusu hili. Sio kukwepa wajibu Wangu, lakini ni hadithi yote tu. Hili ni jambo ambalo linapaswa kuwa wazi kabisa, na kuanzia sasa halitahitaji kutajwa tena.

Leo, Nilipata nuru kutoka kwa Mungu. Kazi ya Mungu duniani ni kazi ya wokovu; haihusiani na jambo lingine lolote. Watu wengine wanaweza kufikiria vingine, lakini Mimi huhisi kila mara kwamba Roho Mtakatifu anafanya tu hatua ya kazi ya wokovu, na sio kazi nyingine. Hili linapaswa kuwa wazi. Ni kufikia sasa tu ndipo kazi ambayo Roho Mtakatifu amekuwa akifanya China bara imekuwa wazi—ni kwa nini Mungu angetaka kufungua njia zote na kufanya kazi mahali hapa ambapo pepo wabaya wanakimbia na kutapakaa kila mahali? Inaweza kuonekana kutokana na hili kwamba kazi anayofanya Mungu kwa kiasi kikubwa ni kazi ya wokovu. Kuwa dhahiri kabisa, ni kwa kiasi kikubwa kazi ya ushindi. Kuanzia mwanzo jina la Yesu liliitwa. (Labda wengine hawajapitia hili, lakini Nasema kwamba hii ilikuwa hatua ya kazi ya Roho Mtakatifu.) Hili lilikuwa na makusudi ya kumwacha Yesu wa Enzi ya Neema, kwa hivyo sehemu ya watu walichaguliwa mapema, na kisha baadaye uteuzi huo ulifanywa kuwa mdogo. Baada ya hapo, jina la Witness Lee liliitwa katika China bara—hii ilikuwa sehemu ya pili ya kazi ya kupata tena ya Roho Mtakatifu katika China bara. Hii ilikuwa hatua ya kwanza ya kazi ambapo Roho Mtakatifu alianza kuwateua watu, ambayo ilikuwa kukusanya watu kwanza, kungoja mchungaji awatunze, na jina “Witness Lee” lilitumiwa kutenda huduma hiyo. Mungu binafsi alifanya kazi Yake baada ya kushuhudia jina “Mwenye Nguvu” na kabla ya hapo, ilikuwa katika hatua ya matayarisho. Kwa hivyo, haijalishi ikiwa hilo lilikuwa sahihi au baya, na sio suala kuu katika mpango wa Mungu. Baada ya kushuhudia jina “Mwenye Nguvu,” Mungu alianza rasmi kufanya kazi Yake binafsi na baada ya hilo, matendo Yake kama Mungu katika mwili yalianza rasmi. Kupitia jina “Bwana Mwenye Nguvu,” Aliwatawala wale wote waliokuwa waasi na wakaidi, na wakaanza kuchukua ufanano wa binadamu, kama vile tu mtu anapoingia katika miaka yake ya ishirini na tatu au ishirini na nne, anaanza kuonekana kama mtu mzima halisi. Yaani, watu walikuwa tu wameanza kuwa na maisha ya binadamu wa kawaida, na kupitia jaribio la watendaji huduma, kazi ya Mungu ilibadilika kwa kawaida kwa hatua ya kutenda kazi takatifu. Ingesemwa kwamba hatua hii ya kazi pekee ndiyo kiini cha kazi Yake nyingi na kwamba ni hatua ya msingi katika kazi Yake. Watu wanajijua na wanajichukia. Wamefikia mahali ambapo wanaweza kujilaani wenyewe, wanafurahia kusalimu amri maisha yao wenyewe na wana hisi hafifu ya kupendeza kwa Mungu. Ni juu ya msingi huu ndipo wanaelewa maana halisi ya maisha. Hii ni kutimiza mapenzi ya Mungu. Kazi ya Mungu katika China bara inakaribia mwisho. Mungu amekuwa akitekeleza matayarisho Yake katika nchi hii ya uchafu kwa miaka kadhaa, lakini watu hawakuwa wametimiza kiwango ambacho wamefikia sasa. Hii inamaanisha kwamba ni sasa tu ndio Mungu ameanza rasmi kazi Yake. Hakuna haja ya kueleza kila kitu kwa utondoti kuhusu hili; hili halihitaji kuelezwa na wanadamu. Hatua hii ya kazi bila shaka inafanywa moja kwa moja kupitia kwa utakatifu wa Mungu, lakini inatekelezwa kupitia kwa mwanadamu. Hakuna awezaye kukana hili. Kwa hakika ni kwa sababu ya nguvu kuu za Mungu duniani ndio kazi Yake ingefikia kiasi ambacho imefikia sasa katika watu wa nchi hii ya uasherati. Tunda la kazi hii lingepelekwa popote kuwaridhisha watu. Hakuna ambaye angethubutu kutoa hukumu kwa wepesi kuhusu hili na kulikana.

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING