13 Jul
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia … (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi MunguNjia … (4)

Kwamba watu wanaweza kugundua kupendeza kwa Mungu, kutafuta njia ya kumpenda Mungu katika enzi hii, na kwamba wako radhi kukubali mafunzo ya ufalme wa leo—hii yote ni neema ya Mungu na hata zaidi, ni Yeye ndiye anawainua wanadamu. Kila Nifikiriapo juu ya hili Mimi huhisi kwa uthabiti kupendeza kwa Mungu. Ni kweli kwamba Mungu anatupenda. La sivyo, nani angeweza kutambua kupendeza Kwake? Ni kutoka tu kwa hili ndio Naona kwamba kazi hii yote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na watu wanaongozwa na kuelekezwa na Mungu. Natoa shukrani kwa Mungu kwa hili, na Ningependa ndugu na dada Zangu wajiunge na Mimi kumsifu Mungu: “Utukufu wote uwe Kwako, Mungu Mwenyewe mwenye uwezo mkubwa kabisa! Utukufu Wako uzidishwe na kufichuliwa ndani yetu sisi ambao tumeteuliwa na kupatwa na Wewe”. Nimepata nuru kutoka kwa Mungu—kabla ya enzi Mungu alikuwa tayari ametujaalia na Alitaka kutupata katika siku za mwisho, hivyo kuruhusu vitu vyote katika ulimwengu kuona utukufu wa Mungu katika uzima wake kupitia kwetu. Hivyo, sisi ni dhihirisho la miaka elfu sita ya mpango wa usimamizi wa Mungu; sisi ni vielelezo, sampuli za kazi ya Mungu katika ulimwengu wote. Ni kufikia wakati huu tu ndio Nimeweza kugundua ni upendo wa kiasi gani alio nao Mungu kwa kweli kwetu, na kwamba kazi Afanyayo ndani yetu na mambo Ayasemayo yote yanapita yale ya enzi zilizopita mara milioni. Hata katika Israeli na ndani ya Petro, Mungu hakuwahi kufanya binafsi kazi nyingi hivyo na kuzungumza mengi hivyo. Hili linaonyesha kwamba, hili kundi la watu, kweli wamebarikiwa ajabu sana—limebarikiwa zaidi ya watakatifu wa nyakati zilizopita kwa kiasi kisichoweza kulinganishwa. Hii ndio maana Mungu amesema kila mara kwamba watu wa enzi ya mwisho wamebarikiwa. Haijalishi wengine wanasema nini, Naamini kwamba sisi ndio wale wamebarikiwa zaidi na Mungu. Tunapaswa kukubali baraka tulizopewa na Mungu; labda kuna wengine ambao watalalamika kwa Mungu, lakini Naamini kwamba baraka hutoka kwa Mungu na hiyo inathibitisha kwamba hizo ndizo tunastahili. Hata kama wengine wanalalamika au hawatufurahii, Mimi huamini kila mara kwamba hakuna anayeweza kukubali au kuchukua baraka ambazo Mungu ametupa. Kwa sababu kazi ya Mungu inatekelezwa juu yetu na Ananena nasi ana kwa ana—kwetu sisi, sio kwa wengine—Mungu hufanya chochote Anachotaka kufanya, na ikiwa watu hawaridhiki, huko si kujitakia tu tatizo? Je, huko si kukaribisha aibu? Ni kwa nini Niseme hili? Ni kwa sababu Nina uzoefu wa kina na hili. Kama tu kazi ambayo Mungu hufanya juu Yangu ambayo ni Mimi tu Niwezaye kuikubali—je, mtu yeyote mwingine anaweza kuifanya? Nina bahati kwamba Mungu amenikabidhi Mimi hili—je, mtu yeyote mwingine angeweza kufanya hilo bila kuchagua kwa busara? Lakini Natarajia kwamba ndugu na dada Zangu wataweza kufahamu moyo Wangu. Sio kushikilia kwa nguvu sifa Zangu mimi kujisifu kwa watu, lakini ni kueleza suala fulani. Niko radhi kumpa Mungu utukufu wote na kumwacha Yeye achunguze kila mojawapo ya mioyo yetu ili mioyo yetu yote itakaswe mbele ya Mungu. Ningependa kutoa ombi moja kwa dhati kabisa: Natarajia kupatwa na Mungu kabisa, kuwa mwanamwali safi anayetolewa kama dhabihu juu ya madhabahu, na hata zaidi kuwa na utii wa mwanakondoo, kujitokeza miongoni mwa wanadamu wote kama mwili mtakatifu wa kiroho. Hii ni ahadi Yangu, kiapo Nilichoanzisha mbele ya Mungu. Niko radhi kuitimiza na kulipa upendo wa Mungu kupitia hii. Je, uko radhi kufanya hili? Naamini kwamba ahadi hii Yangu itawatia moyo ndugu na dada wadogo zaidi, na kuwapa tumaini vijana wadogo zaidi. Nahisi kuwa inaonekana kwamba Mungu huweka sisitizo maalum juu ya vijana. Labda ni upendeleo Wangu mimi, lakini Mimi huhisi kila mara kwamba vijana wana tumaini kuhusu siku zao za baadaye; inaonekana kwamba Mungu hufanya kazi ya ziada katika vijana. Ingawa wanapungukiwa na utambuzi na hekima na wao wote ni wachangamfu kupita kiasi na wakaidi kama ndama aliyezaliwa, Naamini kwamba vijana hawajakosa sifa njema kabisa. Unaweza kuuona umaasumu wa ujana ndani yao na wao ni wepesi kukubali mambo mapya. Ingawa vijana huelekea kwa kiburi, ukali, na uamuzi wa ghafla, mambo haya hayaathiri uwezo wao wa kupokea mwanga mpya. Hii ni kwa sababu vijana kwa jumla huwa hawashikilii sana vitu vya mtindo wa zamani. Hii ndiyo maana Naona matumaini yasiyo na mipaka katika vijana, na uchangamfu wao; ni kutokana na hili ndio maana Nina hisia njema kwao. Ingawa Sina chuki yoyote kwa ndugu na dada wazee, pia sina haja na wao. Mimi Naomba radhi kwa dhati kutoka kwa ndugu na dada wazee. Labda Nilichosema hakifai au ni kisichojali hisia za wengine, lakini Natarajia kwamba nyote mtawia radhi kutojali Kwangu, kwa sababu Mimi ni mdogo sana na Sitilii mkazo sana mwenendo Wangu wa kuzungumza. Hata hivyo, kusema kweli, ndugu na dada wazee, hata hivyo, wana kazi zao wanazopaswa kutenda—wao sio bure kamwe. Hii ni kwa sababu wana uzoefu wa kushughulikia mambo, wako thabiti jinsi wanavyoshughulikia mambo, na hawafanyi makosa mengi sana. Je, huu si uwezo wao? Ningependa sote tuseme mbele ya Mungu: “Ee Mungu! Sote na tuweze kutimiza kazi zetu katika nafasi mbalimbali, na sote tufanye vizuri kabisa tuwezavyo kwa ajili ya mapenzi Yako! ”Naamini haya lazima yawe mapenzi ya Mungu!

Kutokana na yale Niliyoona katika uzoefu Wangu, wengi ambao wameupinga mkondo huu, yaani, wengi ambao wamepinga Roho wa Mungu wazi, wamekuwa wazee. Fikira za kidini ambazo watu hawa wanashikilia ni za nguvu sana na wao hulinganisha mambo ya mtindo wa zamani kwa maneno ya Mungu katika kila hali. Wao kila mara hutumia mambo waliyokubali katika wakati uliopita kwa maneno ya Mungu. Je, wao si wa upuuzi? Mtu kama huyo anaweza kufanya kazi ya Mungu? Mungu anaweza kumtumia mtu wa aina hiyo kwa kazi Yake? Roho Mtakatifu ana utaratibu kwa siku yoyote ile ya kazi Yake; ikiwa watu watashikilia mambo ya mtindo wa zamani, siku itakuja ambayo watasukumwa kutoka kwa jukwaa la historia. Katika kila hatua ya kazi Yake, Mungu huwatumia watu wapya kila mara. Ikiwa mtu angewahubiria wengine na mambo yasiyotumika siku hizi, hii haingekuwa tu kuwaangamiza watu? Hii haingekuwa kuchelewesha kazi Yake? Kwa hiyo kazi ya Mungu inaweza kutimizwa lini? Labda kuna wengine ambao wana fikira zingine kuhusu kile ambacho Nimesema sasa. Labda hawataridhishwa. Hata hivyo, Natarajia kwamba huna wasiwasi; mambo mengi kama haya yatafanyika hapo baadaye, na hili linaweza tu kufafanuliwa kupitia kwa ukweli. Huenda hata tukawatembelea watu fulani wa maana, wachungaji fulani wenye hadhi kuu au wafasiri wa Biblia na kuwahubiria mkondo huu. Hapo mwanzo, kwa hakika hawatapinga waziwazi, lakini watachomoa Biblia kushindana na wewe. Watakufanya usimulie Kitabu cha Isaya na Kitabu cha Danieli, na hata watakufanya ueleze Kitabu cha Ufunuo. Na kama hutaweza kuizungumzia, watakukataa, na kukuita Kristo wa uongo, na kusema kwamba unaeneza njia ya upuuzi. Baada ya saa nzima watatoa lawama za uongo dhidi yako mpaka utakosa pumzi. Je, huu si upinzani ulio wazi? Lakini huo ni mwanzo tu. Hawawezi kuzuia hatua inayofuata ya kazi ya Mungu, na kabla ya muda mrefu, Roho Mtakatifu atawalazimisha kuikubali. Huu ni mwelekeo wa jumla; ni kitu ambacho wanadamu hawawezi kukifanya na kitu ambacho watu hawawezi kukiwaza. Naamini kwamba kazi ya Mungu itaenea kote ulimwenguni bila kuzuiwa. Haya ni mapenzi ya Mungu, na hakuna anayeweza kuyazuia. Mungu na atupe nuru na kutufanya tukubali nuru mpya zaidi na sio kuingilia usimamizi wa Mungu katika suala hili. Mungu atuonee huruma ili kwamba sote tuweze kuona kuja kwa siku Yake ya utukufu. Mungu atakapotukuzwa kote katika ulimwengu mzima huo ndio wakati ambao tutapata utukufu pamoja Naye. Inaonekana kwamba huo pia ndio wakati ambao Nitaondoka kwa wale wanaotembea na Mimi. Natarajia kwamba ndugu na dada Zangu watapaza sauti zao pamoja na Yangu kumwomba Mungu: Kazi kuu ya Mungu na ikamilike hivi punde ili tuione siku Yake ya utukufu wakati wa maisha yetu. Bado Natarajia kutimiza mapenzi ya Mungu wakati wa maisha Yangu, na Natarajia kwamba Mungu ataendelea kufanya kazi Yake ndani yetu na kwamba hakutakuwa na vizuizi vyovyote. Hii ndiyo hamu Yangu ya milele. Mungu awe miongoni mwetu kila mara na upendo Wake ujenge daraja kati yetu ili urafiki ulio kati yetu uwe wa thamani zaidi. Natarajia kwamba upendo utasababisha uelewano zaidi kati yetu na kwamba upendo utatufanya tukaribiane, kuondoa pengo lililo kati yetu, na kwamba upendo ulio kati yetu uwe wa kina zaidi, mpana zaidi, na wa kupendeza zaidi. Naamini kwamba haya ni mapenzi ya Mungu. Natarajia kwamba ndugu na dada Zangu watakuwa na urafiki wa karibu sana nami, na kwamba sote tuthamini siku chache tulizo nazo pamoja na zinaweza kuwa kumbukumbu nzuri kwetu.

Kumekuwa na hatua zaidi za kazi ya Mungu katika China bara lakini si zenye utata hata kidogo. Kufikiria juu ya hatua hizo zote, hazikosi sababu—zote zimekamilishwa na Mungu Mwenyewe, na watu wote huchukua nafasi mbalimbali katika kazi Yake. Kila onyesho katika mchezo huu ni la kuchekesha kwa watu, na la ajabu kila mtu ana nafasi ndani yake. Katika kila jaribio, utendaji wa watu huwa wa kweli kwa maisha, na kila mtu amechorwa kwa dhahiri sana na kikamilifu na kalamu ya Mungu. Kila mtu ana mengi yanayofichuliwa katika mwangaza wa siku. Sisemi kwamba Mungu anawadhihaki watu kupitia kwa kazi Yake; hakungekuwa na maana katika hilo. Kazi yote ya Mungu ina kusudi lake; bila shaka Hafanyi chochote kisichokuwa na umuhimu au thamani. Mambo yote Ayafanyayo ni ya kuwakamilisha na kuwapata wanadamu. Ni kutoka tu kwa hayo ndio Nimeona kweli kwamba moyo wa Mungu wote ni kwa wema wa mwanadamu. Ingawa unaweza kuitwa mchezo wa kuigiza, inaweza pia kusemwa kwamba mchezo huu wa kuigiza ni mfano wa maisha ya kweli, lakini kwa mwendeshaji mkuu wa tamthiliya, Mungu, watu wote wanatakiwa kushirikiana ili kuikamilisha kazi hii. Lakini kutoka upande mwingine, Mungu huwapata watu kupitia hili na kuwafanya watu wampende Yeye zaidi. Je, haya si mapenzi Yake? Kwa hiyo Natarajia kwamba hakuna aliye na matatizo. Je, hujui lolote kuhusu mapenzi ya Mungu? Nimesema mengi sana—Natarajia kwamba ndugu na dada Zangu wote wanaweza kufahamu na sio kutofahamu moyo Wangu. Naamini kwamba Mungu atawapata kikamilifu. Kila mtu hutembea njia tofauti. Natarajia kwamba njia iliyo chini ya miguu yenu ni ile ambayo imefunguliwa na Mungu, na kwamba nyote mtaomba na kusema: “Ee Mungu! Nipate mimi ili roho yangu ikurudie Wewe.” Je, uko tayari kutafuta uongozi wa Mungu ndani ya kina cha roho yako?

Chanzo: Njia … (4)

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING