05 Jul
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Biblia (1)

Biblia inapaswa kuangaliwaje kuhusiana na imani kwa Mungu? Hili ni swali muhimu sana. Kwa nini tunawasiliana swali hili? Kwa sababu wakati ujao utaeneza injili na kupanua kazi ya Enzi ya Ufalme, na haitoshi tu kuweza kuzungumza juu ya kazi ya Mungu leo. Ili kupanua kazi Yake, ni muhimu zaidi kwamba unakuwa na uwezo wa kubadilisha dhana za watu za dini ya kale na njia za kale za imani, na kuwaacha wakiwa wameshawishika kabisa—na kufikia katika hoja hiyo Biblia inahusishwa. Kwa miaka mingi, imani ya watu ya kitamaduni (hiyo ya Ukristo, moja ya dini kuu tatu za dunia) imekuwa ni kusoma Biblia; kujitenga na Biblia sio imani kwa Bwana, kujitenga na Biblia ni kufuata imani tofauti tofauti na uzushi, na hata pale watu wanaposoma vitabu vingine, msingi wa vitabu hivi ni lazima uwe ni ufafanuzi wa Biblia. Ni kusema kwamba, kama unasema unamwamini Bwana, basi ni lazima usome Biblia, unapaswa kula na kunywa Biblia, na nje ya Biblia hupaswi kuabudu kitabu kingine ambacho hakihusishi Biblia. Ikiwa utafanya hivyo, basi unamsaliti Mungu. Kuanzia kipindi ambapo kulikuwa na Biblia, imani ya watu kwa Bwana imekuwa imani katika Biblia. Badala ya kusema watu wanamwamini Bwana, ni bora kusema kwamba wanaamini Biblia; badala ya kusema wameanza kusoma Biblia, ni bora kusema wameanza kuamini Biblia; na badala ya kusema wamerudi mbele ya Bwana, ingekuwa vyema kusema wamerudi mbele ya Biblia. Kwa njia hii, watu wanaiabudu Biblia kana kwamba ni Mungu, kana kwamba ni damu yao ya uzima na kuipoteza itakuwa ni sawa na kupoteza maisha yao. Watu wanaitazama Biblia kuwa ni kuu kama Mungu, na hata kuna wale wanaoiona kuwa ni kuu kuliko Mungu. Kama watu hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, ikiwa hawawezi kuhisi Mungu, wanaweza kuendelea kuishi—lakini punde tu watakapoipoteza Biblia, au kupoteza sura na maneno maarufu sana kutoka katika Biblia, basi inakuwa ni kana kwamba wamepoteza maisha yao. Na hivyo, pale ambapo watu wataanza kumwamini Bwana wanaanza kusoma Biblia, na kuikariri Biblia, na kadri ya sehemu kubwa ya Biblia wanayoweza kukariri, ndivyo hii inathibitisha kwamba wanampenda Bwana na ni watu wenye imani kuu. Wale ambao wameisoma Biblia na wanaweza kuizungumzia kwa wengine wote ni kaka na dada wazuri. Kwa miaka yote hii, imani ya watu na uaminifu kwa Bwana vimepimwa kulingana na kiwango cha ufahamu wao wa Biblia. Watu wengi hawaelewi kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu, wala jinsi ya kumwamini Mungu, na hawafanyi chochote zaidi ya kutafuta kiupofu dondoo ili kufasiri sura za Biblia. Hawajawahi kufuata mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu; muda wote huo, hawajafanya chochote, bali kujifunza na kuchunguza Biblia kwa papara, na hakuna hata mmoja ambaye amepata kazi mpya ya Roho Mtakatifu nje ya Biblia, hakuna ambaye amewahi kujitenga na Biblia, wala kuthubutu kujitenga na Biblia. Watu wamejifunza Biblia kwa miaka yote hii, wamekuja na maelezo mengi sana, na kufanya kazi kubwa sana, pia wana maoni mengi tofauti kuhusu Biblia, ambayo yamekuwa ni mdahalo usiokwisha, kiasi kwamba ziadi ya madhehebu elfu mbili yameanzishwa hadi leo. Wote wanataka kutafuta ufafanuzi maalumu, au siri za kina zaidi katika Biblia, wanataka kuichunguza, na kuipata katika usuli wa kazi ya Yehova katika Israeli, au usuli wa kazi ya Yesu katika Yudea, au siri nyingi zaidi ambazo hakuna yeyote anayejua. Watu wanavyoichukulia Biblia ni shauku na imani, na hakuna anayeweza kufafanua kikamilifu kisa cha ndani au kiini cha Biblia. Kwa hivyo, leo watu bado wana hisia zisizoelezeka za kimiujiza linapokuja suala la Biblia; hata zaidi ya hapo, wana shauku nayo sana, na wanaiamini. Leo, kila mtu anataka kutafuta unabii wa kazi ya siku za mwisho katika Biblia, wanataka kugundua ni kazi gani Mungu hufanya wakati wa siku za mwisho na kuna ishara gani ya siku za mwisho. Kwa njia hii, kuabudu kwao Biblia kunakuwa na maana sana, na kadri wanaposogelea siku za mwisho, ndivyo wanavyozidi kuonyesha imani kwenye unabii wa Biblia, hususani ule wa siku za mwisho. Kwa imani hiyo ya upofu katika Biblia, kwa imani hiyo katika Biblia, hawana shauku ya kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu. Katika dhana za watu, wanadhani kwamba ni Biblia pekee ndiyo inayoweza kuleta kazi ya Roho Mtakatifu; ni katika Biblia pekee ndimo wanamoweza kupata nyayo za Mungu; ni katika Biblia pekee ndimo kulimofichika siri za kazi ya Mungu; ni kwenye Biblia pekee—na sio katika vitabu vinginevyo au watu—wanaoweza kufafanua kila kitu cha Mungu na ujumla wa kazi Yake; Biblia inaweza kuleta kazi ya mbinguni duniani; na Biblia inaweza kuanzisha na kuhitimisha enzi. Kwa dhana hizi, watu hawana shauku kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu. Hivyo, licha ya kiasi gani Biblia ilikuwa ina msaada mkubwa kwa watu wa wakati wa nyuma, imekuwa ni kikwazo katika kazi ya Mungu ya hivi karibuni. Bila Biblia, watu wanaweza kutafuta nyayo za Mungu mahali kwingineko, bado leo, nyayo zake zimejumuishwa na Biblia, na kupanua kazi Yake ya hivi karibuni, imekuwa na ugumu mara mbili, na mapambano magumu. Hii yote ni kwa sababu ya sura na misemo maarufu kutoka katika Biblia, vilevile unabii mbalimbali wa Biblia. Biblia imekuwa sanamu katika akili za watu, limekuwa ni fumbo katika akili zao, na hawawezi kabisa kuamini kwamba Mungu anaweza kufanya kazi nje ya Biblia, hawawezi kuamini kwamba watu wanaweza kumpata Mungu nje ya Biblia, achilia mbali kuwa na uwezo wa kuamini kwamba Mungu angeweza kujitenga na Biblia wakati wa kazi ya mwisho na kuanza upya. Hili suala haliingii akilini mwa watu; hawawezi kuliamini, na wala hawawezi kulifikiria. Biblia imekuwa kikwazo kikubwa kwa watu kukubali kazi mpya ya Mungu, na imefanya kuwa vigumu kuipanua kazi hii mpya. Hivyo, kama hamwelewi kisa cha ndani ya Biblia, hamtaweza kueneza injili kwa mafanikio, wala hamtaweza kuwa na ushuhuda wa kazi mpya. Ingawa, leo, hamsomi Biblia, bado ni maridhia katika Biblia, ambapo ni sawa na kusema, Biblia inaweza isiwe mikononi mwenu, lakini dhana zenu nyingi zinatoka humo. Huelewi asili ya Biblia au kisa cha ndani kuhusu hatua mbili za awali kuhusu kazi ya Mungu. Ingawa hamnywi na kula Biblia, mnapaswa kuielewa Biblia, mnapaswa kupata maarifa sahihi ya Biblia, na ni kwa njia hii tu ndipo mtaweza kujua mpango wa kazi ya Mungu ya usimamizi ya miaka 6000 inahusiana na nini hasa. Mtatumia mambo haya kuwapata watu, kuwafanya wakiri kwamba mkondo huu ni njia ya kweli, kuwafanya wakiri kwamba, njia mnayoiendea leo, ni njia ya kweli, ambayo inaongozwa na Roho Mtakatifu, na haijawahi kufunguliwa na mwanadamu mwingine yeyote.

Kabla ya Enzi za Neema watu walisoma Biblia, lakini wakati huo kulikuwa na Agano la Kale tu; hakukuwa na Agano Jipya. Kwa kuwa kulikuwa na Agano la Kale la Biblia, watu walianza kusoma maandiko matakatifu. Baada ya kuongozwa kwake na Yehova kukamilika, Musa aliandika Mwanzo, Kutoka, na Kumbukumbu la Torati…. Alikumbuka kazi ya Yehova wakati huo, na akaiandika. Biblia ni kitabu cha historia. Ni kweli, pia kinahusisha baadhi ya unabii wa manabii, na unabii huu, kwa namna yoyote ile si historia. Biblia inajumuisha sehemu kadhaa—sio unabii tu, au kazi ya Yehova tu, wala hakuna nyaraka za Paulo pekee. Unapaswa kujua ni sehemu ngapi ambazo Biblia inajumuisha; Agano la Kale linajumuisha Mwanzo, Kutoka…, na pia kuna vitabu vya unabii ambavyo manabii waliandika. Mwishoni, Agano la Kale linakamilika kwa kitabu cha Malaki. Linarekodi kazi ya Enzi ya Sheria, ambayo iliongozwa na Yehova; kuanzia Mwanzo hadi Kitabu cha Malaki, ni rekodi kamilifu ya kazi ya Enzi ya Sheria. Ni sawa na kusema, Agano Jipya linarekodi yote ambayo yalipitiwa na watu ambao waliongozwa na Yehova katika Enzi ya Sheria. Wakati wa Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, idadi kubwa ya manabii iliinuliwa na Yehova, walizungumza unabii kwa niaba Yake, walitoa maelekezo kwa makabila mbalimbali na mataifa, na wakatoa unabii juu ya kazi ambayo Yehova angefanya. Watu hawa ambao wameinuliwa wote walipewa na Yehova Roho ya unabii: Waliweza kutazama njozi kutoka kwa Yehova, na kusikia sauti Yake, na hivyo walivuviwa Naye na wakaandika unabii. Kazi waliyoifanya ilikuwa udhihirisho wa sauti ya Yehova, ilikuwa ni kazi ya unabii ambayo waliifanya kwa niaba ya Yehova, na kazi ya Yehova wakati huo ilikuwa ni kuwaongoza watu kwa njia ya Roho Mtakatifu; Hakufanyika mwili, na watu hawakuona uso Wake. Hivyo, aliwainua manabii wengi kufanya kazi Yake, na akawapatia mashauri ambayo waliyapelekea katika kila kabila na ukoo wa Israeli. Kazi yao ilikuwa ni kusema unabii, na baadhi yao waliandika maelekezo ya Yehova kwa ajili yao ili kuwaonesha wengine. Yehova aliwainua watu hawa kuzungumza unabii, kutoa unabii wa kazi ya wakati ujao au kazi ambayo ilikuwa bado haijafanyika wakati huo, ili kwamba watu wangeweza kutazama maajabu na hekima ya Yehova. Vitabu hivi vya unabii vilikuwa tofauti kabisa na vitabu vingine vya Biblia; yalikuwa ni maneno yaliyozungumzwa au kuandikwa na wale waliopewa Roho ya unabii—na wale ambao walipata njozi au sauti kutoka kwa Yehova. Kuacha vitabu vya unabii, kila kitu kingine katika Agano la Kale ni rekodi zilizochukuliwa na watu baada ya Yehova kukamilisha kazi Yake. Vitabu hivi haviwezi kusimama badala ya unabii uliozungumzwa na manabii walioinuliwa na Yehova, kama ambavyo Mwanzo na Kutoka haviwezi kulinganishwa na Kitabu cha Isaya na Kitabu cha Danieli. Unabii ulikuwa unazungumzwa kabla ya kazi haijafanyika; wakati huo, vitabu vingine viliandikwa baada ya kuwa kazi imemalizika, kazi ambayo watu walikuwa wanaiweza. Manabii wa wakati huo walivuviwa na Yehova na kuzungumza unabii, walizungumza maneno mengi, na walitoa unabii wa mambo ya Enzi ya Neema, na vilevile uharibifu wa dunia katika siku za mwisho—kazi ambayo Yehova alipanga kufanya. Vitabu vilivyosalia vyote vinarekodi kazi iliyofanywa na Yehova katika Israeli. Hivyo, unaposoma Biblia, unakuwa unasoma kile ambacho Yehova alifanya katika Israeli; Biblia ya Agano la Kale kimsingi inarekodi kazi ya Mungu ya kuwaongoza Israeli, kumtumia Musa kuwaongoza Waisraeli kutoka Misri, aliyewaondoa katika shida za Farao, na kuwachukua na kuwapeleka jangwani, ambapo baada ya hapo wakaingia Kaanani na kila kitu baada ya hapa ilikuwa ni kuanza maisha yao Kaanani. Yote, isipokuwa hii ni rekodi za kazi ya Yehova katika Israeli yote. Kila kitu kilichorekodiwa katika Agano la Kale ni kazi ya Yehova katika Israeli, ni kazi Aliyoifanya Yehova katika nchi ambapo Aliwaumba Adamu na Hawa. Kuanzia wakati ambapo Mungu alianza rasmi kuwaongoza watu duniani baada ya Nuhu, yote ambayo yamerekodiwa katika Agano la Kale ni kazi ya Israeli. Na kwa nini hakuna kazi yoyote iliyorekodiwa ambayo ni nje ya Israeli? Kwa sababu nchi ya Israeli ni chimbuko la binadamu. Mwanzoni hakukuwa na nchi yoyote tofauti na Israeli, na Yehova hakufanya kazi katika sehemu nyingine yoyote. Kwa namna hii, kile kilichorekodiwa katika Biblia ni kazi katika Israeli pekee wakati huo. Maneno yaliyozungumzwa na manabii, na Isaya, Danieli, Yeremia na Ezekieli… maneno yao yanatabiri kazi Yake nyingine duniani, yanatabiri kazi ya Yehova Mungu Mwenyewe. Yote haya yalitoka kwa Mungu, ilikuwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, na tofauti na vitabu hivi vya manabii, mambo mengine yote ni rekodi ya uzoefu wa watu juu ya kazi ya Yehova wakati huo.

Kazi ya uumbaji ilitokea kabla ya binadamu kuwepo, lakini Kitabu cha Mwanzo kilikuja tu baada ya kuwepo binadamu; kilikuwa ni kitabu kilichoandikwa na Musa wakati wa Enzi ya Sheria. Ni kama vitu vilivyotokea miongoni mwenu leo: Baada ya kutokea, mnayaandika ili kuwaonyesha watu katika maisha ya baadaye, na kwa watu wa baadaye, mliyoyarekodi ni mambo yaliyotokea wakati uliopita—na si chochote zaidi ya historia. Mambo yaliyorekodiwa katika Agano la Kale ni kazi ya Yehova katika Israeli, na kile kilichorekodiwa katika Agano Jipya ni kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema; ni rekodi ya kazi iliyofanywa na Mungu katika enzi mbili tofauti. Agano la Kale linarekodi kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria, na hivyo Agano la Kale ni kitabu cha kihistoria, wakati Agano Jipya ni zao la kazi ya Enzi ya Neema. Wakati kazi mpya ilipoanza, hii pia ilipitwa na wakati—na hivyo, Agano Jipya pia ni kitabu cha kihistoria. Kimsingi Agano Jipya halina mpangilio mzuri kama Agano la Kale, wala halirekodi mambo mengi. Maneno yote mengi yaliyozungumzwa na Yehova juu ya Agano la Kale yamerekodiwa katika Biblia, ambapo baadhi tu ya maneno ya Yesu yamerekodiwa katika Injili Nne. Ni kweli, Yesu pia alifanya kazi nyingi sana, lakini haikurekodiwa kwa kina. Mambo machache yamerekodiwa katika Agano Jipya ni kwa sababu ya kazi kubwa ambayo Yesu aliifanya; kiwango cha kazi Yake katika miaka mitatu na nusu duniani na kazi ile ya mitume ilikuwa ni pungufu zaidi kuliko kazi ya Yehova. Na hivyo, kuna vitabu pungufu katika Agano Jipya kuliko Agano la Kale.

Biblia ni kitabu cha aina gani? Agano la Kale ni kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria. Agano la Kale la Biblia linarekodi kazi yote ya Yehova wakati wa Enzi ya Sheria na kazi Yake ya uumbaji. Lote linarekodi kazi iliyofanywa na Yehova, na hatimaye linahitimisha maelezo ya kazi ya Yehova kwa kitabu cha Malaki. Agano la Kale linarekodi kazi mbili zilizofanywa na Mungu: Moja ni kazi ya uumbaji, na nyingine ni kuamrisha sheria. Zote ni kazi zilizofanywa na Yehova. Enzi ya Sheria inawakilisha kazi chini ya jina la Yehova Mungu; ni ujumla wa kazi iliyofanywa kimsingi chini ya jina la Yehova. Hivyo, Agano la Kale linarekodi kazi ya Yehova, na Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu, kazi ambayo kimsingi ilifanywa chini ya jina la Yesu. Umuhimu wa jina la Yesu na kazi Aliyoifanya imerekodiwa sanasana katika Agano Jipya. Wakati wa Agano la Kale Enzi ya Sheria, Yehova alijenga hekalu na madhabahu katika Israeli, Aliongoza maisha ya Waisraeli duniani, kuzingatia kwamba walikuwa watu Wake, kundi la kwanza la watu ambalo alilichagua duniani na ambao walikuwa wanautafuta moyo Wake, kundi la kwanza ambalo Yeye Mwenyewe aliliongoza; ni sawa na kusema, makabila kumi na mawili ya Israeli walikuwa ni wateule wa kwanza wa Yehova, na hivyo siku zote Alifanya kazi ndani yao, hadi ambapo kazi ya Yehova ya Enzi ya Sheria ilihitimishwa. Hatua ya pili ya kazi ilikuwa ni kazi ya Enzi ya Neema ya Agano Jipya, na ilifanyika katika kabila la Yuda, moja ya makabila kumi na mawili ya Israeli. Kwamba mawanda ya kazi yalikuwa madogo ilikuwa kwa sababu Yesu alikuwa Mungu alifanyika mwili. Yesu alifanya kazi katika eneo lote la Yudea pekee, na Alifanya tu kazi ya miaka mitatu na nusu; hivyo, kile kilichorekodiwa katika Agano la Kale kiko mbali zaidi kupitiliza kiwango cha kazi kilichorekodiwa katika Agano la Kale. Kazi ya Yesu ya Enzi ya Neema kimsingi imerekodiwa katika Injili Nne. Njia iliyopitiwa na watu wa Enzi ya Neema ilikuwa ile mabadiliko ya juu juu katika tabia yao ya maisha, nyingi zaidi ambayo imerekodiwa katika nyaraka. Nyaraka zinaonyesha jinsi ambavyo Roho Mtakatifu alifanya kazi wakati huo. (Ni kweli, licha ya ama Paulo aliadibiwa au alikutana na majanga, katika kazi aliyofanya alikuwa ameelekezwa na Roho Mtakatifu, alikuwa ni mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu wakati huo; Petro pia, alitumiwa na Roho Mtakatifu, lakini hakufanya kazi kubwa kama aliyofanya Paulo. Ingawa kazi ya Paulo ilikuwa na uchafu wa mwanadamu, kwa kuangalia nyaraka zilizoandikwa na Paulo, inaweza kuonekana ni jinsi gani Roho Mtakatifu alifanya kazi wakati huo; njia ambayo Paulo aliiongoza ilikuwa njia njema, ilikuwa ni sahihi, na ilikuwa ni njia ya Roho Mtakatifu.)

Ikiwa unatamani kuiona kazi ya Enzi ya Sheria, na kuona jinsi gani Waisraeli waliifuata njia ya Yehova, basi ni lazima usome Agano la Kale; ikiwa unatamani kuelewa kazi ya Enzi ya Neema, basi ni lazima usome Agano Jipya. Lakini unawezaje kuona kazi ya siku za mwisho? Ni lazima ukubali uongozi wa Mungu wa leo, na kuingia katika kazi ya leo, maana hii ni kazi mpya na hakuna ambaye ameirekodi katika Biblia hapo nyuma. Leo, Mungu amefanyika mwili, na Amewachagua wateule wengine katika nchi ya China. Mungu anafanya kazi ndani ya watu hawa, Anaendelea na kazi Yake duniani, Anaendelea kutoka katika kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya leo ni njia ambayo mwanadamu hajawahi kuiendea, na njia ambayo hakuna mtu ambaye amewahi kuiona. Ni kazi ambayo haijawahi kufanywa hapo kabla—ni kazi ya Mungu ya hivi karibuni kabisa duniani. Hivyo, kazi ambayo haijawahi kufanywa kabla sio historia, kwa sababu sasa ni sasa, na bado haijawa muda uliopita. Watu hawajui kwamba Mungu amefanya kazi kubwa, mpya duniani, na nje ya Israeli, yaani imevuka mawanda ya Israeli, na zaidi ya unabii wa manabii, ambayo ni kazi mpya na ya kushangaza nje ya unabii, na kazi mpya kabisa nje ya Israeli, na kazi ambayo watu hawawezi kuielewa au kufikiria. Inawezekanaje Biblia kuwa na rekodi za wazi za kazi kama hiyo? Ni nani ambaye angeweza kurekodi kila hatua ya kazi ya leo, bila kuondoa kitu? Ni nani angeweza kurekodi kazi hii kubwa na yenye hekima ambayo inakataa maagano ya kitabu cha kale? Kazi ya leo sio historia, na kama vile, ikiwa unatamani kutembea katika njia ya leo, basi mnapaswa kutengana na Biblia, unapaswa kwenda mbele zaidi ya vitabu vya unabii au historia ya Biblia. Baada ya hapo tu ndipo utaweza kutembea njia mpya vizuri, na baada ya hapo ndipo utaweza kuingia katika ufalme mpya na kazi mpya. Unapaswa kuelewa ni kwa nini leo unaambiwa usisome Biblia, kwa nini kuna kazi nyingine ambayo inajitenga na Biblia, kwa nini Mungu haonekani mpya na wa kina zaidi katika Biblia, kwa nini badala yake kuna kazi kubwa zaidi nje ya Biblia. Haya ndiyo yote mnayopaswa kuelewa. Unapaswa kuelewa tofauti kati ya kazi ya zamani na kazi mpya, na hata kama hausomi Biblia, unapaswa kuitenganisha; kama hautaweza, bado utakuwa unaiabudu Biblia, na itakuwa ni vigumu sana kwako kuingia katika kazi mpya na kupitia mabadiliko mapya. Kwa kuwa kuna njia ya juu, kwa nini mjifunze hiyo ya chini, njia ya kale? Kwa kuwa kuna matamshi mapya, na kazi mpya, kwa nini uishi katikati ya rekodi za kale za kihistoria? Matamshi mapya yanaweza kukupa, ambayo yanathibitisha kwamba hii ni kazi mpya; rekodi za kale haziwezi kukushibisha, au kutosheleza mahitaji yako ya sasa, kitu ambacho kinathibitisha kwamba ni historia, na sio kazi ya hapa na sasa. Njia ya juu zaidi ni njia mpya zaidi, na kazi mpya, bila kujali njia ya zamani ni ya juu kiasi gani, bado ni historia ya kumbukumbu ya watu, na haijalishi ina thamani kiasi gani kama rejeleo, bado ni njia ya kale. Ingawa imerekodiwa katika “kitabu kitakatifu,” njia ya kale ni historia; ingawa hakuna rekodi yake katika “kitabu kitakatifu,” njia mpya ni ya hapa na sasa. Kwa njia hii inaweza kukuokoa, na kwa njia hii inaweza kukubadilisha, maana hii ni kazi ya Roho Mtakatifu.

Mnapaswa kuielewa Biblia—kazi hii ni ya umuhimu mkubwa sana! Leo, unapaswa kusoma Biblia, maana hakuna jipya ndani yake; yote ni ya kale. Biblia ni kitabu cha kihistoria, na ikiwa ungekula na kunywa Agano la Kale wakati wa Enzi ya Neema—ikiwa ungeweka katika vitendo kile kilichokuwa kinatakiwa katika wakati wa Agano la Kale wakati wa Enzi ya Neema—Yesu angekukataa, na kukuhukumu; ikiwa ungetumia Agano la Kale katika kazi ya Yesu, basi ungekuwa Farisayo. Ikiwa, leo, utaweka pamoja Agano Jipya na la Kale kula na kunywa, na kuliweka katika vitendo, basi Mungu wa leo Atakuhukumu; utakuwa umebaki nyuma ya kazi ya leo ya Roho Mtakatifu! Ikiwa unakula na kunywa Agano la Kale na Agano Jipya, basi upo nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu! Wakati wa kipindi cha Yesu, Yesu aliwaongoza Wayahudi na wale wote ambao walimfuata Yeye kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu katika Yeye wakati huo. Hakuichukulia Biblia kama msingi wa kile Alichofanya, bali Alizungumza kulingana na kazi Yake; Hakutilia maanani kile ambacho Biblia ilisema, wala hakutafuta katika Biblia njia ya kuongoza wafuasi Wake. Kuanzia pale Alipoanza kufanya kazi, Aliongoza njia ya toba—neno ambalo halikutajwa kabisa katika unabii wa Agano la Kale. Sio kwamba tu Hakutenda kulingana na Biblia, lakini pia Aliongoza njia mpya, na Akafanya kazi mpya. Na wala Hakurejelea kabisa Biblia Alipohubiri. Wakati wa Enzi ya Sheria, hakuna ambaye aliweza kufanya miujiza Yake ya kuponya wagonjwa na kutoa mapepo. Hivyo, pia, kazi Yake, mafundisho Yake, na mamlaka na nguvu za maneno Yake yalizidi mtu yeyote wakati wa Enzi ya Sheria. Yesu alifanya tu kazi Yake mpya, na ingawa watu wengi walimhukumu kwa kutumia Biblia—na hata wakatumia Agano la Kale kumsulubisha—kazi Yake ilipitiliza Agano la Kale; kama hii haikuwa hivyo, kwa nini watu walimwangika msalabani? Ilikuwa ni kwa sababu haikusema kitu katika Agano la Kale la mafundisho Yake, na uwezo Wake wa kuponya wagonjwa na kutoa mapepo? Kazi Yake ilikuwa ni kwa ajili ya kuongoza katika njia mpya, haikuwa ni kwa makusudi ya kufanya ugomvi dhidi ya Biblia, au kwa makusudi kujitenga na Agano la Kale. Alikuja tu kufanya huduma Yake, kuleta kazi mpya kwa wale waliomtamani sana na kumtafuta. Hakuja kufafanua Agano la Kale au kutetea kazi yake. Kazi Yake bado haikuwa ni kwa ajili ya kuruhusu Enzi ya Sheria kuendelea kukua, maana kazi Yake haikuzingatia Biblia kama msingi wake; Yesu alikuja kufanya tu kazi ambayo Alipaswa kufanya. Hivyo, Hakufafanua unabii wa Agano la Kale, wala Hakufanya kazi kulingana na maneno ya Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Alipuuzia kile ambacho Agano la Kale lilisema, Hakujalia kama lilikubaliana na kazi Yake au la, na Hakujali kile ambacho watu wengine walijua kuhusu kazi Yake, au namna walivyokuwa wakiihukumu. Aliendelea tu kufanya kazi ambayo Alipaswa kufanya, ingawa watu wengi walitumia unabii waliousema manabii wa Agano la Kale kumhukumu. Ilionekana kwa watu kana kwamba kazi Yake haikuwa na msingi, na kulikuwa na mengi ambayo yalikuwa hayapatani na rekodi za Agano la Kale. Je, huu sio upuuzi? Je, kuna ulazima wa kutumia mafundisho ya dini katika kazi ya Mungu? Je, ni lazima iwe kulingana na maneno ya unabii waliyosema manabii? Hata hivyo, kipi ni kikubwa? Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? Ikiwa Angetunza Sabato na matendo mengine kulingana na amri za Agano la Kale, kwa nini Yesu Hakutunza Sabato baada ya kuja, lakini badala yake Aliitawadha miguu, Alivunja mkate, na kunywa divai? Je, sio kwamba haya yote hayapatikani katika amri za Agano la Kale? Ikiwa Yesu aliliheshimu Agano la Kale, kwa nini Aliyakataa mafundisho haya. Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia! Kuwa Bwana wa Sabato, je, Asingeweza pia kuwa Bwana wa Biblia?

Kazi iliyofanywa na Yesu wakati wa Agano Jipya ilifungua kazi mpya: Hakufanya kazi kulingana na kazi ya Agano la Kale, wala Hakutumia maneno yaliyozungumzwa na Yehova wa Agano la Kale. Alifanya kazi yake mwenyewe, na Alifanya kazi mpya zaidi, na kazi ambayo ilikuwa ya juu kuliko sheria. Hivyo, Alisema: “Msidhani ya kwamba Nilikuja kuiharibu torati au manabii; Sikuja kuharibu, bali kutimiliza.” Hivyo, kulingana na kile Alichokitimiza, mafundisho mengi yalikuwa yamevunjwa. Siku ya Sabato Alipowachukua wanafunzi wake kuenda katika shamba la nafaka, walichuma na kula masuke: Alikuwa Anaivunja Sabato, na Akasema, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana hata wa siku ya sabato.” Kwa wakati huo, kulingana na sheria za Waisraeli, yeyote ambaye alikuwa haitunzi Sabato angepigwa na mawe hadi kufa. Hata hivyo Yesu, wala Hakuingia hekaluni wala Hakuitunza Sabato, na kazi Yake haikuwa imefanywa na Yehova wakati wa Agano la Kale. Hivyo, kazi aliyoifanya Yesu inapita sheria ya Agano la Kale, ilikuwa ni ya juu kuipita, na haikuwa na ulinganifu nayo. Wakati wa Enzi ya Neema, Yesu hakufanya kazi kulingana na sheria ya Agano la Kale, Aliyakataa mafundisho hayo. Leo bado kuna watu wanaoitii Biblia na sheria ya Agano la Kale—je, kufanya hivi sio kuikataa kazi ya Yesu? Baadhi ya watu wanasema, “Biblia ni kitabu kitakatifu, na inapaswa kusomwa.” Baadhi ya watu husema, “Kazi ya Mungu inapaswa itetewe milele, Agano la Kale ni agano la Mungu na Waisraeli, na haliwezi kubadilishwa, na Sabato inapaswa kutunzwa siku zote!” Je, hawa sio wapuuzi? Kwa nini Yesu Hakutunza Sabato? Je, Alikuwa Anafanya dhambi? Nani anaweza kuelewa mambo hayo? Haijalishi unasoma Biblia kiasi gani, itakuwa ni vigumu kuijua kazi ya Mungu kwa kutumia nguvu za ufahamu za mwanadamu. Sio tu kwamba utapata maarifa ya Mungu, bali dhana zako zitakuwa za ujinga kupita kiasi, kiasi kwamba utaanza kumpinga Mungu. Kama ingekuwa sio kwa ajili ya Mungu kupata mwili leo, watu wangepotezwa na dhana zao wenyewe, na wangekufa katikati ya kuadibu kwa Mungu.


Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING