22 Dec
Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi

Mwenyezi Mungu


       Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ni kitu ambacho kilikuwa hata zaidi kimeshaamuliwa kabla Nilipoiumba dunia. Watu huenda hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho na pia huenda hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda wale walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini, adui Yangu alipoungana katika vita na Mimi, Nilikuwa Nimeshamwambia kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kufanywa watoto wake na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake. Maana ya asili ya kushinda ni kuangamiza, kufedhehesha. Katika lugha Waisraeli walivyoeleza, ni kushinda kabisa, kuharibu, na kumfanya mwanadamu kutoweza kunipinga zaidi. Lakini leo kama linavyotumika kati yenu binadamu, maana yake ni kushinda. Mnapaswa kujua kwamba dhamira Yangu ni kuzima kabisa na kuangamiza yule mwovu kati ya binadamu, ili asiweze tena kuasi dhidi Yangu, sembuse kuwa na pumzi ya kupinga au kuleta fujo kwa Kazi Yangu. Hivyo, kulingana na wanadamu, imekuja kumaanisha kushinda. Haijalishi kidokezo cha neno hili, kazi Yangu ni kumshinda mwanadamu. Kwani. wakati ni ukweli kwamba mwanadamu ni kijalizo cha usimamizi Wangu, kwa usahihi zaidi, mwanadamu si kitu kingine ila ni adui Yangu. Mwanadamu ni yule mwovu anayenipinga na kuniasi. Mwanadamu si mwingine ila kizazi cha yule mwovu aliyelaaniwa na Mimi. Mwanadamu si mwingine ila ukoo wa malaika mkuu ambaye alinisaliti Mimi. Mwanadamu si mwingine ila mrithi wa shetani ambaye, akiwa amekataliwa kwa dharau na Mimi kitambo, amekuwa adui Wangu asiyeweza kupatanishwa tangu wakati huo. Anga iliyo juu ya jamii ya binadamu ni nzito sana, ni yenye giza na huzuni, bila hata dalili ya uwazi, na ulimwengu wa mwanadamu uko katika giza totoro, kiasi kwamba anayeishi ndani yake hawezi hata kuona mkono wake mwenyewe wakati anapounyosha mbele yake au jua anapoinua kichwa chake. Barabara chini ya miguu yake, ni matope na imejaa mashimo makubwa, ni mipindopindo na ya minyongo; nchi yote imejaa maiti. Pembe za giza zimejaa mabaki ya wafu. Na katika pembe zenye baridi na giza magenge ya mapepo yameshika makazi. Na kila mahali katika dunia ya binadamu, mapepo yanakuja na kwenda katika magenge. Kizazi cha wanyama wa aina yote, waliojawa na uchafu, wanapigana mkono kwa mkono katika mapambano ya kikatili, sauti ambayo huleta hofu moyoni. Nyakati kama hizo, katika dunia kama hiyo, “paradiso ya kidunia” ya aina hii, ni wapi ambako mwanadamu huenda kutafuta bahati ya maisha? Ni wapi ambako mtu ataenda kupata hatima ya maisha yake? Mwanadamu, akiwa amekanyagwa chini ya miguu ya Shetani kwa muda mrefu, amekuwa tangu mwazo mwigizaji akitenda kwa mfano wa Shetani—hata zaidi, kuwa na mwili wake, wakitumika kama shahidi wa kushuhudia kwa Shetani, kwa uwazi. Aina hii ya jamii ya binadamu, aina hii ya watu wachafu walioharibika tabia, na watoto wa aina hii wa familia hii ya binadamu potovu, inawezaje kuwa na ushuhuda kwa Mungu? Utukufu Wangu unatoka wapi? Mtu anaweza kuanza wapi kuongea juu ya shahidi Wangu? Kwa adui ambaye, baada ya kupotosha mwanadamu, anasimama dhidi Yangu, tayari amemchukua mwanadamu—mwanadamu ambaye niliumba kitambo sana na ambaye alikuwa amejawa na utukufu Wangu kuishi kulingana na Mimi—na kumchafua. Amepokonya utukufu Wangu, na yote ambayo imetia moyoni mwa mwanadamu ni sumu iliyojawa na ubaya wa Shetani, na maji ya matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Hapo mwanzo, Nilimuumba mwanadamu, yaani, Nilimuumba babu wa binadamu, Adamu. Alijaliwa na umbo na sura, mwenye kujawa na uhai, kujawa na nguvu ya maisha, na isitoshe, pamoja na utukufu Wangu. Hiyo ilikuwa ni siku tukufu Nilipomuumba mwanadamu. Baada ya hapo, Hawa alitengenezwa kutoka katika mwili wa Adamu, naye alikuwa pia babu wa binadamu, na hivyo watu niliowaumba walikuwa wamejazwa na pumzi Yangu na kujazwa na utukufu Wangu. Adamu kiasili aliumbwa kutoka kwa mkono Wangu na alikuwa akiwasilisha mfano Wangu. Hivyo maana ya asili ya “Adamu” ilikuwa kiumbe kilichoumbwa na Mimi, kilichojawa na nishati Yangu ya uhai, kilichojawa utukufu Wangu, kinacho sura na umbo, kinacho roho na pumzi. Alikuwa kiumbe wa pekee, aliyemilikiwa na roho, ambaye aliweza kuniwakilisha Mimi, kuwa na picha Yangu, na kupokea pumzi Yangu. Hapo mwanzo Hawa alikuwa mtu wa pili kujazwa na pumzi ambaye uumbaji wake nilikuwa nimeamuru, hivyo maana asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe ambaye angeendeleza utukufu Wangu, aliyejazwa na nguvu Zangu na zaidi ya hayo aliyejawa na utukufu Wangu. Hawa aliumbwa kutoka kwa Adamu, kwa hivyo alikuwa pia mfano Wangu, kwa maana yeye alikuwa mtu wa pili kuumbwa kwa mfano Wangu. Maana ya asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe hai, mwenye roho, mwili na mifupa, ushuhuda Wangu wa pili na pia mfano Wangu wa pili miongoni mwa mwanadamu. Walikuwa mababu wa wanadamu, hazina safi na ya thamani ya binadamu, na, kutoka awali, viumbe hai waliojaliwa na roho. Hata hivyo yule mwovu alikichukua kizazi cha mababu wa wanadamu na kukikanyaga na kukiteka nyara, kutosa ulimwengu wa binadamu katika giza totoro, na kuifanya kwamba kizazi chenyewe hakiamini tena katika uwepo Wangu. Kilicho cha chukizo zaidi ni kwamba, hata yule mwovu anapowapotosha watu na kuwakanyagia chini, anapokonya kwa ukatili utukufu Wangu, ushuhuda Wangu, nguvu Yangu Niliyowatolea watu, pumzi na maisha Niliyopuliza ndani yao, utukufu Wangu wote katika dunia ya binadamu, na damu yote ya roho ambayo nimetumia kwa mwanadamu. Mwanadamu hayupo tena katika mwanga, na amepoteza kila kitu Nilichompa, akiutupilia mbali utukufu ambao nimeutoa. Wanawezaje kukiri kwamba Mimi ndiye Bwana wa viumbe vyote? Wanawezaje kuendelea kuamini kuwepo Kwangu mbinguni? Wanawezaje kugundua udhihirisho wa utukufu Wangu duniani? Hawa wajukuu wa kiume na kike wanaweza kumchukua vipi Mungu ambaye mababu zao walimcha kama Bwana Aliyewaumba? Hawa wajukuu wenye kuhurumiwa “wamewasilisha” kwa ukarimu kwa yule mwovu utukufu, mfano, na vile vile ushahidi ambao Nilikuwa nimewatolea Adamu na Hawa, na pia maisha Niliyompa binadamu na ambayo ategemea ili kuwepo, na, bila kujali hata kidogo uwepo wa yule mwovu, amempa utukufu Wangu wote. Je, si hiki ni chanzo cha jina la “uchafu”? Jinsi gani aina hii ya mwanadamu , mapepo mabaya, aina hii ya maiti inayotembea, aina hii ya umbo la Shetani, na aina hii ya maadui Wangu zinaweza kumilikiwa na utukufu Wangu? Nitaumiliki tena utukufu Wangu, niumiliki ushuhuda Wangu ambao huwa miongoni mwa wanadamu na vyote vilivyowahi kuwa mali Yangu na Nilivyokuwa Nimewapa wanadamu hapo zamani—nitamshinda mwanadamu kikamilifu. Hata hivyo, unapaswa kujua, wanadamu Nilioumba walikuwa watu watakatifu na wenye mfano Wangu na utukufu Wangu. Hawakuwa wa Shetani, wala hawakukabiliwa na kukanyagwa kwake, bali walikuwa tu udhihirisho Wangu, walikuwa huru kutokana na dalili hata kidogo ya sumu yake. Na hivyo, Niliwajulisha wanadamu wote kwamba Ninataka tu kile kilichoumbwa na mkono Wangu, wale watakatifu ambao nawapenda na wasio wa mwingine yeyote. Aidha, Mimi nitakuwa na furaha nao, na kuwaona kama utukufu Wangu. Hata hivyo, Ninachotaka sio mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani, ambaye ni wa Shetani leo, ambaye si kiumbe Changu cha asili tena. Kwa sababu Ninanuia kuchukua tena utukufu Wangu katika dunia ya wanadamu, Nitashinda kikamilifu manusura waliobaki kwa wanadamu, kama ushahidi wa utukufu Wangu katika kumshinda Shetani. Mimi huchukua tu ushahidi Wangu kama udhihirisho wa nafsi Yangu, kama kusudi la starehe Yangu. Haya ndiyo mapenzi Yangu.


       Mwanadamu ameendelea kwa makumi ya maelfu ya miaka ya historia mpaka kufikia alipo leo. Hata hivyo, mwanadamu wa uumbaji Wangu wa asili kwa muda mrefu uliopita amezama katika upotovu. Tayari amecha kuwa kile Ninachotaka, kwa hivyo wanadamu, Ninavyowaona, hawastahili tena jina la uanadamu. Badala yake wao ni uchafu wa wanadamu, ambao Shetani amewateka nyara, maiti zilizooza zinazotembea ambamo Shetani huishi na huvalia. Watu hawaamini hata kidogo kuwepo Kwangu, wala hawakaribishi kuja Kwangu. Mwanadamu kwa shingo upande tu huyajibu maombi Yangu, na kwa muda anakubaliana nayo, na hashiriki kwa kweli katika furaha na huzuni za maisha pamoja na Mimi. Kwa vile wanadamu huniona Mimi kama Asiyeeleweka, bila ya kutaka wao hujifanya wanatabasamu Kwangu, kuleta namna ya kujidekeza kwa yule aliye na madaraka. Hii ni kwa sababu watu hawana ufahamu wa kazi Yangu, sembuse mapenzi Yangu kwa wakati wa sasa. Nitakuwa wazi na nyinyi nyote: Siku itakapofika, mateso ya mwanadamu yeyote ambaye huniabudu yatakuwa rahisi kubeba kuliko yenu. Kiwango cha imani yenu Kwangu hakiwezi, kwa hakika, kuzidi kile cha Ayubu—hata imani ya Mafarisayo Wayahudi inaishinda yenu—na hivyo, siku ya moto ikifika, kuteseka kwenu kutakuwa kali zaidi kuliko kule kwa Mafarisayo walipokemewa na Yesu, kuliko kwa wale viongozi 250 waliompinga Musa, na kuliko kulw kwa Sodoma chini ya moto mkali wa uharibifu wake. Musa alipougonga mwamba, na maji yaliyokuwa yametolewa na Yehova yakaruka, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Daudi alipocheza kinubi kwa kunisifu Mimi, Yehova—moyo wake ukiwa umejaa furaha—ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Ayubu alipowapoteza wanyama wake waliojaa kote milimani na mali nyingi sana, na mwili wake kujawa na majipu mabaya, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Alipoweza kusikia sauti Yangu, Yehova, na kuuona utukufu Wangu, Yehova, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Kwamba Petro aliweza kumfuata Yesu Kristo, ilikuwa ni kwa imani yake. Kwamba Alitundikwa misumari msalabani kwa ajili Yangu na kutoa ushahidi mtukufu, pia ilikuwa kwa imani yake. Yohana alipoona mfano wa utukufu wa Mwana wa Adamu, ilikuwa kwa imani yake. Alipoona maono ya siku za mwisho, yote yalikuwa zaidi kwa sababu ya imani yake. Sababu ya yanayodaiwa kuwa mataifa mengi yasiyo ya Kiyahudi kupata ufunuo Wangu, na yakajua kwamba Nimerudi katika mwili kufanya kazi Yangu miongoni mwa wanadamu, pia ni kwa sababu ya imani yao. Je si wote ambao wamepigwa na maneno Yangu makali na bado wanafarijiwa nayo, na ambao wameokoka—wamefanya hivyo kwa sababu ya imani yao? Wale wanaoamini Kwangu lakini bado hupitia mateso, je si pia wamekataliwa na dunia? Wale wanaoishi nje ya neno Langu, wakikimbia mateso ya majaribu, si wao wote wanazurura tu ulimwengu? Wao ni sawa na majani ya msimu wa kupukutika kwa majani yanayopeperuka hapa na pale, bila pahali pa kupumzika, sembuse neno Langu la kufutia machozi. Ingawa adabu na usafishaji wangu hauwafuati wao, je, wao si waombaji, wanaoelea kila mahali, ambao wakitangatanga katika mitaa iliyo nje ya Ufalme wa mbinguni? Je, dunia ni mahali pako pa mapumziko kweli? Je, unaweza kweli kupata tabasamu hata dhaifu ya kutosheleza kutoka kwa dunia kwa kuepuka adabu yangu? Je, unaweza kweli kutumia starehe zako za kidunia kuficha utupu ulio katika moyo wako usioweza kufichika? Unaweza kumdanganya mtu yeyote katika familia yako, ilhali huwezi kunidanganya Mimi kamwe. Kwa kuwa imani yako ni ndogo sana, mpaka wa leo huna uwezo wa kupata raha inayoletwa na maisha. Nakushauri: heri kutumia nusu ya maisha yako kwa ajili Yangu kwa dhati kuliko kuishi maisha yako yote katika hali hafifu na kujishughulisha kwa ajili ya mwili, kuvumilia mateso yote ambayo ni vigumu binadamu kuvumilia. Kuna faida gani ya wewe kujipenda sana na kuikimbia adabu Yangu? Kuna faida gani wewe kujificha kutoka kwa adabu Yangu ya muda mfupi tu, na mwishowe kupate aibu ya milele, na adabu ya milele? Mimi, kwa hakika, Simlazimishi yeyote kufanya mapenzi Yangu. Iwapo mtu kweli anayo nia ya kujiwasilisha kwa mipango Yangu yote, Sitamtendea vibaya. Lakini Nahitaji kwamba watu wote waamini ndani Yangu, kama vile Ayubu alivyoamini ndani Yangu, Yehova. Iwapo imani yenu inazidi ile ya Tomaso, basi imani yenu itapata pongezi Zangu, katika uaminifu wenu mtapata furaha Yangu, na hakika mtapata utukufu Wangu katika siku zenu. Hata hivyo, watu, wanaoamini katika dunia na wanaomwamini ibilisi, wamefanya mioyo yao kuwa migumu, kama vile halaiki za mji wa Sodoma, na chembe za mchanga zilizovumwa na upepo katika macho yao na sadaka kutoka kwa ibilisi zikiwa zimeshikiliwa vinywani mwao, akili zao zilizodanganywa tangu kitambo zimemilikiwa na yule mwovu ambaye ameipora dunia. Mawazo yao nusura yameporwa na ibilisi wa nyakati za kale. Na hivyo, imani ya mwanadamu imekwenda na upepo, na hawezi hata kuitambua Kazi Yangu. Anachoweza tu kufanya ni kujaribu nkwa unyonge kuvumilia au kuchambua kwa kukisia sana, kwa sababu kwa muda mrefu tayari amejawa na sumu ya Shetani.


       Mimi Nitawashinda wanadamu kwa sababu wanadanu waliumbwa na Mimi wakati mmoja na pia, kilicho cha ziada, wamefurahia vitu vyote karimu vya uumbaji Wangu. Lakini wanadamu pia wamenikataa Mimi, na nyoyo zao haziko na Mimi ndani yao, na wao huniona kama mzigo kwa uwepo wao, hadi kwa kiwango ambacho, wakiwa kwa kweli wameniona, watu bado wananikataa, na kukuna vichwa wakiwaza kila njia inayoweza kuwawezesha kunishinda Mimi. Watu huwa hawaniruhusu Mimi kuwachukulia kwa umakini au kuweka madai kali juu yao, wala hawanikubali huhukumu au kuadibu udhalimu wao. mbali na kuona hili kuwa jambo la kuvutia, wanakasirika. Na hivyo Kazi Yangu ni kuchukua mwanadamu ambaye hula, hunywa na kusherehekea Kwangu lakini hanijui na kumshinda. Nitawapokonya zana wanadamu, na kisha, Nikiwachukua malaika Wangu, Nikiuchukua utukufu Wangu Nitarejea kwenye makao Yangu. Kwa kuwa kile ambacho watu wamefanya kimenivunja moyo kabisa na kuitawanya kazi Yangu kwa vipande muda mrefu uliopita. Nanuia kuumiliki tena utukufu ambao yule mwovu ameiba kabla ya kuondoka kwa furaha, na kuwaacha wanadamu waendelee kuishi maisha yao, waendelee na “kuishi na kufanya kazi kwa amani na furaha,” na Mimi sitaingilia kati tena katika maisha yao. Lakini Mimi sasa Nanuia kikamilifu kuumiliki tena utukufu Wangu kutoka kwa mkono wa yule mwovu, kuurejesha ukamilifu wa utukufu Niliouumba ndani ya mwanadamu wakati wa kuumbwa kwa dunia, na kamwe tena kutotolea mwanadamu wa dunia. Kwa kuwa wanadamu hawajashindwa tu kuuhifadhi utukufu Wangu, bali pia wao wameugeuza kuwa mfano wa Shetani. Watu hawathamini kuja Kwangu, wala hawaiwekei thamani siku ya utukufu Wangu. Wao hawasherehekei kupokea adabu Yangu, sembuse kuwa tayari kuurejesha utukufu Wangu Kwangu. Wala hawako tayari kutupa mbali sumu ya yule mwovu. Wanadamu bado siku zote wananidanganya kwa njia ile ile ya zamani, bado wakivaa tabasamu za kung’aa na nyuso zenye furaha kwa njia ile ile ya zamani. Wao hawajui kina cha huzuni ambayo wanadamu watakabiliwa nao baada ya utukufu Wangu kuwaondoka, na hasa hawajui kwamba siku Yangu itakapokuja kwa wanadamu wote, watakuwa na wakati hata mgumu zaidi kuliko watu katika nyakati za Nuhu. Kwa maana wao hawajui giza iliyokuwepo Israeli wakati utukufu Wangu ulitoweka kwa kuwa mwanadamu husahau kunapokucha jinsi ilivyokuwa vigumu kupita katika giza la usiku wa manane. Jua linaporejea mafichoni tena na giza kumshukia mwanadamu, ataanza tena kuomboleza na kusaga meno yake gizani. Je, mmesahau, wakati utukufu Wangu ulipotoweka kutoka Israeli, ilivyokuwa vigumu kwa watu wake kuishi siku zao za mateso? Huu ndio wakati ambapo mnaona utukufu Wangu, na pia ndio wakati ambapo mnashiriki siku ya utukufu Wangu. Mwanadamu ataomboleza katikati ya giza wakati utukufu Wangu unapoondoka kutoka katika nchi chafu. Sasa ndio siku ya utukufu Ninapofanya kazi Yangu, na pia ndio siku ambapo Namwondoa mwanadamu kutoka kwa mateso, kwa kuwa sitapitia nyakati za uchungu na ugumu nao. Mimi Nataka tu ushindi kamili juu ya wanadamu na kumshinda kikamilifu yule mwovu wa wanadamu.


Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING