11 Oct

Kuhusu Maisha ya Petro


Petro ni mfano ambao Mungu aliutambulisha kwa wanadamu, na yeye ni mtu mashuhuri anayejulikana vizuri. Kwa nini mtu mnyonge kama huyo aliwekwa mahala kama mfano na Mungu na amesifiwa na vizazi vya baadaye? Bila shaka, ni wazi kwamba hili halitenganishwi na maonyesho yake na azimio lake la upendo kwa Mungu. Kuhusu wapi ambapo moyo wa Petro wa upendo kwa Mungu ulionyeshwa na kile ambacho uzoefu wake wa maishani ulivyokuwa kwa kweli, lazima turudi kwa Enzi ya Neema kutazama tena desturi za wakati huo, ili kumwona Petro wa enzi hiyo.


Petro alizaliwa katika nyumba ya kawaida ya wakulima wa Kiyahudi. Wazazi wake waliikimu familia yote kwa kufanya ukulima, naye alikuwa mzaliwa wa kwanza kati ya watoto wote; alikuwa na ndugu wanne. Bila shaka hii siyo sehemu muhimu ya hadithi ya kusimulia—Petro ni mhusika wetu mkuu tu. Alipokuwa na umri wa miaka mitano, wazazi wake walianza kumfunza kusoma. Wakati huo Wayahudi walikuwa wenye maarifa kabisa—walikuwa walioendelea sana katika mawanda kama vile kilimo, viwanda, na biashara. Chini ya athari ya aina hiyo ya mazingira ya kijamii, wazazi wote wawili wa Petro walikuwa wamepata elimu ya juu zaidi. Hata ingawa walitoka mashambani, walikuwa na jumla ya maarifa mengi kabisa, ikifananishwa na mwanafunzi wa kawaida wa chuo kikuu wa leo. Ni wazi kwamba kuzaliwa katika hali bora sana za kijamii kama hizo ilikuwa bahati nzuri ya Petro. Alikuwa mwenye akili sana na alielewa mambo mapya kwa urahisi. Baada ya yeye kuanza shule, katika masomo yake aliweza kufanya uamuzi kutoka kwa vitu vingine bila kuonekana kutumia juhudi zozote. Wazazi wake walijivunia kuwa na mwana stadi kama huyo, kwa hiyo walifanya kila juhudi kumkubalia kwenda shuleni, wakitumaini kwamba angefaulu, na angeweza kupata aina fulani ya cheo cha urasimu katika jamii ya wakati huo. Bila kutambua, Petro alikuza moyo wa kupenda kumjua Mungu, kwa hiyo alipokuwa na umri wa miaka kumi na minne na katika shule ya upili, alichoshwa na mtalaa wa Tamaduni za Wagiriki za Kale alizokuwa akijifunza, na hasa aliwadharau watu na vitu vya kubuni katika historia ya Kigiriki ya kale. Kuanzia wakati huo na kuendelea, Petro, ambaye alikuwa ameingia tu katika uchipukizi wa ujana wake, alianza kuchunguza maisha ya binadamu na kuwasiliana na jamii. Hakulipiza kujitahidi sana kwa wazazi wake na dhamiri kwa sababu aliona kwa dhahiri kwamba watu wote walikuwa wakiishi katika kipindi cha kujidanganya, na wote walikuwa wakiishi katika maisha yasiyo na maana, wakiharibu maisha yao wenyewe kwa ajili ya kushindania umaarufu na mali. Sababu iliyomchochea kuona hili ilihusiana hasa na mazingira ya kijamii aliyokuwa ndani. Kadri ambavyo watu wanakuwa na maarifa, ndivyo mahusiano ya kati ya watu wawili yanavyokuwa magumu zaidi kufahamika, na kadri ambavyo dunia za ndani za watu zinavyokuwa ngumu zaidi kufahamika, ndivyo panavyokuwa tupu zaidi mahali ambapo pana watu. Chini ya hali hizi, Petro alianza kutafuta habari kila mahali wakati wake wa ziada, na watu wa dini walikuwa katika idadi ya wengi wa wale aliotafuta habari kutoka kwao. Ilionekana kwamba alikuwa na hisia isiyo dhahiri moyoni mwake kwamba mambo yote yasiyotambulikana katika ulimwengu wa binadamu yangebainishwa katika ulimwengu wa dini, kwa hiyo alienda mara kwa mara katika sinagogi iliyokuwa karibu na nyumbani kwake ili kuhudhuria ibada ya kuabudu. Wazazi wake hawakujua kuhusu jambo hili, na kabla ya muda mrefu Petro, ambaye kila mara alikuwa na mwenendo na taaluma bora sana, alianza kuchukia kwenda shuleni. Chini ya uangalizi wa wazazi wake alimaliza shule ya upili kwa shida. Aliogelea hadi pwani kutoka katika bahari ya maarifa, akavuta pumzi kabisa, na tangu wakati huo na kuendelea hakuna aliyemfunza au kumwekea mipaka.


Baada ya yeye kumaliza shule alianza kusoma kila aina ya vitabu, lakini alipokuwa na umri wa miaka kumi na saba, bado alikosa uzoefu wa jamii. Baada ya kuhitimu na kuondoka shuleni, alijiruzuku kwa ukulima huku pia akitenga muda mwingi alivyoweza kusoma vitabu na kuhudhuria ibada za kuabudu za dini. Wazazi wake, ambao walijawa na tumaini kwake mara kwa mara waliilaani Mbinguni kuhusu “mtoto mwasi” huyu. Lakini licha ya hili, moyo wake ambao ulikuwa na njaa na kiu ya haki haungekomeshwa. Alipitia vipingamizi si haba katika uzoefu wake, lakini alikuwa na moyo wenye uroho, kwa hiyo alichipuka kama nyasi baada ya mvua kunyesha. Kabla ya muda mrefu “alibahatika” kukutana na watu wa kiwango cha juu katika ulimwengu wa dini, na kwa sababu moyo wake wa kuwa na hamu ulikuwa thabiti sana, aliwasiliana na watu hao zaidi na zaidi kwa kawaida na alitumia karibu muda wake wote miongoni mwao. Wakati ambapo alikuwa tu amezamishwa ndani ya furaha ya kuridhika kwake, aligundua ghafula kwamba miongoni mwa watu hao, wengi wao walikuwa na imani kwa maneno tu lakini hakuna kati yao aliyejitolea katika moyo wake. Na moyo wake mwadilifu, wa kweli, Petro angewezaje kuhimili pigo kama hilo? Aligundua kwamba karibu watu wote ambao aliwashughulikia walikuwa wanyama ndani ya mavazi ya binadamu—walikuwa wanyama wenye sura za binadamu. Wakati huo Petro alikuwa mnyofu sana, kwa hiyo mara nyingi aliwasihi kwa yakini, lakini ni vipi ambavyo watu wa dini wa hila, wajanja wangeweza kusikiliza kusihi kwa kijana aliyejawa na nguvu na bidii? Ni wakati huo ndipo Petro alihisi utupu wa maisha ya binadamu, na alipochukua hatua yake ya kwanza kuelekea katika hatua ya maisha, alishindwa…. Mwaka mmoja baadaye, alihama kutoka kwenye sinagogi na akaanza maisha yake ya kujitawala mwenyewe.


Baada ya Petro mwenye umri wa miaka 18 kupitia kipingamizi kimoja, alikuwa mkomavu na mstaarabu zaidi. Usungo wake wote wa ujana ulitoweka tu, na maasumu ya ujana na kutokuwa na hila alikokuwa nako kulizimwa bila huruma na kipingamizi hicho. Tangu wakati huo na kuendelea akaanza maisha kama mvuvi. Baada ya hilo, mtu angeweza kuona kwamba kulikuwa na watu juu ya mashua yake ya kuvua waliokuwa wakisikiliza alichokuwa akihubiri; alikuwa akivua ili kupata riziki na kuhubiri kotekote mahali hapo. Kila mtu aliyemhubiria alifadhaishwa na mahubiri yake kwa sababu alichozungumzia kilikubaliana sana na mioyo ya watu wa kawaida wakati huo. Watu wote walivutwa sana na uaminifu wake, na aliwafunza watu mara kwa mara kuwashughulikia wengine kwa yakini na kumwita Bwana wa mbingu na dunia na vitu vyote ndani ya kila kitu, na kutopuuza dhamiri zao na kufanya yale mambo yasiyo ya kupendeza, bali kumridhisha Mungu wanayempenda mioyoni mwao katika mambo yote…. Watu walivutwa sana mara kwa mara baada ya kusikiliza mahubiri yake. Wote walitiwa moyo naye na wangetokwa na machozi kwa uchungu mara kwa mara. Wakati huo, kila mtu aliyemfuata alikuwa na uvutiwaji sana naye. Wote walikuwa fukara, na kwa sababu ya athari za kijamii wakati huo, bila shaka alikuwa na wafuasi wachache; alikuwa pia mwenye kupatwa na mateso mara kwa mara kutoka kwa ulimwengu wa dini katika jamii ya wakati huo. Kwa sababu hii alikuwa akizunguka kote siku zote, na aliishi maisha ya upweke kwa miaka miwili. Alipata ujuzi mwingi sana katika miaka miwili hiyo ya matukio yasiyo ya kawaida, na alijifunza kiasi kikubwa sana cha mambo ambayo hakuwa ameyajua awali. Petro wakati huo alikuwa mtu tofauti kabisa na yule aliyekuwa katika umri wa miaka 14—ilionekana hawakuwa na chochote sawa. Katika miaka hiyo miwili alikutana na kila aina ya watu na aliona kila aina ya ukweli kuhusu jamii; tangu wakati huo na kuendelea alijiondoa polepole na kila aina ya kaida za dini kutoka kwa ulimwengu wa dini. Kwa sababu ya mwelekeo katika kazi ya Roho Mtakatifu wakati huo, aliathiriwa kabisa. Wakati huo Yesu pia alikuwa amefanya kazi kwa miaka kadhaa, kwa hiyo kazi yake pia iliathiriwa na kazi ya Roho Mtakatifu wakati huo, hata hivyo, bado hakuwa amekutana na Yesu. Kwa sababu hiyo, wakati ambapo alikuwa akihubiri, alipata vitu vingi ambavyo vizazi vya watakatifu havikuwa vimepata kamwe. Bila shaka, wakati huo alikuwa anafahamu kwa uchache kuhusu Yesu lakini hakuwa kamwe amepata nafasi ya kukutana na Yeye ana kwa ana. Alitumaini tu na kuwa na kiu ndani ya moyo wake ya kumwona mtu huyo wa mbinguni aliyezaliwa kwa Roho Mtakatifu.


Alikuwa anavua juu ya mashua yake wakati wa utusiutusi jioni moja (karibu na pwani ya Bahari ya Galilaya iliyotajwa wakati huo), na ingawa alikuwa na ufito wa kuvua mikononi mwake, alikuwa na mambo mengine katika mawazo yake. Nuru ya magharibi iliangaza juu ya maji kama dimbwi la damu ndani ya eneo pana na wazi la bahari. Nuru iliakisi juu ya uso mchanga wa Petro, tena mtulivu na thabiti, kana kwamba alikuwa amezama katika mawazo. Wakati huo upepo mwanana ulijitokeza, na akahisi papo hapo kwamba maisha yake yalikuwa ya ukiwa, na hivyo ghafula alipitia hisia ya huzuni. Maji ndani ya bahari yaliakisi nuru hiyo wimbi baada ya wimbi, na ilikuwa wazi kwamba hakuwa na moyo wa kuvua. Wakati ule ule alipokuwa amezama ndani ya mawazo ya kila aina ya mambo, ghafla alimsikia mtu nyuma yake akisema: “Simoni Myahudi, mwana wa Yona, siku za maisha yako ni za ukiwa. Je, utanifuata?” Petro aliposikia haya alipigwa na butwaa, na akaangusha ufito wa kuvua uliokuwa mikononi mwake, na punde ukazama chini ya maji. Petro alikurupuka kugeuka pande zote, na akamwona mtu amesimama ndani ya mashua yake. Alimtazama Yeye toka juu hadi chini: nywele Zake, zilining’inia juu ya mabega Yake, zilikuwa manjano kama dhahabu kidogo katika nuru ya jua na nguo Zake zilikuwa za rangi ya kijivu. Alikuwa wa kimo cha wastani na mavazi Yake yalikuwa ya mwanamume wa Kiyahudi kabisa. Katika nuru ya utusiutusi, nguo Zake za rangi ya kijivu zilionekana nyeusi kidogo, na uso Wake ulionekana kuwa na mng’ao kidogo. Petro alijitahidi kumwona Yesu mara nyingi lakini kila wakati hakuweza kufanya hivyo. Wakati huo aliamini ndani ya roho yake kwamba mtu huyo bila shaka alikuwa Yule mtakatifu katika moyo wake, kwa hiyo alisujudu katika mashua yake: “Yaweza kuwa Wewe ni Bwana ambaye amekuja kuhubiri injili ya ufalme wa mbinguni? Nimesikia kuhusu matukio Yako lakini sijawahi kukuona Wewe. Nimekuwa nikitaka kukufuata Wewe, lakini singekupata Wewe.” Yesu alikuwa tayari ametembea hadi kwa sehemu ya kuwekea mizigo ya mashua yake na Alikuwa Ameketi chini kwa utulivu. Akasema:[a] “Simama na uketi karibu na Mimi. Nimekuja kuwatafuta wale wanipendao Mimi kweli, na kueneza injili ya ufalme wa mbinguni. Naenda kila mahali kuwatafuta wale ambao ni wenye moyo mmoja na Mimi. Je, uko radhi?” Petro akajibu: “Lazima nimfuate yule ambaye ametumwa na Baba wa mbinguni. Lazima nimkubali yule ambaye ameteuliwa na Roho Mtakatifu. Kwa vile nampenda Baba wa mbinguni, ningewezaje kukosa kuwa radhi kufuata?” Ingawa dhana za dini ndani ya maneno ya Petro zilikuwa thabiti sana, Yesu alitabasamu na kuashiria kwa kichwa Chake kwa ridhaa. Wakati huo, hisia ya upendo wa baba kwa Petro ilikua ndani Yake.


Petro alimfuata Yesu kwa miaka kadhaa na aliona mambo mengi ndani ya Yesu ambayo watu hawana. Baada ya kumfuata Yeye kwa mwaka mmoja, aliteuliwa na Yesu kama mkuu wa wanafunzi kumi na wawili. (Bila shaka hili lilikuwa jambo la moyo wa Yesu, na watu hawakuweza kabisa kuliona.) Kila kitendo cha Yesu kilikuwa mfano kwake katika maisha yake, na mahubiri ya Yesu yaliwekwa hasa katika kumbukumbu ndani ya moyo wake. Alikuwa mwenye busara sana na wa kujitolea kwa Yesu, na kamwe hakuwa na malalamiko kumhusu Yesu. Hii ndiyo maana alikuwa mwandani mwaminifu wa Yesu popote Alipoenda. Petro alichunguza mafunzo ya Yesu, maneno Yake yasiyo makali, na kile Alichokula, Alichovaa, maisha Yake ya kila siku, na safari Zake. Alifuata mfano wa Yesu katika kila njia. Hakuwa wa kujidai, lakini alitupa vitu vyake yote vya awali vilivyopitwa na wakati akafuata mfano wa Yesu katika maneno na matendo. Ni wakati huo ndipo alihisi kwamba mbingu na dunia na vitu vyote vilikuwa ndani ya mikono ya Mwenyezi, na kwa sababu hii hakuwa na chaguo lake mwenyewe, lakini alichukua kila kitu ambacho Yesu alikuwa ili kiwe mfano wake. Angeweza kuona kutoka kwa maisha yake kwamba Yesu hakuwa wa kujivuna katika kile Alichofanya, wala Hakujigamba kuhusu Mwenyewe, lakini badala yake, Aliwavuta watu na upendo. Katika hali mbalimbali Petro angeweza kuona kile ambacho Yesu alikuwa. Hiyo ndiyo maana kila kitu ndani ya Yesu kilikuwa chombo ambacho Petro alikifuata kama mfano. Katika uzoefu wake, alihisi kupendeza kwa Yesu zaidi na zaidi. Alisema kitu kama hiki: “Nilimtafuta Mwenyezi katika ulimwengu na nikaona maajabu ya mbingu na dunia na vitu vyote, na hivyo nilikuwa na hisi kuu ya kupendeza kwa Mwenyezi. Lakini sikuwa kamwe na upendo halisi ndani ya moyo wangu, na sikuona kamwe kupendeza kwa Mwenyezi kwa macho yangu mwenyewe. Leo, katika macho ya Mwenyezi, nimetazamwa na fadhila na Yeye na hatimaye nimehisi kupendeza kwa Mungu, na hatimaye nimegundua kwamba kwa Mungu, siyo tu kuumba vitu vyote ambavyo vingewafanya wanadamu wampende Yeye. Katika maisha yangu ya kila siku nimepata kupendeza Kwake kusiko na kikomo; ni vipi ambavyo ingewezekana kuwekewa mipaka tu katika hali hii leo?” Muda ulipopita, vitu vingi vya kupendeza vilipatikana pia ndani ya Petro. Alikuwa mtiifu sana kwa Yesu, na bila shaka alipitia hasa vipingamizi vingi kwa kiasi fulani. Wakati ambapo Yesu alimpeleka katika sehemu mbalimbali kuhubiri, yeye alijinyenyekeza kila mara na kuyasikiliza mahubiri ya Yesu. Hakuwa kamwe mwenye kiburi kwa sababu ya miaka yake ya kufuata. Baada ya Yesu kumwambia kwamba sababu ya Yeye kuja ilikuwa kusulubiwa ili kuimaliza kazi Yake, alikuwa na huzuni sana mara kwa mara na angetokwa na machozi akiwa pekee yake kisiri. Hata hivyo, siku ile “ya kusikitisha” ilifika. Baada ya Yesu kushikwa, Petro alitokwa na machozi pekee yake juu ya mashua yake ya kuvua na akaomba kiasi kikubwa kuhusu jambo hili, lakini ndani ya moyo wake alijua kwamba yalikuwa mapenzi ya Mungu Baba na hakuna ambaye angeyabadilisha. Yeye alikuwa akihuzunika na kutokwa na machozi siku zote kwa sababu ya athari ya upendo—bila shaka, huu ni udhaifu wa binadamu, kwa hiyo wakati ambapo alijua kwamba Yesu angepigiliwa misumari msalabani, alimuuliza Yesu: “Baada ya Wewe kuondoka Utarudi kuwa miongoni mwetu na kutuchunguza? Je, bado tutaweza kukuona Wewe?” Ingawa maneno haya yalikuwa manyofu kabisa, na pia yalikuwa yamejawa na fikira za binadamu, Yesu alijua ladha ya mateso ya Petro, kwa hiyo kupitia upendo Wake alikuwa mwenye huruma kuhusu udhaifu wake: “Petro, Nimekupenda wewe. Je, wajua hilo? Ingawa hakuna maana katika kile usemacho, Baba ameahidi kwamba baada ya kufufuka Kwangu, Nitaonekana kwa wanadamu kwa siku 40. Je, huamini kwamba Roho Wangu atatoa neema juu yenu mara kwa mara?” Baada ya hilo Petro alikuwa na faraja kiasi kidogo, lakini alihisi kila mara kulikuwa na kipingamizi katika kile ambacho kilikuwa kamili kwa upande mwingine. Kwa hiyo, baada ya Yesu kufufuliwa, Alionekana kwake wazi kwa mara ya kwanza, lakini ili kumzuia Petro kuendelea kushikilia fikira zake, Yesu alikataa chakula kingi mno ambacho Petro alikuwa amemwandalia Yeye na akatoweka kufumba na kufumbua macho. Wakati huo Petro hatimaye alikuwa na ufahamu wa kina kuhusu Yesu, na akampenda Bwana Yesu hata zaidi. Baada ya kufufuka Kwake, Yesu alimwonekania Petro mara kwa mara. Baada ya siku 40 wakati ambapo Alipaa mbinguni, Alimwonekania Petro mara tatu. Kila wakati ambapo Yeye alionekana ulikuwa wakati ambao kazi ya Roho Mtakatifu ilikuwa karibu kukamilishwa na kazi mpya ilikuwa karibu kuanzwa.


Petro alipata riziki kwa kuvua kotekote katika maisha yake yote, lakini hata zaidi, aliishi kwa ajili ya kuhubiri. Katika miaka yake ya baadaye, aliandika waraka wa kwanza na wa pili wa Petro, na aliandika barua kadhaa kwa kanisa la Filadelfia la wakati huo. Watu wakati huo walivutwa sana na yeye. Hakuwahubiria watu kamwe kwa kutegemea sifa zake mwenyewe, bali aliwapa ruzuku ya kufaa ya uzima. Katika maisha yake, hakusahau kamwe mafunzo ya Yesu wakati wa maisha Yake—alisalia kutiwa moyo. Wakati ambapo alikuwa akimfuata Yesu aliamua kuulipiza upendo wa Bwana kwa kifo chake na kwamba angefuata mfano wa Yesu katika vitu vyote. Yesu alimuahidi hili, kwa hiyo wakati ambapo alikuwa na umri wa miaka 53 (zaidi ya miaka 20 baada ya kuachana na Yesu), Yesu alionekana kwake kutambua azimio lake. Katika miaka saba ya kufuata jambo hilo, Petro alitumia maisha yake katika kujijua. Siku moja miaka saba baadaye, alisulubiwa juu chini, kukakomesha maisha yake yasiyo ya kawaida.

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 


Soma Zaidi: Nini maana ya uzima wa milele? Kutokao uzima wa milele ni wapi? Sisi Wakristo tunafaa kutafuta vipi ili tuweze kupata uzima wa milele? Yaliyomo katika sehemu hii yatajibu maswali yako.

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING