03 Oct
1. Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Sura ya 2 Ukweli wa Majina ya Mungu

1. Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?


Maneno Husika ya Mungu:

Je, Jina la Yesu “Mungu pamoja nasi,” linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru! Je, unaamini kwamba jina la Yesu, Mungu pamoja nasi, linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu? Mungu Anaweza kuitwa majina mengi, lakini baina ya majina haya mengi, hamna moja ambalo linaweza kujumlisha yote ambayo Mungu Anamiliki, na hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu. Na hivyo Mungu Ana majina mengi, lakini majina haya mengi hayawezi kuelezea tabia ya Mungu kikamilifu, kwa kuwa tabia ya Mungu ni tajiri sana, na inapita maarifa ya mwanadamu. Lugha ya mwanadamu haina uwezo wa kumfafanua Mungu kwa ukamilifu. Mwanadamu ana msamiati finyu tu ambao anaweza kufafanua yote anayojua kuhusu tabia ya Mungu: kubwa, yenye heshima, ya ajabu, isiyoeleweka, kuu, takatifu, yenye haki, yenye hekima, na kadhalika. Maneno mengi sana! Msamiati kama huo finyu hauwezi kuelezea kile kidogo mtu ameshuhudia juu ya tabia ya Mungu. Baadaye, watu wengi waliongeza maneno zaidi ili kueleza vizuri zaidi ari ndani ya mioyo yao: Mungu ni mkuu sana! Mungu ni mtakatifu sana! Mungu ni wa kupendeza sana! Leo, maneno kama haya yamefikia kilele chake, lakini bado mwanadamu hawezi kujieleza wazi wazi. Na kwa hiyo, kwa mwanadamu, Mungu ana majina mengi, lakini Hana jina moja, na hilo ni kwa sababu nafsi ya Mungu ni ya ukarimu sana, na lugha ya mwanadamu haitoshi sana. Neno au jina moja maalum halina uwezo wa kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake. Kwa hivyo, je, Mungu Anaweza kuchukua jina moja lisilobadilika? Mungu ni mkuu sana na mtakatifu, kwa hivyo mbona wewe huwezi kumruhusu Yeye abadili jina Lake katika kila enzi mpya? Kwa hivyo, katika kila enzi ambayo Mungu binafsi hufanya kazi yake mwenyewe, Yeye hutumia jina ambalo linafaa enzi hiyo ili kujumlisha kazi ambayo anaifanya. Yeye hutumia hili jina haswa, ambalo linamiliki umuhimu wa wakati, kuwakilisha tabia yake katika enzi hiyo. Mungu hutumia lugha ya mwanadamu kuelezea tabia yake mwenyewe. Hata hivyo, watu wengi ambao wamepata uzoefu wa kiroho na wamemuona Mungu binafsi bado wanahisi kuwa jina moja maalumu haliwezi kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake—ole wetu, hili linasikitisha, hivyo mwanadamu hamwiti Mungu kwa jina lolote, lakini humwita tu “Mungu.” Moyo wa mwanadamu unaonekana kujawa na upendo, lakini pia unaonekana kuzongwa na ukinzani, kwa maana mwanadamu hajui jinsi ya kumueleza Mungu. Kile Mungu alicho ni cha ukarimu sana, hakuna kabisa njia ya kukieleza. Hakuna jina moja ambalo linaweza kutoa muhtasari wa tabia Ya Mungu, na hakuna jina moja ambalo linaweza kuelezea yote ambayo Mungu anacho na Alicho. Kama mtu ataniuliza, “Ni jina gani hasa unalotumia?” Nitamwambia, “Mungu ni Mungu!” Je, hilo silo jina bora zaidi la Mungu? Je, huko sio kufafanua bora zaidi kuhusu tabia ya Mungu? Basi kwa nini mtumie juhudi nyingi sana kutafuta jina la Mungu? Kwa nini ufikirie sana, kukaa bila kula na kulala, kwa ajili ya jina? Siku itawadia ambapo Mungu hataitwa Yehova, Yesu, au Masihi—Yeye Ataitwa tu Muumba. Wakati huo, majina yote ambayo Alichukua hapa duniani yatafikia kikomo, kwa kuwa kazi yake hapa duniani itakuwa imefika mwisho, na baada ya hapo Mungu hatakuwa na jina. Wakati mambo yote yatakuja kuwa chini ya utawala wa Muumba, kwa nini umwite kwa jina sahihi ila bado halijakamilika? Je, bado unatafuta jina la Mungu sasa? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaitwa tu Yehova? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaweza tu kuitwa Yesu? Je, unaweza kubeba dhambi ya kumkufuru Mungu? Unapaswa kujua kuwa Mungu mwanzoni hakuwa na jina. Yeye Alichukua tu jina moja, au majina mawili, ama majina mengi kwa sababu Alikuwa na kazi ya kufanya na Alikuwa na jukumu la kumsimamia mwanadamu. Jina lolote ambalo anaitwa Yeye, je, si lile analolichagua kwa hiari yake? Je, Yeye anakuhitaji wewe, kiumbe, kuamua jina lake? Jina ambalo Mungu Anaitwa ni kwa mujibu wa kile ambacho mwanadamu anaweza kufahamu na lugha ya mwanadamu, lakini hili jina haliwezi kujumlishwa na mwanadamu. Wewe unaweza kusema tu kuwa mbinguni kuna Mungu, ya kwamba Yeye anaitwa Mungu, na kwamba Yeye mwenyewe ni Mungu mwenye nguvu nyingi, busara tele, wakuinuliwa sana, wa ajabu kuu, mwenye siri kuu, mwenye uweza mkuu sana, na huwezi kusema mengi zaidi; hayo ndiyo yote unayoyajua. Kwa njia hii, je, jina la Yesu tu linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe? Wakati siku za mwisho zitawadia, ingawa ni Mungu ndiye anafanya kazi yake, ni sharti jina lake libadilike, kwa kuwa ni enzi tofauti.

kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi. “Yesu” linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, nao usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hiyo ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nililichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, nalo si jina ambalo kwalo Nitawaangamiza wanadamu wote. Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza kwa ufasaha tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitatamatisha enzi nzima.

kutoka katika “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING